Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,024
- 10,195
Hili swali ni tricky...kwani kama Ukristu si Dini kama dini nyingine.Yesu hakuhubiri dini, ila Injili.Na ndio panapowachanganya waislam na wakristu.
Baadaya kuamua jinsi ya ku approach hizo dini then ndio unaingia katika theology za hayo makundi bila kuwa biased ndipo utajua kundi gani utafuata mafundisho yao.Halafu katik hilo kundi ndipo utaangalia ni jinsi gani utafuata hayo mafundisho kufikia malengo yako.Kama ni ukombozi na kuiona mbingu au kama ni kuweza yaishi haya maisha ya dunia kwa kuwa na identity fulani.
Ni vizuri kujua kwanza na lengo la wewe kuamini.Halafu tafuta univeral values ambazo mwanadamu anahitaji kuzishika ili mahusiano yake na dunia, na wengine na yake binafsi yawe mazuri.Jaribu ziangalia zitatumikaje kufanikisha wokovu wako.Then angalia dini gani ina zitekeleza vyema.then zitumie kama vipimo vya kupima mafundisho yao,utekelezaji wake, kwani katika dini nyingine mambo hayatekelezeki kiasi cha kuchanganya waumini wao katika mambo ya msingi.Pia angalia staha, wasifu binafsi wa nabii husika.Kama nabii anakupa shida sana kumwelezea kukupata karaha, kama sifa zake zinatosha mpatia nafasi katika maisha yako na ungependa ufanyake kama yeye bila kuvunja universal principles ulizoziandika.Pia huyo nabii awe na sifa za kiroho asiwe tuu just kiongozi.Nadhani utakuwa katika sehmu nzuri ya kuifuata hiyo dini.
Haya mambo ya dini wakati mwingine yanakuja pale binadamu anaposhindwa kuwa na majawabu ya sintofahamu ya mambo mbalimbali kuhusu yeye na mazingira yanayomzunguuka