Mwanadada mrembo, nisha ghimire, na kifo chake cha huzuni na upweke kitandani

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Na DaVinci XV




61DB0BC5-6AED-4088-B2B9-B28B6759AF3F.jpeg




Wakati mwingine hakuna umaskini mkubwa kama upweke wakati wa magagasiko na dhiki, wakati ambao unahitaji faraja ya umoja.
Wale uliokuwa nao kwenye furaha wanapokuacha kwenye Chumba cha Upweke ni majonzi na maumivu makali ya moyo na akili zaidi ya jeraha la msumari.
Ukifumbua macho hukutani na kitu cha tofauti na wakati uliofumba macho ni Giza mwishowe ni bubujiko la machozi ya huzuni,sonona na Unyonge.


Anitha Mwashilindi (Code name) kutoka kule Songwe Alisafiri kutoka huko ardhi ya wazee wake, hadi kuja mjini katika hospitali fulani kupata matibabu ,juu ya Maradhi yaliyomsibu .
Anitha alikuwa mfanyakazi wa kanisa mtu wa Usafi wa Mazingira na mshirika wa Karibu wa Kanisa hilo X.

Maradhi yake Anitha yalihitaji vipimo na matibabu ya hali ya juu hivyo alifunga safari kufuata huduma hiyo mbali kidogo na ardhi ya nyumbani kwake katika hospitali yenye huduma kama hizo kama inenavywo na Wengi ya kwamba Afya ni mtaji.

Bad lucky , Familia yake haikuwa na uwezo wa kumudu gharama hizo ambazo ziliendelea kutafuna afya ya Bidada huyu polepole mithiri ya mdudu mchwa na Ukuta , Taratibu waliendelea kujichanga ili kupunguza gharama inapobidi ,Wanasema jikune mkono unapofika.

3716D449-8B8D-4C0A-93E4-28AAE418505D.jpeg

Matibabu ya Anitha yalikwenda vizuri na deni bado lilizidi kuongezeka kadri siku na wiki zilivyokata kujongea mbele na afya yake kuzidi kuimarika.

Tofauti na matumani ya wengi anitha aliendelea kuwa katika majonzi na huzuni haikutegemewa, unyonge wa hali ya juu pamoja na kato la tamaa vilionekana dhahiri kwenye wajihi wake mtulivu pasi na kupepesa, haikuhitaji hata elimu ya darasa la Chekechea kutanabahi ya kwamba wajihi huu wa mwanamama huyu ulikumbwa na wimbi zito la huzuni.

Kama ilivyo wajibu wa Wahudumu wa Afya , tuliitaji kung'amua tatizo zaidi, Kwa maana kinyume na matarajio tuliteyotegemea Anitha awe , ilitegemea aanze kurejesha furaha yake kama ilivyo awali kwasababu hali yake ilishaanza kutengamaa.
B98D8612-87ED-4EA2-922A-D3DB724FA360.jpeg


Majibu kulingana na maelezo ya Anitha ni Upweke uliomkumba baada ya kuona washirika wake wa kanisa , wamemtupa pekee katika dimbwi la maradhi na matatizo, hakuwa na mfariji zaidi ya wale wale ndugu zake wa pale nyumbani kwake.
Achilia mbali kumpigia simu kumtaka hali, anitha muda mwingi alilalama akibubujikwa machozi akagusia ndugu zake kuhangaika kila kukicha kulipa madeni na ilhali washirika wake wa karibu huwa na utaratibu wa kuchangishana lipatokea tatizo kwa mwenzao., imefanyika mara kadhaa kwa viongozi baadhi wa kanisa lile imekuaje yeye washindwe mfanyia hivyo!??
Au kwa sababu ya uduni wa maisha yake alibaki dhalili hakuwa na jibu.
Hata Hivyo nani angempa lawama sasa???

Jukumu la watu wa Afya jingine ni kutoa pyschological support ili kumuweka mgonjwa emotionally stable hii inachangia sana kwenye maswala ya healing process, na total recovery.

Hivyo pychological therapy zikaanza ili Anitha aweze kucopy na kuadapt mazingira. Akubaliane na mazingira na situation iliyomkuta

Ni kama pigo hilo hakulitegemea ., hata rafiki zake wa ibadani wakati huu hakuwa nao mwishowe, mwanamama huyu ali undergo depression ya hali ya juu ikapelekea kupata hadi suicidal ideation.
Kufupisha stori ili isije kuwa ni propaganda , hadi mudaa huu ninaokuandikia habari hii anitha yupo moja hospital kubwa ya watu wa akili hapa tanzania akiendelea na matibabu.
Tatizo likaaza tatizo yakawa matatizo.

SAD😔




C87154EE-B0AC-43F3-A817-BABC4986FC0E.jpeg



Siku miongoni mwa masiku nliyowahi kupiga soga na Anitha nikampa hadithi moja nliyowahi kuisoma mtandaoni huko Nepal kwa binti mrembo aitwaye Nisha.
Nilimpa anitha hadithi hii ili aelewe kuwa sio kila rafiki au jamaa yupo naye kwa dhati bali huenda ni kwasababu fulani, usitegemee kila ulienae sasa kwenye maisha ikitokea ukakwama jambo fulani mkaenda sambamba watakokuja kukusaidia huwenda wakakushngaza zaidi kuliko waliokukimbia.
Kwamba hadi huyu amesnisaidia SIKUTEGEMEA

AJABU🤔

19FAF850-5414-4CC4-AC93-0152D839FCC7.jpeg


NISHA GHIMIRE


Nisha Ghimire mwanadada huyu mrembo ambaye mwaka 2018 nyota yake ilionekana kunga'aa sana baada ya kuonekana sehemu tofauti ikiwemo mitandao ya kijamii , filamu na matangazo mbalimbali ya bidhaa.
Kama ilivyokuwako kwa mrembo wenu hapa Tanzania , Wema Abraham Sepetu kutoka kwenye Umiss Tanzania hadi Filamu , ndivyo hivyo hivyo kwa Nisha ghimire.

C375C9FE-C6BE-4897-8C96-6DB011F679F1.jpeg


Huyu alikuwa miss kutoka nepal na alianza kupata deals nyingi za Mitindo ya mavazi na Filamu kadhaa za Kihindi,baada ya kuonekana huko.

Katika mahojiano mbalimbali aliyowahi kuyafanya Nisha basi alieleza histori yake ni kutoka katika familia duni ambayo Nisha alikuwa anawish ndoto za kutoboa na kuinua familia hii aliyopo , kutokana na jina alilopata wakati huo lililochagizwa na urembo uhodari na talanta yake.

4983C336-A420-430E-9931-625AB5FEF029.jpeg


Makampuni makubwa yalishindana kuwekeza na kumfanya balozi wao, matukio tofauti tofauti alitokeza kama kioo cha matukio ya kisiasa ili kuvuta watu kutokana na uwepo, waswahili husema Supu zake chapati.

Ilipofika 2019 Nisha alisafiri kwenda India kuendelea na zake shuguli zinahusiana na career yake kwa bahati mbaya akapata ajali barabarani akiwa huko huko nchini India,Derahdun.
52E26A89-958F-4407-AEB8-344727BD4810.jpeg


Ajali aliyoipata nisha ilipelekea tatizo mwilini mwake na kupelekea pia organs za muhimu kama moyo na mafigo yake yakafeli na kushindwa kufanya kazi vizuri, ikapelekea matatizo mengine zaidi na zaidi hata kushindwa kutumia vyakula vigumu, aliihitajika kutumia vyakula vilivyo katika mfumo wa kimiminika tu.
5E214B01-46D5-4780-B24A-30AB7ACAB742.jpeg



Matibabu ya Nisha, yaligharimu gharama tele zilizopelekea Nisha kuishiwa.
Na kibaya zaidi watu maarufu wenzake ambao alikuwa nao kipindi cha mafanikio yake walimkimbia. Na mzigo huu ulibaki kwa familia yake ambayo haikuwa na uwezo, familia masikini na duni.

Hivyo Nisha alirudishwa nchini kwao nyumbani kwa familia yake kusubiri chochote kitakachotokea.

Wale marafiki wa kipindi cha raha walifika hapo na kupiga tu picha kisha kuzipost mitandaoni, kupata likes na mengineyo tofauti na hapo hawakufanya kingine chochote cha zaidi.

A4143A5B-DCFA-47C0-878B-3898843DB3FF.jpeg


Habari zilisambaa sana baada ya picha kumuonesha Nisha akiwa dhoofu lhali kitandani wala hajiwezi.

Mjasiriamali mmoja aitwaye Megha Chaudhary, aliguswa sana na tukio hilo baada ya kuona habari hizi mtandaoni juu ya ugonjwa wa Nisha. Moyoni mwake ikajengeka huruma ya utu na ubinadamu

Mjasiriamali huyu ambaye kipindi Nisha yuko on top , meneja wa nisha alikataa kufanya kazi ya mjasiriamali huyu ya kutangaza biashara yake. Kwa madai kwamba biashara ya Megha bado changa na kwa hadhi ya Nisha hawezi kufanya kazi na Mjasiriamali huyo, na wakatii huu wa shida na maswahibu meneja huyo wa nisha ambaye alimshinikiza kukataa kufanya deal la mjasiriamali Megha, naye alishazamia mitini mithili ya nuru ya mchana inavyomezwa na kiza kizito.

CB91D6DF-4102-4349-90F7-88978D4DF5D4.jpeg


Mjasiriamali yule Megha ndiye alikuwa mwokozi dakika za mwishoni , baada ya kuguswa na kadhia ya Ugonjwa Nisha.

Alikuja kujitolea kulipa bili za hospitali matibabu na huduma nyingine alizohitaji nisha lakini bahati mbaya sana walishachelewa nisha alifariki akiwa hospitalini hapo 01/09/2021 kifo cha unyonge na huzuni kuu.

Hivyo megha pia alihusika kwenye gharama za mazishi za mrembo huyo lakini pia akaingia jukumu la kulipia ada ndugu zake nisha waliokuwa mashuleni na chuo.

THOSE WHO CHEER YOU ARE WINNING WILL MOST PROBABLY NOT BE ON YOUR SIDE WHEN YOU ARE LOOSING






NB: Nliandika hii baada ya Taarifa za kifo cha huyo msanii Haitham zikanikumbusha kitu






Na DaVinci XV
 

Attachments

  • F3A62239-3E5F-4168-99F9-45ECCFA646C5.jpeg
    F3A62239-3E5F-4168-99F9-45ECCFA646C5.jpeg
    16.8 KB · Views: 7
Ajali aliyoipata nisha ilipelekea tatizo mwilini mwake na kupelekea pia organs za muhimu kama moyo na mafigo yake yakafeli na kushindwa kufanya kazi vizuri, ikapelekea matatizo mengine zaidi na zaidi hata kushindwa kutumia vyakula vigumu, aliihitajika kutumia vyakula vilivyo katika mfumo wa kimiminika tu
Hivi ikitokea mtu yupo katika chronic stage hawezi pewa kasindano kakumrudisha tu kwa sir God kuepusha kuendelea kuteseka na maumivu?

Au kidini ni dhambi ya kujiua kuyaruhusu hayo?
 
Hivi ikitokea mtu yupo katika chronic stage hawezi pewa kasindano kakumrudisha tu kwa sir God kuepusha kuendelea kuteseka na maumivu?

Au kidini ni dhambi ya kujiua kuyaruhusu hayo?
Nchi kama Belgium au Uholanzi kuna , aina hii ya action lakini kwa matakwa na sahihi za mgonjwa mwenyewe ili kupunguza mateso na maumivu makali. Baada ya form ya kuridhia hayo kusigniwa na mgonjwa mwenyewe. Inaitwa Euthanasia.

Baadhi ya dawa huchanganywa na huchomwa mgonjwa. Na kupelekea coma, na mwishowe kifo , baadhi ya nchi zinazui hili

Lakini pia kuna lethal injection itazame hii pia hii pia nayo hutumika kuwauwa wagonjwa taratibu ili kupunguza mataabiko ya Mateso na maumivu ya magonjwa hii pia hutumiwa , kwenye sheria kwa wale waliopata hukumu za kifo.
 
Back
Top Bottom