Kwa hiyo sisi mamessenger tusiolewe jamani nyie watu mna balaa nyie. Mwanamke mzuri wa kuoa ni yule mwenye tabia na maadili mema, mwenye heshima, adabu, uvumilivu bila kusahau upendo. Hiyo ni taaluma tu hakuna uhusiano na kuolewa
siwezi kubadilisha. Ndio maana katikati ya thread nimeuliza kama hii kitu ni kweli.
Soma tena thread vzuqi.
nitakupm nikwambie. Au unataka nimwage mchele kwenye kuku wengi..
Ukitaka kuoa oa mwanamke ambaye ni mwalimu.
Huwa ni watu wenye hekima, wanaweza malezi kwasababu huwa wanakutana na watoto wengi wa tabia tofauti so wa kwake hawatomshinda.
Ni watu ambao hawawi overworked mara nyingi hivyo anapata muda wa kuwa na familia yake.
Na inasemekana wanaume wengi wenye hela huoa walimu.
Hiyo ni kweli wadau?
Wenye taaluma zingine mbona kazi tunayo.
watu washaelewa na ndio maana wanachangia. Hujaelewa wapi mpendwa?
Hebu nisome vizuri sio unaleta ushabiki wa kitoto!
Ila Walimu wa Kizazi hiki cha Dot Com aka Voda Fasta nasikia wanamegwa sana na Ma Head Teacher na Maafisa Elemu ha ha ha
Kuna sifa nyingine muliyoisahau! Mwalimu yuko mobile anaweza kuishi na kufanya kazi sehemu yoyote. kwa hiyo mme akihamia popote anaenda na familia. Ogopa fani zinazolazimisha mme na mke kuishi mbali kwa sababu ya kazi.
Siku hizi uzuri wa ndoa ni Pesa tu.Kama huna pesa au mna mapunfuku katika mapato ya kyuendesha familia hata ukiolewa/kuoa nani upendo kwenye familia ni sifuri.
My friend, money is not happyness kama unabisha angalia wenye pesa wake zao wana lala na house boys wao, na pia wanalia usiku kucha nyumba haina amani wala raha, mume anarudi asubuhi mke anachunwa na maserengeti, mume bize na wanafunzi na machangu. Mke mwema na Mume mwema, na ndoa yenye amani na furaha inatoka kwa mungu, na imepewa kibali na mungu mwenyewe. Pesa is ina play part ndogo sana kwenye maadili ya ndoa. Sijaolewa but nalijua hilo.
hapo kwenye red una maana gani? ni round ipi unamaanisha?Ha ha ha ha...
hi thread imenifurahisha maana mie nnaye teacher
wangu almost tabia mlizozieleza ndivyo zilivyo
tatizo lao kwa vile anakaa muda mrefu na wanafunzi
humfanya mmewe kama student vile utaelekezwa hata pasipoelekezwa
utafundishwa hata yasiyofundishika na kuna wakati utafananishwa na wanafunzi wake
ila kwa malezi ya watoto ni namba wani
si unakumbuka ulipokuwa msingi walivyokuwa wanabana
kupigwa round kitu cha kawaida, ndivyo wanavyowabana watoto
wakali hao...