Mwanaume Hana Moods

Dena mpenzi sijakuelewa yani huwa haongelesheki baada ya kutibuana au ni masaa yote yuko hivo
 
Wapendwa MMU habari zenu nimewamiss mjue? Mimi nashida na shida iko kwa my huby ana mood mbaya plz help haongelesheki kamwe! (msinitukane tafadhali nawaomba)

hatuwezi kufanya hivyo Dena jamani........
huyo we mwache usimuulize mpaka moods zake ziishe.....
hiyo huwa inatokea......
 
Mpendwa, huwezi kushambuliwa unless mume kanuna mara ya kwanza tu unauliza kwa kumkashifu. Kama ni kitu umejaribu kupata suluhisho ukashindwa tunafurahi kushirikiana nawe (Dr Mbu anakuja sasa hivi,lol)
DA, especially kwa wanaume na baadhi ya wanawake huwa wanahitaji 'hibernation' .

Kama sio wakati mwingi, wewe mpotezee tu. Akiwa na mood hiyo muambie tuangalie movie ili mkae kimya tu na kucheka, or else jiingize kwenye shughuli ya kupanga ama usafi.

Kama anatumia muda mwingi kwenye mood, msubiri wakati yuko kwenye mood nzuri afu uanze kumuibia kwa style ya MJ1, "mpenzi, sometimes unakua na moods and it feels like u ar nt here with me. I miss u wakati ukiwa kwenye mood. I understand unahitaji muda wa kutafakari na kuwa kimya lakini nahisi kama unanipunja mie muda wa kuwa na ww.

Is there something I or we can do to improve this? ww ni rafiki yangu na tunaweza kuongea lolote, mazuri hata mabaya pia..", usisahau ka-juice na his fav meal ishakua tumboni teh teh.

swali la msingi: zamani alikua hivyo ama ni badiliko la ghafla? pole sana,i know it is very disturbing.
 
Pole Sana Dena, i guess muache tu kwanza akitulia i guess he will come back to his senses
 
....Dena,

mara nyingi hiyo ni kiashiria kwamba kuna jambo/mambo linalomkera ambalo kila akikwambia unapinga,
au unamkatisha anapokuwa anaongea, au una react tofauti (ujeuri?) na yeye anavyokuelewa.

kwakuwa "unashindwa" kukubaliana na mtazamo wake, anajionea bora kukaa kimya kuliko muendelee kugombana.
Chunguza; mara nyingi atakuwa keshakwambia humsikilizi, unabisha kila kitu, unadhani unajua kila kitu, au katika maneno kama hayo..

pole mama jichunguze na wewe wapi unapomkwaza ujirekebishe, "mgomba huo, palilia..!"

Fanya hivi, Panga siku wiki hii, Ingia jikoni wewe mwenyewe(sio beki tatu) umpikie chakula kizuri akipendacho, pale chumbani ktk kitanda chenu tandika shuka zuuri katikati ya kitanda weka zawadi kwa ajili yake(either perfume aipendayo,boxer,maua etc etc), lengo akiingia tu room akutane nayo, siku hiyo usiku sasa vaa gauni ambalo hajawahi kukuona nalo, ambalo litamtia wazimu tu. .....................(reserved)............
Then baadae utamuuliza whats wrong, kama umegundua ulimkosea muombe msamaha.
 
Dena hizi moods zilikuwepo tangu mwanzo wa mahusiano yenu?
Kama jibu ni hapana basi jichunguze na wewe kama alivyosema Mbu
Kama huna makosa (yaani unashindwa kulink matendo, maneno na tabia zako) na moods zake basi angalia na pembeni maana inawezekana pia amependa kwingine na wewe anakuona kama kizibio cha furaha yake ya kuwa na ampendaye ni vile tu nd hivyo tena haweziondoka/kukuacha/tengua ndoa.
 
...hapana mwanajamiione,...hapo kwenye red wanaume hatupo hivyo...
mwanaume anapokuwa na alternative, huwa hanuni hata siku moja...ni ujeuri kwa kwenda mbele.
 
Fanya hivi, Panga siku wiki hii, Ingia jikoni wewe mwenyewe(sio beki tatu) umpikie chakula kizuri akipendacho, pale chumbani ktk kitanda chenu tandika shuka zuuri katikati ya kitanda weka zawadi kwa ajili yake(either perfume aipendayo,boxer,maua etc etc), lengo akiingia tu room akutane nayo, siku hiyo usiku sasa vaa gauni ambalo hajawahi kukuona nalo, ambal litamtia wazimu tu. .....................(reserved)............
Then baadae utamuuliza whats wrong, kama umegundua ulimkose muombe msamaha.
Kivumah Finest shahidi nampikia namfanyia yote but mood haziishi
 
Dena hizi moods zilikuwepo tangu mwanzo wa mahusiano yenu?
Kama jibu ni hapana basi jichunguze na wewe kama alivyosema Mbu
Kama huna makosa (yaani unashindwa kulink matendo, maneno na tabia zako) na moods zake basi angalia na pembeni maana inawezekana pia amependa kwingine na wewe anakuona kama kizibio cha furaha yake ya kuwa na ampendaye ni vile tu nd hivyo tena haweziondoka/kukuacha/tengua ndoa.
Asante my dear
 
Mdogo wangu The Finest, hapo kwenye Gubu la mume acha kabisa.....mara mia la wifi nakwambia!
Hahaha!!! Lol....mimi huwa naamini kila mtu ana Mood na Mood huwa zinaisha sasa hii inawezekana sio Mood tena bali GUBU....umenikumbusha kuna mdada mmoja alianiambia kama wewe kuwa mwanaume mwenye GUBU ni balaa kupita maelezo hata ufanye zuri lipi kwake ni baya kwenda mbele
 
Back
Top Bottom