Mwanamke: Hata kama huzai kinakuuma nini..?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
AfricanCouple.jpg

Mnaweza kufikia umri huu bila mtoto na ndoa ikaendelea kuwa ya upendo.......

Inaelezwa kwamba wanawake huwa wanavurugikiwa sana kiakili pale wanapogundua kwamba hawana kizazi au hawawezi kupata watoto.

Kuna ukweli kwamba mwanaume kama mwanamke huwa anasikitishwa na kukosa mtoto katika ndoa lakini kwa bahati mbaya tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba mwanamke huathirika zaidi kwa kujaribu kwake kuikataa hali hiyo. Wanawake huchukulia suala la kukosa mtoto au watoto kama ndio mwisho wa maisha yao.

Sio kwamba wanaume hawaumii kwa tukio kama hilo, la hasha huumia sana, lakini kinachotokea ni kwamba wao hulichukulia kwa uzito wa kawaida na hii husaidia kupandisha kiwango cha uwezekano kwao kupata ufumbuzi au suluhu ya tatizo hilo.

Wanawake mara nyingi wamekuwa wakihesabiwa kama ndio chanzo cha matatizo ya ndoa zisizo na watoto na kwa bahati mbaya wanawake wameonekana kwa kiasi kikubwa kuamini lawama hizo. Jambo hili huenda ndilo ambalo linawafanya wanawake kukosa raha kabisa pale wanapokuwa hawana watoto ukilinganisha na wanaume. Wanawake huogopa kwamba kwa kukosekana watoto ndani ya ndoa waume zao wanaweza kuchukua uamuzi wa kuoa wake wengine na kuwaacha wao au wao kuwa wake wakubwa wasio na thamani.

Hii ni njia ambayo imekuwa ikitumika sana katika mila karibu zote za Kiafrika. Lakini jambo kama hili halipaswi kuogopwa sana na mwanamke kwa sababu mume anayeamua kwenda kuoa mke mwingine kwa sababu mkewe wa awali hakubahatika kupata mtoto, huyo ni mwanaume asiye na upendo. Kwa nini basi mwanamke asione hiyo ni nafuu kwake ya kuachana na mtu ambaye alikuwa akiishi naye bila upendo.

Kwanza siku za nyuma wakati wa ujima mwanamke angeweza kulalamika sana kukosa mtoto, kwani mtoto alikuwa ni rasilimali. Lakini siku hizi mtoto ni sehemu ya ukamilisho wa jukumu la kimaumbile la mtu kulea kama alivyolelewa. Kama mwanamke anajikuta hana mtoto anaweza kwenda kuchukuwa mtoto kwenye nyumba za watoto yatima au kuomba ustawi wa jamii ili apewe mtoto aliyetupwa au kutelekezwa na wazazi. Huyu naye ni mtoto sawa au kumzidi yule wa kumzaa kama atapata malezi mema.

Imefika wakati ambapo inabidi wanawake wajue kwamba kukosa mtoto au watoto siyo mwisho wa dunia na wala haiwapunguzii hata chembe ya utu wao.
 
they feel incomplete. its psychological and unless u're in the same boat u can't really understand.
 
Uyasemayo ni kweli mkuu lakini tatizo ni jamii inayomzunguka pia (Mume, wakwe, mawifi nk) hawa huchangia sana matatizo kw ndoa ya aina hii...Mume anaweza kuwa undestanding na wapo hata waliokubalia wenzi wao kutafuta mtoto nje kisha akalelewa kwenye familia lakini hao nilowataja hapo juu bado watakuwa na wataendelea kuwa tatizo na sio kwa Tanzania peke yake bali karibu nchi zote za dunia ya 3 tunashea utamaduni huo.
 
hizi extended family zetu hizi...
ukichelewa kupata mtoto wanaweka midomo juu utafikiri uliolewa na ukoo mzima...

uombe upate mume mwenye msimamo, kama mumeo bendera fuata upepo.....lazima uwe stressed!!!!!!!!!!!
 
