MwanaJF mwenzetu kavamiwa na wezi na kukatwa katwa Mapanga

duh,pole sana mkuu,lakini mbona kama picha ni ya siku nyingi.nimeuliza tu,usinifikirie vibaya.

No kaka siwezi kudanganyia maumivu,siwezi ombea nivamiwe,siwez danganyia matatizo, hapa ni upenzi wa jf lakini nipo wodin picha hiyo imepigwa na cm ndogosana kisha nikaziomba kadoda11
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu Mungu akujalie upone haraka hawa watu si wema wanapokuvamia.
 
Ndugu wanajamvi habari zenu,

Mwana JamiiForums mwenzetu amevamiwa na watu wasioulikana nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. Watu hao walifanikiwa kuvunja mlango wa nyumba yake na kumkuta akiwa na simu mikononi. Kwa maelezo yake, alikuwa katika Jukwaa la Siasa akijaribu kusoma baadhi ya taarifa ndani ya JF.

Ghafla alishitushwa na sauti ya kubomolewa kwa mlango kisha tochi ikimulika macho yake na kuambiwa atulie papohapo. Akapigwa Mapanga kichwani, mdomoni, mikononi, na tumboni; walisikika wakisema aoneshe mahali pesa zipo. Waliweza kuchukua Pikipiki, TV 2, Deki 1, Baiskeli 1 na Pesa taslimu 270,000/=.

Humu anatumia ID ya MOTOCHINI.

Tumuombee mwenzetu akiwa kalazwa mpaka sasa!

Mmh pole sana, Dinazarde binamu tukae mkao wa kula unaona mwenzetu yamemkuta? Mdomo huo upunguze
 
Last edited by a moderator:
Pole sana MOTOCHINI, ila km alikuwa jukwaa la siasa huenda comments zake ziligusa wale wang'oa kucha maarufu mjini!???
 
Last edited by a moderator:
Pole sana ndugu yangu. Ila ningekushauri kitu kimoja hiyo picha yako itoe humu ndani maana huwezi jua hao walionusurika wana mpango gani na wewe.. Pia kumbuka marehemu ana ndugu zake na hatujua ni wa aina gani na wao hiki kifo wamekichukuliaje.. Ni ushauri tu maana aduia yako humjui. MOTOCHINI
 
Last edited by a moderator:
Pole kamanda yote hiyo inaletwa na usimamizi mbovu wa uchumi wa nchi yetu unaokoleza umaskini uliokithiri/kuongeza uhalifu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom