TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

captain dunga

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
282
627
Mwanamuziki Maunda Zorro, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (Alhamis ya April 14) baada ya gari alilokuwa amepanda aina ya VITZ kugongana uso kwa uso na lori la mchanga huko Kigamboni, Dar es Salaam.

Maunda Zorro ni mtoto wa muimbaji nguli wa muziki Zahir Ally Zorro pia ni mdogo wa mwanamuziki Banana Zorro.

Maunda Zorro aliwahi kutamba na vibao kama vile 'NATAKA NIWE WAKO' na 'MAPENZI NI YA WAWILI' ambavyo mpaka sasa vinapendwa na wapenzi wa muziki kwani ni aina ya muziki usiochuja.

Apumzike kwa Amani

=============================
Kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Banana Zorro amesema:

"Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospitali ya Kigamboni, taarifa ni za kweli tulikuwepo kwenye msiba jioni ya leo wa rafiki yetu mwingine wa karibu, nilikuwa nae Maunda hadi jioni saa 11 hadi 12 nikarudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangoma.

"Chanzo cha kifo ni ajali ya gari, niliachana na Maunda saa 12 jioni ajali amepata mida ya saa 4 usiku, ila sina uhakika sana (wa muda aliopata ajali) hadi nikifika Hospitali maana nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana."

=============================

MWILI WA MAUNDA KUZIKWA JUMAMOSI

Kaka wa marehemu Maunda Zorro, Banana Zorro ametoa ratiba rasmi ya MAZISHI ya dada yake Maunda Zorro.
Marehemu Maunda Zorro atazikwa siku ya Jumamosi Aprili 16, 2022 nyumbani kwake Twangoma Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

IMG_20220414_050443_969.jpg



RATIBA YA MAZISHI APRILI 16, 2022
Maunda.jpg
 
Back
Top Bottom