Mwanaume Hana Moods

Aseeee!!
Duh!!
Mpendwa, huwezi kushambuliwa unless mume kanuna mara ya kwanza tu unauliza kwa kumkashifu. Kama ni kitu umejaribu kupata suluhisho ukashindwa tunafurahi kushirikiana nawe (Dr Mbu anakuja sasa hivi,lol)
DA, especially kwa wanaume na baadhi ya wanawake huwa wanahitaji 'hibernation' .

Kama sio wakati mwingi, wewe mpotezee tu. Akiwa na mood hiyo muambie tuangalie movie ili mkae kimya tu na kucheka, or else jiingize kwenye shughuli ya kupanga ama usafi.

Kama anatumia muda mwingi kwenye mood, msubiri wakati yuko kwenye mood nzuri afu uanze kumuibia kwa style ya MJ1, "mpenzi, sometimes unakua na moods and it feels like u ar nt here with me. I miss u wakati ukiwa kwenye mood. I understand unahitaji muda wa kutafakari na kuwa kimya lakini nahisi kama unanipunja mie muda wa kuwa na ww.

Is there something I or we can do to improve this? ww ni rafiki yangu na tunaweza kuongea lolote, mazuri hata mabaya pia..", usisahau ka-juice na his fav meal ishakua tumboni teh teh.

swali la msingi: zamani alikua hivyo ama ni badiliko la ghafla? pole sana,i know it is very disturbing.
 
Hapo tu ndio kina mama huwa mnachemsha. Mtu akishakuwa kimya akitafakari mambo ya familia basi inakuwa ishu. Mara baba fulani unaumwa? hapana. Umekasirika? hapana. Mbona uko kimya? Kuna mambo natafakari? Mambo gani unatafakari? naomba muda ni tafakari mwenyewe nitakujulisha? Au nimekuudhi? Hapana? Sasa kwa nini hutaki kuniambia kinachokufanya uwaze? nimesema naomba muda nitafakari wewe hauhusiki? Kwa nini sihusiki wakati mimi ni mke wako? Au huniamini ndio maana hutaki kuniambia kinachokupa mawazo? Bwana eee *&@##...........**&^^^&. Yaani ni maswali kwenda mbele mpaka sasa inakuwa kero.

Ushauri wa bure kwa kina mama: Lazima ujue behaviour ya mwanaume. Sisi hatuna kawaida ya kumweleza kila mtu yanayotusibu na ni mara chache sana kukuta mwanaume anaongea mambo ya ndani kwake kwa marafiki ama kwenye vijiwe/bar. Na kabla hujaanza kimweleza mtu inabidi utafakari kama kwa kufanya hivyo unajenga au kubomoa. Na kuna vitu vingi huwa tunaamua kuvificha vifuani kwa maslahi ya wanawake zetu na watoto. Hivyo ukiona mwanaume yuko kimya anawaza au kutafakari mpe muda amalize mambo yake sio unaanza kuingilia kati kwa maswali na kutaka kugeuza suala zima kuwa ni kati yako na yeye. Siyo kila mara anapowaza ina maana ni wewe ndiye chanzo. Kuna vyanzo vingi vya stress na wakati mwingine siyo busara sana kuvisema.
 
Dena Amsi, hujambo dada yangu? mimi nataka kujua tu sababu hapa ulipata ushauli wa kila aina. Je mwanaume kasharudisha mood? sasa hivi mambo yanaendeleaje? Mia
 
Back
Top Bottom