MwanaJF mwenzetu kavamiwa na wezi na kukatwa katwa Mapanga

LAGOSA

Member
Jan 8, 2014
69
54
Ndugu wanajamvi habari zenu,

Mwana JamiiForums mwenzetu amevamiwa na watu wasioulikana nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. Watu hao walifanikiwa kuvunja mlango wa nyumba yake na kumkuta akiwa na simu mikononi. Kwa maelezo yake, alikuwa katika Jukwaa la Siasa akijaribu kusoma baadhi ya taarifa ndani ya JF.

Ghafla alishitushwa na sauti ya kubomolewa kwa mlango kisha tochi ikimulika macho yake na kuambiwa atulie papohapo. Akapigwa Mapanga kichwani, mdomoni, mikononi, na tumboni; walisikika wakisema aoneshe mahali pesa zipo. Waliweza kuchukua Pikipiki, TV 2, Deki 1, Baiskeli 1 na Pesa taslimu 270,000/=.

Humu anatumia ID ya MOTOCHINI.

Tumuombee mwenzetu akiwa kalazwa mpaka sasa!

===================

Taarifa hii ni sahihi, ilikuwa mida ya saa 7:45 usiku ikiwa ni siku 2 toka nitoke jijini Mwanza kumpumzisha Bibiangu alietangulia mbele za haki, nami nimepatwa na mkasa huu. Japo si vyema kufurahia kifo cha mwanadam mwenzie, ila nilifanikiwa kumpiga mmoja kichwani na kipande cha chuma na nikaweza kutoroka na kukimbia huku nikivuja damu nyingi sehem za kichwa.

Taarifa nilizoletewa asubuhi niikuwa yule niliempiga kichwani amekutwa amekufa nyuma ya nyumba yangu, nasikitika kusikia kufa mwanadamu lakini ni katika kujihami.

Picha na maelezo zaidi nitajitahid hapo kesho niziweke hapa pindi nimalizapo mahojiano na police, kwani naogopa kupost picha za mharifu akiwa ni marehemu wakati police wakiendelea na taratibu zao. NIMEPUNGUKIWA DAMU, NAONGEZEWA DAMU.

attachment.php


NAOMBENI KUDRA ZENU. jMali LAGOSA kadoda11 MK254 uaminifukazi
 
MOTOCHINI

Pole sana ndugu yetu, Mwenyeezi Mungu atakuponya haraka na uamke Salaama Salmini... Usijaali Materials zitarudi tu!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanajamvi habari zenu, mwana jamiiforum mwenzetu amevamiwa na watuwasie julikana nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo, watuhao walifanikiwa kuvunja mlango wa nyumbayake na kumkuta akiwa na cm mikononi kwamaelezo yake alikuwa ktk jukwaa la siasa akijaribu kusoma baadhi ya taarifa ndan ya JF.

Ghafla alishitushwa na sauti ya kubomolewa kwa mlango kisha toch ikimulika macho yake na kuambiwa atulie papohapo akapigwa mapanga kichwani,mdomon,mikononi,na tumboni, walisikika wakisema aonyeshe mahali pesa zipo, waliweza kuchukua pikipik, tv 2, deki1, baiskeli1 na pesa taslim 270000.

Humu anatumia id ya MOTOCHINI tumuombee mwenzetu akiwa karazwa mpaka sasa


Pole Mkuu,

Story yako inafanana na ya kwangu tofauti yangu hawakuweza kuchukua kitu chochote bali walivunja mlango tu! Nikawa kama niko usingizini nasikia mlango unapigwa kwa nguvu, ie paaaaaaaaah paaaaaah! mara nikaona mwanga mkali unamulika chumbani mwanga unatokea dirishani, walipoona hakuna mtu sitiing room wakataka kuingia ndani .

Nilikua nikisikia watu wakivamiwa lakin siku ile nilishuhudia kwangu, mara nijisemea wakiingia ndani hata ningepiga kelele namna gani ni lazima wangenitoa ngeu kwa kutumia mapanga kama sio kuniua, basi nikaruka kutoka kitandani nilikua sina hata fimbo ndani, nikachukua maji ambayo yalikua kwenye chupa wakawa sasa wameshafungua mlango kabisa,

nikamwaga yale maji pwaaaaaah! katka mlango mara nikasikia vishindo tiiii tiiii tiiii mara tatu nikaanza kupiga kelele za wezi saa hio ni saa nane usiku majirani wote wamelala fofofo hakuna alieamka, nilipokuja kutoka nje nikakuta geti kubwa liko wazi kama fuso linaingia ndani, kuangalia vizuri kumbe walidondosha ile tochi pamoja na mavyuma mengine wakayi nilipowamwagia maji.

tangu siku hio nikilala nahakikisha milango yote magril yote yamefungwa.
 
Pole sana Motochini, tunamshukuru Mungu kuwa uko mzima, walivyochukua Mungu atakupa nguvu ya kupata vingine, kikubwa uhai.

Vv
 
Amelazwa hospitali gani? Kwa wenye uwezo na nafasi tunaweza kwenda kumjulia hali kama itakuwa sawa kwake though.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom