Moshe Dayan
JF-Expert Member
- Feb 10, 2008
- 815
- 698
jamani ni ngumu sana kubalance vipindi na kufkiria kutafuta maji.hali ya vyoo na mabafu ya mlimani ni mbaya sana hata kipindi ambacho maji yanatoka muda wote, sasa yakikatika ndio balaa.kwa kifupi kama umewahi kusoma pale utaona hali ilivyo mbaya.miundo mbinu ni tangu majengo yalipojengwa, pesa za maintanance watu wanapeleka puani.sasa mtu hajaoga siku tatu afu unataka awe na 'hekima' ya kutofanya fujo, si unafiki huo! shida ya maji inajulikana lakini si kigezo cha kuwanyanyasa wanafunzi kwamba watulie kama makinda ya kuku yaliyopigwa mdondo.kama uongozi wa shule haufany jitihada za ziada kuwapatia maji na walishalalamika kuhusu hili suala, we unategemea watafanya nini zaidi ili wasikilizwe? wamefanya walichofanywa kwa sababu wamelazimika.hayo magari ya maji yanakuja wakati watu wapo kwenye vipindi na pia, si magari ya kutosha na mengi huanza kupeleka maji kwenye nyumba za staffs yakibaki ndo madent wanahudumiwa.ile dhana kwamba mwanafunzi ili ajifunze vizuri ni lazma apitie shida haipo siku hizi, denti anahitaji kusoma katika conducive environment ili afaulu vizuri.na anayesema kua maji hayapo kwa mukandala, ye ndio mkuu wa chuo(baba), ni lazma ahakikisha wanawe(wanafunzi) hawanyanyasiki.suala la mwisho, kuhusu kiwango cha elimu, mlimani kwa stats za 2006, ilikua ya 11 katika vyuo vyote africa, kumi vikiwa south africa.poleni sana familia ya mwanafunzi aliyefariki!