Mwanamke lifestyle yako ndio itaamua ndoa yako

Si ajabu wewe ni katika waliokosea na sasa unaamua kuwapeleka chaka wenzako!

Mleta mada ametanabahisha tu, atakaetaka ajifunze asietaka apuuzie hakuna haja ya makasiriko.
Nimekosea nini? Changia hoja mezani acha kutaka kumjua mtu, ukweli ndio huo Ndoa sio mafanikio ya Mwanamke, somesheni watoto wenu kisha watoeni wakaione Dunia baadae huko watakuja kuolewa
 
Habari.

Imani Yangu Wote Mnaendelea Vyema Na Majukumu Ya Kila Siku.

Turudi Kwenye Mada Hapo Juu Kuhusu Lifestyle Ya Mwanamke Ndio Itaamua Mwanamke Kuolewa Au Kutokuolewa.

Wanawake Wengi Wamekuwa Wahanga Wa Lifestyle Zao Hivyo Kukosa Wanaume Wa Kuwaoa, Na Kufikia Mahali Kuanza Kusema Ndoa Ni Bahati Au Hakuna Wanaume Wa Kuoa.

Ila Ukweli Ni Kwamba Lifestyle Yao Wanayoishi Imewaondoa Kwenye Sifa Za Kuwa Nafasi Ya Kuolewa.

Wanawake Ni Wengi Ila Lifestyle Yao Imewapunguza Kwenye Idadi Ya Wanawake Wanaostahili Kuolewa.


Umri Wa Miaka 20 - 26 Kwa Mwanamke Hapa Tunasema Mwanamke Anakuwa Katika Peak Na Inahitaji Umakini Sana Kwa Mwanamke Ili Usipite Bure Kama Ambavyo Wengine Imewapita.

Kutokana Na Wanawake Kuwa Katika Ubora Wao Kwenye Age Hiyo (20yrs - 26yrs) Wanawake Wamefanya Makosa Na Kuanza Kuishi Kitalii. Maadili Na Malezi Ya Kitanzania Yapo Wazi Kabisa Yameonyesha Namna Gani Mwanamke Uwe Na Stara Pamoja Na Heshima Kwenye Jamii.


Niwape Siri Ndogo Tu Wanawake, Mwanaume Utafuta Mwanamke Wa Kuoa Si Kwa Sababu Yake Mwenyewe Bali Utafuta Wanamke Wenyewe Maadili Na Stara Kwa Sababu Ya Watoto Wake Wawe Kwenye Mikono Salama Hata Kama Hatokuwepo.

Maana Kuacha Watoto Kwa Mwanamke Mpumbafu Ni Kupoteza Generation Zijazo Pamoja Na Ndoto Zao. Angalia Vyema Unavyoishi Kwenye Jamii Yako Usifate Sana Mkumbo.

Wengi Wamesombwa Na Wimbi La Maisha Walivyokuwa Wanaishi Vyuoni Wamepeleka Mtaani Na Hapo Ndio Kosa Kubwa Lilipoanzia.

Namna Ulivyokuwa Ukiishi Vyuoni Na Mtaa Ni Vitu Viwili Tofauti, Maana Umri Utakuwa Unasonga Wakati Ulitakiwa Kuwa Kwenye Track Nzuri.

Wanaanza Kutambua Na Kujutia Katika Age Ya Nenda Kwa Usalama (27yrs - 29yrs) Na Hapo Wanakuwa Wanatembea Kwenye Deadline.

Wakifika 30yrs Hapa Sasa Wanakuwa Desperate Na Kuanza Kukashifu Ndoa Na Wanaume, Kumbe Walikosea Wenyewe Kwenye Age Ambayo Walitakiwa Wafanye Maamuzi Sahihi Ila Wakafata Lifestyle Ambazo Zimeharibu Mipango Na Kuwaondolea Sifa Za Kuwa Mke.

Yote Kwa Yote Wanawake Wenye Age 20 - 27yrs Msifanye Makosa Waliofanya Makosa Waliowatangulia Mtakuja Kukumbuka Mkifika 30's.


Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
Wanaume wanaooa kisa maadili siku hizi hawapo.

Ingekuwa hivyo mtu kama Elizabeth Michael asingeolewa,Zaiylisa, Dida, Irene Uwoya, nk
 
Wanaolewa Wale Ambao Wapo Kwenye Wakati Wao Wengine Waliojichetua Wanabaki Kutupa Malalamiko Umri Umesoga. Na Kusema Ndoa Ni Bahati Wakati Hakuna Bahati Bali Kila Kitu Utokea Kwa Preparation.
Watu wanaolewa kila siku acheni kuwatisha, nyie vijana ambao bado mnajotafuta hua mnapenda sana kuwakatisha tamaa mabinti zetu, kama ndoa ni mafanikio basi jua hata wenye 60s wanaolewa.....

Kama unahisi kuenjoy maisha ni kufanya uhuni basi wewe exposure imekupita mbali
 
Watu wanaolewa kila siku acheni kuwatisha, nyie vijana ambao bado mnajitafuta hua mnapenda sana kuwakatisha tamaa mabinti zetu, kama ndoa ni mafanikio basi jua hata wenye 60s wanaolewa.....

Kama unahisi kuenjoy maisha ni kufanya uhuni basi wewe exposure imekupita mbali
Wanaolewa Wale Ambao Wapo Kwenye Wakati Wao Wengine Waliojichetua Wanabaki Kutupa Malalamiko Umri Umesoga. Na Kusema Ndoa Ni Bahati Wakati Hakuna Bahati Bali Kila Kitu Utokea Kwa Preparation.
Wote mpo sahihi

'usasa' sio mbaya moja kwa moja, umalaya ndo mbaya
 
Yaan binti wa miaka 20 aache kuenjoy ujana wake akimbilie ndoa ili akafujwe humo ndoani awe kizee kisichotamanika, waacheni mabinti zetu wafurahie ujana wao, muda ukifika wa wao kuoelewa wataolewa tu, watu wanaolewa na miaka 60 sembuse 30+

Pia acheni mawazo ya kijima, ndoa sio mafanikio ya mwanamke, wafundisheni hayo mabinti zenu, wapeni elimu, waacheni waka explore dunia wapate exposure ukifika wakati sahihi which is wakiwa Matured enough wataolewa.
Kweli kabisaa.
 
Tafsiri yake ni kwamba sisi tuao waoa nyie wanawake ndio tunajua kwanini hatuwaoi.
Hapo juu mdau amewarahisishia nyie wanawake ili mzitambue sababu zinazo pelekea mnakosa kuolewa.
Sasa mmeamua kutowaoa na sababu mnazijua wenyewee si mtulizane hivyo hivyo? Tumechoka na kelele zenu.

Nyie ndo mnahitaji ndoa kuliko hao wanawake, ndo maana kutwa mnalalama,
 
Back
Top Bottom