Mwakyembe mgonjwa afya yake yadorora; ngozi yavimba mwili mzima. Yadaiwa alitegeshewa sumu

Eeh bana dah! Mungu wa aman ampe uzima na kumwepusha na kusudi la waovu wote.
 
huyu mheshimiwa tangu aingie kwenye siasa imekuwa ni kizungumkuti tu - i think it is high time arudi chuoni akaendelee kutufundishia wanasheria wetu sasa
 
Kwa nini apelekwe India wakati hospitali ya maana ya MUHIMBILI ipo?

huu ndio ufisadi wenyewe...muhimbili wa avifaa na madaktari

ikishindikana si wampeleke hapo Nairobi hospital

why India?

Kwanza habari hii siiamini kabisaaaa!!! Mtoa mada anaonekana mzoefu tu humu jamvini; lakini anaonekana ka-join 07/10/2011 na ka-post thread moja tu ambayo ndiyo hiyo hiyo cha kuwekewa sumu! Ina maana hakuwahi kuwa member na akaamua kuwa member ili tu atoe hiyo habari?! Na kama hivyo ndivyo; then WHY?! Au labda ndio yeye katekeleza hilo zoezi ( la kumuwekea sumu) kisha akaamua kutumia ID nyingine tofauti na ile iziyozoeleka kisha akaja kutuhabarisha kwamba ameshafanya huo umafia. Likewise, kama ni kweli, basi ni kheri apelekewe huko huko India manake hata kama hilo tatizo la sumu ni la kawaida(xdentally food posisoning) basi akipelekwa Muhimbili halafu (god forbid) akafa; wapo watakaosema "alipofikishwa muhimbili hakuwa ameathirika sana lakini wakammalizia palepale!"

Hata hivyo, sizani kama kuna mpuuzi wa kumwua Dr. Mwakyembe kwa staili kama hiyo ambayo inaweza kutumiwa na un-professional killer/planner peke yake. Watu walio na bifu na Mwakyembe sio unprofessional mafia kiasi hicho otherwise iwe ni wanyakyusa wenzake wa huko huko kyela! Halikadhalika, haiwezi kuwa CCM wala RA, ambao wote ni professionals ambao wakitaka kufanya umafia kwa mwakyembe; hawawezi kutumia weak technique kama hiyo!na kama ni CCM, basi ni CCM ya kyela!

But all in all, anything can happen! am very cautious with Dr. Mwakyembe! Huyu mtu ni mjanja sana na ni hodari wa kucheza sarakasi na maigizo!! Huyu jamaa is capable hata yeye mwenyewe kunywa sumu ambayo anajua (kwa kushauriwa) kuwa haiwezi kumuondoa uhai ili tu kucheza sarakasi zake! Ukilifikiria kwa haraka haraka, unaweza kutoona mantiki yake; but for mwakyembe is possible!
 
Nimeshtushwa sana na habari hii. Kwa vile imekuja katika mazingira haya naweka benefit of the doubt kwa waliotoa taarifa. Namwombea Dr. Mwakyembe ahueni na nafuu ya haraka . Isije ikawa ni allergic reaction au food poisoning. Tusisome mengi kuliko yale ambayo yapo; ni vizuri kusitisha hukumu hadi taarifa zaidi zitoke.
 
Guys, Mwakyembe was a thorn then not now... nachelea kuamini kalishwa sumu bali naamini inawezekana ni matatizo kama aliyonayo Mwandosya... this is just my personal view, na kama ni sumu basi mwandosya would the best target

I think ni bahati mbaya kumekua na hali hiyo, i wish him quick recovery and we need him wizara ya ujenzi!!!

As boss said, things fall apart and sometimes kila kitu huharibika kwa wakati mmoja, it is somehow realised kwa CCM na majembe mengine mazuri ndiyo yamefikia umri wa kustaafu, ukiangalia vijana ndio hakuna hata kichwa kimoja chenye matumaini kwani wameingizwa kwenye siasa za majitaka.. na walio wasafi kama mwigulu wamejichafua wenyewe

GET WELL SOON KAMANDA
 
CCM wauaji sana. Habari za ndani zinasema alitofautiana na Magufuli juu ya mradi wa barabara ya Mtwara
 
Twendeni taratibu - ngojeni kupambazuke taarifa zaidi zitakuwa wazi. Tusianze kujenga minara, majengo, kuchimba mitaro na mahandaki. Mnaulizwa mbona mnajiandaa kama kunakuja vita? majibu "tumeambiwa kuwa Adui anakuja"....
 
Hali yake kweli si nzuri, hii nadhani imetokea juzi au jana, nimejaribu kumtafuta kupitia simu yake lakini haikuwa ikipokelewa.
Nini "hii imetokea juzi au jana," kulishwa sumu?

Twendeni taratibu - ngojeni kupambazuke taarifa zaidi zitakuwa wazi. Tusianze kujenga minara...
Katika ulimwengu wa leo wa mapinduzi ya habari hakuna mambo ya "ngojeni kupambazuke"! Ukiambiwa ndugu yako yu mahututi utasema "subiri kupambazuke"? Wewe ngoja, acha wengine watafute habari.
 
the centre cannot hold....things falls apart......hii inchi soon italipuka.....

mungu atulinde.....

Na mlipuko wake hautakuwa wa kawaida kutakuwa na maafa makubwa sana na majeruhi wa kutisha.
 
Tusianze kulaumu wanasiasa wenzake bandugu.

"Kalishwa sumu"
ni kiswahili cha wana habari wetu wakimaanisha maradhi ya food poisoning!

Recall Zitto!
 
Kuugua ni kawaida kila binadamu anaugua.., ila hilo la sumu ndio linatisha sana.., hivyo basi ni vema akaangaliwa na kupatiwa matibabu yote, bila kusahau wachukue vipimo ili kujua ni sumu gani imetumika (kama ni kweli ni sumu) ili kesho keshokutwa waweze kujua ni kina nani alikutana nao na wapi na wakampa nini ili hao wachawi waweze kujibu kilichotokea

Mkuu nani atafanya kazi hiyo nzuri wakati wenye mamlaka hayo ndio waliompa hiyo sumu!
 
Nia ya huyu aliyemlisha sumu ni nini? Au ndio huko kwenye ufisadi wanaona wataanza kulipuana
 
NI NANI AMBAYE ANA NINI NA VIONGOZI WA MKOA WA MBEYA NA BAADAYE NI MKOA GANI HUO?

Ni nani anayetetemesha Mkoa wa Mbeya huyu?????

Miezi miwili iliopita ilikua ni Prof Mwandosya ... na bado Wa-Tanzania hatujapata majibu ya chanzo cha ugonjwa wake, leo hii ni Dr Mwakyembe; tena ni jaribio la pili sasa kuhusiana na uhai wake.

Wakati huyu wa kwanza aliwahi kuwa na ... huko wizara ya Nishati na Madini miaka hiyo, huyu wa pili shida yake ripoti ya DOWANS. Sana kumefikia hapa kwenye sumu mwili mzima kuvimba wakati tu ni wiki mbili tangu cheki ya DOWANS kulipwa kinyume na matarajio ya Wa-Tanzania kwenda kusidia kampeni Igunga.

Swali ni kwamba ni nani au akina nani anafahamu / wanafahamu nini juu ya uhai wa viongozi hawa mahiri wa Mkoa wa Mbeya??? Je, baada ya mkoa huo kunafuata mkoa gani?????????????????? Je, wenye uzazi huo watakubali tu kumezea kweli bila kutafuta majibu kuliko tunvyouliza hapa???????????

Kuna nini kwenye sakata la DOWANS na malipo haya, nasema kuna nini Mkoa wa Mbeya na Mahesabu ya urais wa Tanzania 2015???

Bora maswali haya tukajibiwa leo kabla ya maji kuchafuka kesho watu kujitafutia majibu wenyewe mitaa tena kwa ulazima wakati huo.


Ndugu wana JF hizi ni taarifa za uhakika kabisa, Dr. Mwakyembe Kapewa sumu amevimba mwili mzima hali ni mbaya nilipopata habari hizi walikuwa wanafanya mpango kumkimbiza India. Nitarudi nikipata habari kwa undani

Nawakilisha
 
Doh Inasikitisha sana lakini kama ni kweli tutalia na kusagameno alafu baadae tutasahau kama walivyo muuwa Sokoine tukasahau na tukaendelea kutawaliwa nao, wakamuuwa Kolimba tena tukasahau na tukaendelea kuwachaguwa watutawale, wakamuuwa Karume bado tukawapa kura wendelee kututawala, wakamuuwa Mwahasibu wao wa fedha za EPA na DOwans bado wakashinda kwa kishindo.

Kama ni kweli ni kitendawili kikubwa maana hata adui wa adui wake pia anaweza kummaliza akijuwa atakaye laumiwa ni adui yake hasa kwa wakati huu wa uchaguzi ndani ya hiki chama cha kiaramia, kifisadi na kifirauni kinachoitwa CCM. Acha wauwane shauri yao maana aliye wa kwetu hawezi kuwa nao.

Jamani CDM ongezeni ulinzi kwa Dr. Slaa na Kila Mwanamageuzi atie sala kwa Rais wetu Mtarajiwa ili kila anayemuwazi mabaya atanguliye kama Yahaya Hussein yule Mchawi na Mtabiri wa CCM.
 
Back
Top Bottom