Mwanaume awapa sumu watoto wake watatu na wote wamefariki

enzo1988

JF-Expert Member
May 26, 2018
732
2,874
Tukio la kusikitisha na la kinyama limetokea katika kijiji cha Lusanga ambacho kinapatikana katika wilaya ya Mvomero tarafa ya Turiani.

Tukio lenyewe:
Katika tukio hilo mwanaume ameamua kuwapa sumu watoto wake watatu ambao wote wamefariki. Muhusika aliamua kujitoa uhai wake lakini hakufanikiwa. Muhusika amelazwa katika hospitali ya Bwagala.

Sababu:
Sababu kuu iliyopelekea unyama huu ni mapenzi kwani muhusika alikuwa akimbembeleza mama watoto wake warudiane kwani aliondoka kutokana na ugomvi. Mama watoto alikataa kwani alitaka waoane ,ndipo baba watoto akachukua uamuzi wa kuwanywesha sumu inayoua na kuteketeza magugu.

Mazishi:
Mazishi yamefanyika usiku huu ( Saa tatu usiku) katika kijiji cha Lusanga tarehe 27-11-2018.
Dah!! Mapenzi yana nguvu lakini siyo kwa unyama na ukatili huu.


Chanzo: Mimi mwenyewe.


Nb: Kwa maadili siwezi kuweka picha zao hapa mtandaoni, kwani ni watoto wadogo. Mmoja ana miezi tisa kuelekea kumi mwingine chekechea na mkubwa darasa la kwanza.
 
.*...alikuwa akimbembeleza mama watoto wake warudiane.....
mama watoto alikataa kwani alitaka waoane.....*

Sijaelewa hapa Mkuu.

Pole kwa Ndugu wa karibu na pole baba kwa kutokufa.
 
Kalogwa si bure.
Wababa huwa wanalinda watoto wao sana. sijui huyo baba ni wa wapi
Screenshot_20181127-225800(1).jpeg
12%20black%20little%20girl%20smiling%20while%20dad%20bends%20to%20hug%20her_3.jpeg
 
so sad...RIPs little kids...
Note:zaidi ya nguruwe sijawahi kusikia mnyama anaeua watoto wake so nadhani litafutwe neno mbadala la kinyama
 
.*...alikuwa akimbembeleza mama watoto wake warudiane.....
mama watoto alikataa kwani alitaka waoane.....*


Sijaelewa hapa Mkuu.

Hawakufunga ndoa. Walikuwa wanaishi pamoja tu. Ndiyo maana nimetumia 'mama watoto' na siyo mke.
 
Hii taarifa mbona ina ukakasi??..

Alimbembeleza mama watoto arudi, akakataa kurudi, mpaka waoane

mazishi yamefanyia usiku, kwanini??
 
Hakuna jipya chini ya jua Bandugu wala hkna dhambi mpya tunayarudia2 yaliyokwisha tendwa MAGDA GAOBBELS mke wa katbu mwenezi wa Hitler JOSEPH GAOBBELS aliwanywesha sumu watoto wake6 kabla ya yeye na mumewe kijilipua na kuacha Barua kua wanamfata THE FUHRER
 
Huyo mama aliondoka na kuwaacha watt wake nyuma??kama ndiyo huyo ni mama mpuusi wa karne,kama alikuwa hana uwezo wa kuondoka nao angelikaa kwa mumewe maana inaonekana bado mumewe alikuwa anamhitaji
 
Huyo mama aliondoka na kuwaacha watt wake nyuma??kama ndiyo huyo ni mama mpuusi wa karne,kama alikuwa hana uwezo wa kuondoka nao angelikaa kwa mumewe maana inaonekana bado mumewe alikuwa anamhitaji
Huwenda alikimbia kipigo usiku Sasa angewezane kuwabeba watoto wake jamaaa?
 
Back
Top Bottom