Uyasemayo ni kweli mkuu lakini tatizo ni jamii inayomzunguka pia (Mume, wakwe, mawifi nk) hawa huchangia sana matatizo kw ndoa ya aina hii...Mume anaweza kuwa undestanding na wapo hata waliokubalia wenzi wao kutafuta mtoto nje kisha akalelewa kwenye familia lakini hao nilowataja hapo juu bado watakuwa na wataendelea kuwa tatizo na sio kwa Tanzania peke yake bali karibu nchi zote za dunia ya 3 tunashea utamaduni huo.
Kuna msemo mmoja unasema ndoa ni ya watu wawili.......... hilo ndilo la muhimu kulizingatia.
mawifi, wakwe, majirani, na watu wengine haiwahusu, nyie wanandoa ndio mnatakiwa kuwa na msimamo juu ya ndoa yenu.
 
katika majaribu yoote duniani, omba Mungu wako jaribu hili lisikupitie.....

Ndugu Hute wewe hili ndo umeliona jaribu baya kuliko yoote humu duniani? Hakika kama ndivyo, hujatembea ukaona majaribu ya magonjwa mengine. Hili ambalo unapumua, unaenda popote utakapo, kazi unafanya na starehe zingine zozote wewe ndio unaliona jaribu baya kuliko? Kuna watu hata kunyanyua mguu kwenda haja ndogo hawawezi, na sio mapenzi yao!
 
Hatuoani ili kupata watoto, bali tunaoana kusaidiana, watotoni zawadi toka kwa Mungu aliyetuumba. Sasa kwanini wanawake au wanaume wanavurugukiwa??? Shida yetu wengi tunaoa on behalf of the family as a result if we can not fullfill their desires they will intimidate us and will not be able to bounce back.

Mungu awabariki.
 
Mkuu Mtambuzi hayo uliyosema ni rahisi kuyatimiza kinadharia lakini kihalisia ni mtihani mkuu sana tena sana, wanawake wanapata taabu ndugu yangu we acha tu, pole kwa wanawake wote wenye matatizo kama hayo, wanaitwa majina ya kila namna hasa na mawifi zao na ukikuta mwanamme ndo anafanyia kazi kila anachoambiwa ndoa huwa ni ya matatizo na matokeo yake wanaishia kuachana, lakini vile vile hata kama mwanamme atakuwa ni mwelewa bado mwanamke huathirika tu kutokana na maneno ya majirani, ndugu wa mmewe hufikia hata wanawake wenye matatizo kama haya huogopa kwenda kwenye mikusanyiko kama misiba, harusi.
 
Jamani ndugu zangu Shikamooni na kwa vijana wa rika langu Mambo!

Nimekuelewa sana,na umeelezea vya kutosha,ni wajibu nikusifu.
Unajua kila kitu kina chanzo,ndiyo!! sikatai kuna wengine ni kwa sababu ya kibiologia lakini wengine wanajitakia eidha kwa kutoa mimba ambapo hapo tukiongelea zaidi hawa kaka zetu wanaotamani tu mwanamke kimapenzi utadhani wakioa hawatafanya mapenzi na hata wengine wana wake zao lakini sijui kwanini wanatamani vya nje tena.
Na zaidi kaka'ngu kitu cha ziada ni kwamba kuna methali isemayo:uchungu wa mwana haujuaye ni mzazi:Je kakangu labda sijazaa na nina tatizo hiyo la kutokuzaa ikafikia pahala nikasema niende kwenye mashirika ya watoto yatima hili nikafate utaratibu na hatimaye nipate mtoto.
Swali ni kwamba je nitajua uchungu wa mamaye?au ilikuwaje mpaka akafika hapo?zaidi watakwambia walimuokota,sikatai kabisa kaka yangu hila bado chanzo cha huyo mtoto akijafahamika vizuri.
Kaka kweli kuna mtu amesema maji ya bomba yakatike kwa mwenzio lakini yakikatika kwako ndo utajua faida ya maji,Na msiba usikilizie kwa mwenzio hila ukija kwako hayo ni mengine.
Cha muhimu tuwape vijana elimu ya kutosha kuhusu hasara ya kutoa mimba,na pia zaidi tumuamini Mungu kuwa anaweza yote na ipo siku hatasikia sala kwa Waja wake hasa kwa wale ambao ni matatizo ya kibiologia tu hili suala limewakumba tu na tujihadhari zaidi na tamaa kwani ni mbaya sana ndugu zangu.
 
Ndugu Hute wewe hili ndo umeliona jaribu baya kuliko yoote humu duniani? Hakika kama ndivyo, hujatembea ukaona majaribu ya magonjwa mengine. Hili ambalo unapumua, unaenda popote utakapo, kazi unafanya na starehe zingine zozote wewe ndio unaliona jaribu baya kuliko? Kuna watu hata kunyanyua mguu kwenda haja ndogo hawawezi, na sio mapenzi yao!
ninasema hivi kwasababu ninao ndugu zangu kama wawili hivi wamepitia jaribu hilo na sasa karibia wanapita muda wa kuzaa kwa mwanamke....stress inavyowasumbua pamoja na kwamba wana hela nyingi wana pesa nyingi sana, ni kubwa mno, pressure wanayopata toka kwa ndugu upande wa mume ni kubwa mno, pressure wanayopata toka kwa majirani ni kubwa mno kiasi kwamba mwanamke hana hata raha ya kutembea mtaani au kutembelea vikao mbalimbali vya ukoo au arusi, kwasababu kila mtu anamnyoshea kidole kuwa huyo ni tasa, akigombana na mtu tu anaimbiwa taarabu ya majungu hadi anachoka....ni mateso makubwa sana, unajua kuteseka kisaikolojia ni mbaya kuliko kuteseka na jambo ambalo dawa ipo.....najua kweli kuna matatizo makubwa kuliko hilo lakini hili nalo ni moja wapo ya matatizo makubwa mno....cha kuelewa ni kwamba, mtoto ni zawadi toka kwa Mungu, si zawadi toka kwa mganga au kwa shetani, Mungu awweza kumpa mtu mtoto katika umri wowote ule na wakati wowote ule....na nyie wanawake mnavosemana? na kuimbiana nyimbo za taarabu? mnatiaga aibu.
 
Ndugu hatuendi hivyo,Kila kitu kina malengo,unakula hili ushibe,unavaa hili kuficha uchi,una panda mimea hili ukifika muda uvune na zaidi Hata Mungu aliyeumba dunia yeye kama yeye aliwaumba wanadamu hili waongeze nchi hata ukisoma neno lake kwenye biblia.

Hivyo basi ndo maana kuna faida na hasara.Anayepata faida na abarikiwe na kuweka mbinu zaidi na kukitunza kitu hicho Mfano: mwanamke anayezaa naye anayo budi kukitunza zaidi kiumbe hicho na kukipa malezi bora.

Je yule ambaye hana na hawezi kuwa naye unamshaurije wewe kama wewe?Swali kwako.

Sorry kama nimekukwaza?
 
Dawa ya mjinga ni kumpuuza, hiyo ndio kiboko ya mambo, kama wanaimba taarabu sijui na mafumbo mengine kama ukiwapuuza watafika mahali watazoea na watajiona wao ndio wajinga. Kumbuka mtu kuathiriwa kisakolojia na watu baki ni kutaka mwenyewe, kama kila jambo utalipuuza hakuna kitakachoakuathiri......

Mimi ninachosema hapa ni wanandoa kukubalia matokeo na kutafuta namna nzuri ya kuimarisha ndoa yao kwa jinsi watakavyoona inafaa na sio jamii au ndugu wawapangie namana ya kuishi.

Kuna wanandoa wana watoto, lakini kutokana na watoto hao kuwayumbisha kutokana na kuwa na mienendo isiyofaa, wanatamani hata wasingezaa, kuzaa sio ishu siku hizi kama ilivyokuwa zamani.
 
Ndugu hatuendi hivyo,Kila kitu kina malengo,unakula hili ushibe,unavaa hili kuficha uchi,una panda mimea hili ukifika muda uvune na zaidi Hata Mungu aliyeumba dunia yeye kama yeye aliwaumba wanadamu hili waongeze nchi hata ukisoma neno lake kwenye biblia.

Hivyo basi ndo maana kuna faida na hasara.Anayepata faida na abarikiwe na kuweka mbinu zaidi na kukitunza kitu hicho Mfano: mwanamke anayezaa naye anayo budi kukitunza zaidi kiumbe hicho na kukipa malezi bora.

Je yule ambaye hana na hawezi kuwa naye unamshaurije wewe kama wewe?Swali kwako.

Sorry kama nimekukwaza?
sijajua hili swali umeelekeza kwa nani, manake hapa tumechangia wengi kwelikweli, ni mtoa mada au sisi wengine ambao tumejaribu kuchangia? nisha
 
Last edited by a moderator:
Mnaweza kufikia umri huu bila mtoto na ndoa ikaendelea kuwa ya upendo.......

...... Imefika wakati ambapo inabidi wanawake wajue kwamba kukosa mtoto au watoto siyo mwisho wa dunia na wala haiwapunguzii hata chembe ya utu wao.

Thanks Mtambuzi kwa hii mada yako na hasa kwenye sentensi yako ya mwisho umezungumza vzr sana! Naamini maneno haya yatawatia moyo wanawake wote ambao hawaja jaaliwa kupata watoto ....

Asante,

HorsePower
 
Hebu tusaidiane ,kifanyike nini kwenye jamii hali hii ieleweke .Kwani tayari tunaissu kama hizo nyingi tu
 
Ndugu hatuendi hivyo,Kila kitu kina malengo,unakula hili ushibe,unavaa hili kuficha uchi,una panda mimea hili ukifika muda uvune na zaidi Hata Mungu aliyeumba dunia yeye kama yeye aliwaumba wanadamu hili waongeze nchi hata ukisoma neno lake kwenye biblia.

Hivyo basi ndo maana kuna faida na hasara.Anayepata faida na abarikiwe na kuweka mbinu zaidi na kukitunza kitu hicho Mfano: mwanamke anayezaa naye anayo budi kukitunza zaidi kiumbe hicho na kukipa malezi bora.

Je yule ambaye hana na hawezi kuwa naye unamshaurije wewe kama wewe?Swali kwako.

Sorry kama nimekukwaza?
nisha ............ muuliza swali, wewe unadhani suluhisho ni nini, maana mimi nimehatoa suluhisho katika maelezo yangu hapo juu, labda kama hujasoma maelezo yangu yote.
 
Last edited by a moderator:
Hatuoani ili kupata watoto, bali tunaoana kusaidiana, watotoni zawadi toka kwa Mungu aliyetuumba. Sasa kwanini wanawake au wanaume wanavurugukiwa??? Shida yetu wengi tunaoa on behalf of the family as a result if we can not fullfill their desires they will intimidate us and will not be able to bounce back.

Mungu awabariki.

Asante Mtumishi kwa ufafanuzi. Sikutegemea kugongana na mtumishi wa Bwn hapa jukwaani, ila nimefurahi. I hope kusikia mengi mazuri toka kwako.
 
Hebu tusaidiane ,kifanyike nini kwenye jamii hali hii ieleweke .Kwani tayari tunaissu kama hizo nyingi tu
UPOPO jamii inatakiwa kuelewa kwamba tatizo la kukosa mtoto au watoto katika ndoa sio tatizo la mwanandoa mmoja, inawezekana akawa mume ndio mwenye tatizo au mwanamke.
Inatakiwa jamii ikubali kwamba tatizo hilo lipo na jamii iwakubali wanandoa wasio barikiwa kupata watoto kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wao. kwani kila jambo ni majaaliwa na kama imeshindikana hakuna haja ya kuwanyanyapaa au kumnyanyapaa mwanandoa mwenye tatizo hilo, bali ni kujaribu kumsaidia kuondokana na dhana iliyojengeka katika jamii kwamba kukosa mtoto kwa wanandoa ni tatizo kubwa...........

Inashasngaza mwanaume anaweza kuwa ndiye mwenye tatizo lakini bado jamii ikamuona mwanamke kuwa ndiye mwenye tatizo, wakati mwingine mwanamke hulazimika kutoka nje ya ndoa ili kutafuta mtoto, ili kumfichia mume aibu! je akileta UKIMWI ni nani wa kulaumiwa.....?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom