Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Pole man .... Ingawa sijamuona mwanao thats sounds like typical chronic otitis media a.k.a middle ear infection ipo hivi katika ear canal kabla hujafikia ngoma kuna lil bastards "bacteria" wamefanya inflammation .. nime suspect hii bcz huwa ni common kwa watoto .. nakama hiyo pus inayotoka ni ya njano thn i might be right . nenda kwambie doc. wake .. jaribu ku suggest tu ask him "doc could be otitis media?" do not make conclusion maana ma doc wengine visirani. soma zaidi hapa Otitis Media (Middle

N;B- jitahidi anapokoga ama anapoogeshwa maji yasiingie sikioni..

wakati unatafuta tiba fanya hivi .. msafishe sikio "kwa pamba sio maji epuka maji ndani ya sikio", then weke dawa fulani inaitwa mupirocin ointment cheki picha hapa ni anti bacterial atumie asubuhi na jioni wakati unaiweka unatumia zile pamba za kutoa nta masikioni . kamulia dawa katika ile pamba ya mbele ipake kwa style ambayo inakaa katika kuta za middle ear sababu infection ipo katika kuta zamiddle ear sio ndani kwenye ngoma, baada ya nusu saa muweke ear drops. ofloxin ear drops cheki image hapa

kwa masaada zaidi fanya haraka nenda kwa dactari... suggest to him about otitis media
 
DR OLE WA EKENYWA CLINIC mwembechai nyuma ya sopco petrol station,ni kiboko wa wagonjwa wote niliwapeleka kwa matibabu tatizo halikuridia tena!
 
hilo tatizo je ulikuwa wakati anatumia antibiotic unamsafisha hilo sikio kwa kutumia zile pamba za masikio inasaidia sana huku anatumia dawa nawewe unamfanyia usafi asubuhi mchana na jioni na hico kipamba unatubukiza kwenye maji ya vuguvugu kabla hujamsafisha nacho

Doctor wa masikio alituonya tusimsafishe mtoto sikio na zile pamba. Nenda hospital watamsafisha once a week akipona usijaribu hata siku moja kumsafisha sikio. Sikio linajisafisha lenyewe. Ukizoea kuweka pamba unakuwa addicted na unajikuta unasikia raha tuu vicious cycle.
 
Chukua karafuu afu changanya na mafuta ya naz chemsha pamoja,then muonye ckio,afu utakuwa unamdondoshea ktone kmoja mara 3 kwa cku!dawa no 2 kuna maua fulan yana majan mapana ka kiganja cha m2 mzma manene, nayo ni dawa nimeyasahau jina, unachoma kwenye moto, afu unamkamulia vijimaji vile mtoto ile usimkamulie vkiwa vya moto sana.
 
Anaitwa OLE LENGINE (MASAI) Hospitali yake iko pale Magomeni (EKENYWA DISPENSARY), I recommend that too. Achana na mambo ya muhimbili watakupotezea. Nenda pale asubuhi sana ukafanye appointment ili ukutane naye jioni ya saa tisa.

Mwenyezi akutie nguvu mtoto apate nafuu haraka. Siku ziingine ukiona mtoto ana maumivu makali shika sehemu inayouma anza kuomba kwa hisia blv me utaona changes.

All the best!
 
Hodi jamvini!
Nina sumbuliwa na masikio tangu 2003, sikio langu la kushoto linatoa milio isiyozimika toka mwaka 2003 na pia usikivu wake ni hafifu sana. La kulia nalo usikivu wake ni wastani na huwa kama lina geuka kwa ndani na kusabibisha kutokusikia. Kwa mfano, kama nikimeza chakula, au kupiga chafya.

Nimeshazunguka hospitali zote kubwa hapa Dodoma na mikoani, nimetumia dawa za maji na vidonge but sijapata hata nafuu. Nimeshatumia dawa za wachina hospital ya mkoa wa dodoma hazijasaidia. Nilishaenda Muhimbili (ENT) wakasema kuna mishipa ya fahamu masikioni kama imesinyaa, wakanipa Hearing aid lakini badala ya kunisaidia ikawa inaua zaidi usikivu pindi nikikivua.

Nimenda KCMC (ENT) wakanichunguza wamekuta masikio ni mazima, hayajatoboka, hakuna bakteria ila wakanipa dawa wakisema kuwa kuna kama compresion ndani ya masikio. Wakanipa dawa za vidonge nimetumia ila tatizo bado kupona.
Masikio hayatoi usaha wala uchafu wowote, pia hayaumi.

Hali hii imeninyima amani katika nafsi yangu kwa muda mrefu sasa. Naamini hapa jamvini wako wataalam wa afya wanaweza kunipa jibu la kuondokana na hii hali. Wajameni napata wakati mgumu sana hasa wakati nafanya Oral interview.

Any kind of help please.
--------

Pia soma:
Kuna mtoto ana miaka mitano sasa, mtoto alikuwa mbunifu, mwenye maswali sana, sasa amepata tatizo!

mwanzo alikuwa anasikia vizuri, lakini ametokea kuwa anapoteza uwezo wa kusikia vizuri, ili akusikie lazima awe karibu yako, akiwa mbali hasikii, ingawa masikio hayana usaha.

Nilimpeleka hospitali zetu za kiswahili, akapimwa na akaandikiwa dawa, tena za bei ghali nilizinunua akazitumia wala hazikumpa nafuu yoyote.

Wasamalia wema waliponisikia nikilalama juu ya tatizo hilo walinishauri kumpa amoxiline na dawa ya matone ya kudondoshea, (ingawa siikumbuki jina) ile dawa ilimsaidia akawa anasikia kwa kiasi fulani, lakini baada ya muda mfupi hali ile inarudi.

Naomba msaada wadau, ni dawa gani anatakiwa kupewa mtoto huyo?
 
Pole sana kwa tatizo hilo.
Kwa vile upo Dodoma, tafuta ofisi ya labor (kazi), uwaulize ofisi ya wakala wa afya na usalama kazini. Utakayemkuta mwambie tatizo lako. Nina wasiwasi tatizo lako linahusiana na kazi unayofanya, haswa kelele. Endapo utatokea kuwa Dar, ni-PM nikuelekeze ofisi ambayo utapewa msaada wa kutambua tatizo na kuelekezwa marekebisho/ rehabilitation.
 
Mkuu kuna vitu masikioni vinaitwa sensory hair hivi viko katika sikio la kati ni vingi sana. Hivi hufanya kazi ya kusafirisha mawimbi ama mirindimo ya sauti toka kwenye ngoma kwenda sikio la ndani lenye nerves za kupeleka kwenye ubongo.

Kwa mujibu wa maelezo yako inaonekana baadhi ya vitu hivyo (sensory hairs) vimekufa na vikishakufa haviwezi kufufuka kamwe na wala haviambukizi vingine zaidi bali hubaki kama makovu tu. Kwa hiyo ondoa hofu kuwa tatizo lako litaendelea kukua na kuwa kubwa zaidi.

Kuna sababu mbalimbali ambazo husababisha hizo sensory hairs kudhoofika au kufa kama vile, too much exposure to excessive noise. Mfano kelele za viwandani, viwanja vya ndege, stesheni za treni, madarasani, misituni (mfano kelele za ndege). Ila kuna case nyingi nyingi vilevile za matatizo hayo kusababishwa na lishe na upungufu/ ukosefu wa madini (kama chuma) na vitamini (kama vitamin B) NK

kimsingi, hearing aids hupewa mgonjwa ambaye ana tatizo kwenye ngoma ya sikio au kama sensory hairs zimedhoofika lakini hazijafikia hatua ya kuwa "dead" sasa kwa case yako, hearing aids hazitakusaidia kitu na nakushauri achana nazo kwani sensoiry hair zikifa huwa hakuna tena namna ya kuzihuisha. Mshukuru Mungu kuwa huna tatizo la nta au usaha kujaa masikio vinginevyo hizo hearing aids zingekuwa zinaacha mawimbi yakirindima ndani ya ubongo hata zaidi ya siku mbili baada ya kuvua na hali yako ingekuwa mbaya zaidi. Na kama ukisafiri kwa ngege ile milio ya ndege inaweza kubaki masikioni hata kwa wiki nzima baada ya safari.

Ushauri wangu, jikubali tu katika hali uliyonayo sasa acha kuhanmgaika na mahospitali yanakupotezea muda na hela zako bure. Furahia maisha na usiwazie sana mambo hayo ya masikio, jiamini zaidi na usiwaambie watu hovyo hovyo tatizo lako na wengine hawatakuja kugundua kamwe kama utajiamini. Epuka kuwaza jamabo lolote kwa muda mrefu. Jiburudishe mara kwa mara kwa muziki wenye sauti ya chini na hata kwa vinjwaji visivyo na kilevi kikali mara kwa mara (kama unatumia).

Pole sana mkuu, nakutakia maisha mema yenye furaha.
 
Pole sana kwa tatizo hilo.
Kwa vile upo dodoma, tafuta ofisi ya labor (kazi), uwaulize ofisi ya wakala wa afya na usalama kazini. Utakayemkuta muambie tatizo lako. Nina wasiwasi tatizo lako linahusiana na kazi unayofanya, haswa kelele. Endapo utatokea kuwa dar, ni-pm nikuelekeze ofisi ambayo utapewa msaada wa kutambua tatizo na kuelekezwa marekebisho/rehabilitation.

Nashukuru kwa ushauri,
ila kwa sasa sijaajiriwa, nimemaliza chuo hivi karibuni.
Je naweza kwenda hiyo ofisi ya labor kwa sasa?
 
Pole sana kwa tatizo hilo.
Kwa vile upo dodoma, tafuta ofisi ya labor (kazi), uwaulize ofisi ya wakala wa afya na usalama kazini. Utakayemkuta muambie tatizo lako. Nina wasiwasi tatizo lako linahusiana na kazi unayofanya, haswa kelele. Endapo utatokea kuwa dar, ni-pm nikuelekeze ofisi ambayo utapewa msaada wa kutambua tatizo na kuelekezwa marekebisho/rehabilitation.

kweli kabisa dada King'asti.

mkuu tx 500 ukifika Dar m-PM sister hapo kwa msaada zaidi ila unaweza kwenda moja kwa moja Buguruni Malapa pale kwenye shule ya viziwi utamkuta mtaalamu mshauri wa viziwi na muombe ushauri anaweza kukusaidia. Ila angalia anaweza kukuchomoa mchuzi wa bure kabisa kuwa makini na niamini nilichokueleza kwenye post yangu iliyotangulia.

once again, pole sana na jikaze kiume usonge mbele na maisha kuna watu wanaishi na hilo tatizo lako for decades na maisha yanakwenda kama kawaida na hata huwezi kumshtukia asipokuibia siri kuwa hasikii vizuri unapaswa kujiamini tu.
 
Tx 500,

Tafuta pesa uende India, yaliyoshindikana hapa mengi wao huyaweza, kajaribu na huko. Usione watu wanakimbilia huko burebure kuna manufaa huko.
 
Siku hizi kuna tiba/ tiba mbadala hata mabubu, ambao naturally huwa ni viziwi, wanasikia.

Usikate tamaa, hakuna ugonjwa usio na tiba nenda India. Hao wanaokwambia hakuna tiba ndio madaktari uchwara, watu wamesha "break through" kwenye matatizo ya masikio.
 
Siku hizi kuna tiba/tiba mbadala hata mabubu, ambao naturally huwa ni viziwi, wanasikia.

Usikate tamaa, hakuna ugonjwa usio na tiba nenda India. Hao wanaokwambia hakuna tiba ndio madaktari uchwara, watu wamesha "break through" kwenye matatizo ya masikio.

Duu! Nashukuru kwa ushauri, kwenda India inategemea na uwezo.mWengine ni watoto wa mkulima pure,tunategemea kuishi kwa jembe la mkono.
Thanks da'Faiza fox, mungu akibariki nitaenda India.
 
Tafuta pesa uende India, yaliyoshindikana hapa mengi wao huyaweza, kajaribu na huko. Usione watu wanakimbilia huko burebure kuna manufaa huko.

FF utaratibu gani mtu afuate ili aweza pelekwa India kwa ufadhili wa serikali?
 
FF utaratibu gani mtu anaweza pelekwa India kwa ufadhili wa serikali?

Zamani ilikuwa unaenda ustawi wa jamii, unaanzia hapo, kwa sasa sina uhakika lakini ukienda Wizara ya Afya utapata maelekezo. Halafu haya ni maswala ya wewe kumuona Mbunge wako akushughulikie ndio kazi zao hizo.
 
Pole sana mkuu Tx500. Naomba nikushauri yafuatayo; (1) Jikubali na hiyo hali ulionayo kama ulivyoshauriwa na mchangiaji mmoja.Kuwa mwenye furaha kwani kuna wenzako wanamatatizo zaidi yako,eg kiziwi na bubu, au mapacha walioungana,wewe huoni unanafuu?

(2) Nenda kwenye maombi au hata shika tv wakati pale huduma ya uponyaji inapotolewa. Mimi nilishawahi kuwa na tatizo la kifua,nimeangaika hospitali zote za nje na ndani na sikupona, nikaamua kujikubali, kutokunywa dawa yeyote na kuhudhuria maombi ya live na ya kwenye tv mara nyingi. Sikuona aibu kuweka mkono pale ninapoumwa hadharani wakati mchungaji anapotuambia. Imani iyo imeniponya kabisa huu mwaka wa 8 sasa kifua kilichokua kinanifanya nishindwe kutembea au hata kuinua kilo 1,hakijaumwa kamwe, PRAISE THE LORD.

(3) Usipende kutumia headphones au kukaa karibu na tv au radio kusikiliza kitu. Hii itafanya masikio yako yazoee sauti ndogo na kuongeza vichocheo vya usikivu. Mwangalie mtu usoni/mdomoni anapokua anatamka hasa unapokua kwenye interview. Hii pia hutumiwa na viziwi waliokua wanasikia zamani.

(4) Muone mbunge wako kama alivyoshauri FF, kwa msaada wa kwenda India.
 
Back
Top Bottom