"Nilianguka mkaninyanyuaa sikuweza kusimama mimi,
Hamkukata tamaa, nikajaribu teeena, Mungu akawajalia nikawashika bega...."

"Siri ya ninii, nini faida yake,
Siri ya ninii, nini hasara zake,
Siri ooh, siri ya mapenzii,
Mapenzi ya siriii, nalia lia"

Rest easy legend,
Umetuburudisha kwa sauti nzuri na mashairi mazuri.
 
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Mwanamuziki mkongwe Hussein Jumbe amefariki muda huu wakati akiendelea na matibabu katika Hospital ya Amana, Dar es Salaam.

===========
Updates

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe amefariki dunia.

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound, amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo Mwananchi zimetufikia hivi punde, Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Back
Top Bottom