Mwanafunzi wa chuo cha TIA Mtwara ajiua

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,840
Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Mkoani Mtwara aliyetambulika kwa jina moja la Regan ambaye amekuwa akiishi Mtaa wa Chikongola, Manispaa ya Mtwara- Mikindani anadaiwa kujinyonga hadi kufariki na mwili wake kukutwa ndani ya chumba chake.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa jana July 4,2023 majira ya saa sita mchana na hadi sasa sababu zilizofanya ajitoe uhai hazijajulikana.

Baadhi ya Mashuhuda wameeleza hisia zao na kusema huenda Kijana huyo aliamua kujitoa uhai kutokana na masuala ya kimapenzi kwasababu Siku sio nyingi alikua amegombana na Mpenzi wake waliyekuwa wakiishi pamoja.

Kamanda wa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema amepokea taarifa za tukio hilo na atalitolea ufafanuzi baada ya uchunguzi wa Madaktari kukamilika na kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Ligula.

Marehemu Reagan muda mfupi kabla ya kujitoa uhai aliweka picha yake ya utoto kwenye WhatsApp Status yake na kuandika maneno yafuatayo ——> “🙏🏾 kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa, maana WEWE NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI”
 
Nakumbuka nikiwa third year pale T.I.A Kurasini Dar. Kuna dogo mmoja aliwahi kunywa nyagi na madawa ili afe....ikashindikana....then akatoka na kupanda juu ya ghorofa ( hostel) akajirusha chini....lakini jamaa hakufa aisee wala kuvunjika hata mguu au mkono ...hakutoka hata meno asee daah

Yote hiyo kwasababu ya mapenzi.

Afu dem mwenyewe sasa..

Sisi wanaume bhana!!! Kiazi kweli!!!
 
Afu dem mwenyewe sasa..
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Hahahahaha mapenzi upofu
 
Week iliyopita Ile treni ya Ubungo ilimsagasaga jamaa mmoja pale junction ya kwenda External from Mabibo mwisho, ila ilikuja kugundulika kuwa mshkaji alimuua mke wake kwahio akaamua kujimaliza Kwa kupondwa na treni. Mapenzi haya
 
Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Mkoani Mtwara aliyetambulika kwa jina moja la Regan ambaye amekuwa akiishi Mtaa wa Chikongola, Manispaa ya Mtwara...
kama kweli amejia kwa ajili ya mapenzi,basi huyu alikuwa mjinga sana! wa2 2meshawahi kutendwa mara kibao mpka moyo unakuwa sugu lakini 2najikaza kiume na aisha yanaenda, and then after a certain moment ofa time tunasaahau, kiasi kwamba siku ukikutana nae sehemu unashangaa na kujiuliza "da!!! yaaini huyu x-wangu mwenye masikio kama simbilisi ndio alitesa kweli? au aliniloga nini?

Then mwamba unamwangalia kama kabichi''
 
Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Mkoani Mtwara aliyetambulika kwa jina moja la Regan ambaye amekuwa akiishi Mtaa wa Chikongola, Manispaa ya Mtwara- Mikindani anadaiwa kujinyonga hadi kufariki na mwili wake kukutwa ndani ya chumba chake...
Kwa nini una-justify na kuhitimisha moja kwa moja kwamba amejiua bila ya kuwepo kwa ripoti ya uchunguzi/postmortem?

Umejuaje kama kajiua? Je, kama amenyongwa utasemaje kama amejiua?

No research no right to speak.
 
Back
Top Bottom