Mwakyembe: Mbunge unakwenda kwenye mkutano nje umevaa suti na raba kwanini usidharaulike?

the apparel makes a man. You are what you wear!!!

Nakubaliana na wewe na ndo mana nikaseam SIO MAVAZI PEKE YAKE tafsiri yake iko wazi pia kuna vitu vingine zaidi ya mavazi.. Mavazi yanaweza kumpa mtu first impresion wewe ni mtu wa aina gani tho sio lazima uwe ivo impresion inavosema...
 
Tatizo sio kuvaa mwak tatizo ni kwamba kaka keshatuanika kuwa cc ni ombaX2
 
Naruhisiwa cheka humu ndani? Postings nyingie huwa zinnifanya niangalie na avatar halafu napata imagination then napata kicheko...yupo wapi kipanya, gayo etc waweke comment kupitia vimichoro pengine tutapa picture muonekano wa hao waheshimiwa wanaopoteza heshima kwa uvaaji+uongeaji+kutojua geopolitics na standing ya TZ,
 
Heshima ya mwanaume ni namna unavyoweza kuiongoza familia yako ikajitosheleza kwa chakula na kujenga uchumi imara wa familia utaowawezesha wanafamilia kupata huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na elimu na afya. Heshima ya mwanaume haitokani na uvaaji. Kama ingekuwa hivyo, nchi hii kama siyo wa kwanza basi tungekuwa wa pili kwa uvaaji unaozingatia na hata kupita viwango vya kimataifa. Lakini tunadharauliwa kwa sababu ya KIGUU NA NJIA KUTEMBEZA BAKULI LA MISAADA.
 
Suala la attire ya baadhi ya viongozi au watendaji wetu leaves alot to be desired. Mwakyembe amepasua ukweli ambao unawasumbua wengi. Kwa kweli tunahitaji ku-improve on the way we dress ouselves when we go out there. Tatizo lingine ni kukosa seriousness tunapokuwa kwenye safari zetu za nje na mara kwa mara mtu anatamani mkutano uishe aende kufanya shopping ya kuteketeza per diem alizopewa.

Bora Mwakyembe kawapasulia ukweli.
 
waafrika bwana, wengine mavazi, wengine raba, wengine kiingereza .ha ha ha ha

Mbona George W Bush alikuwa anavaa kajizi kamepaukaa. Na pia sidhani kama Putin wa urusi anafahamu kuongea kiingereza. Mwakyembe naye nafikiri bado ana colonial mentality.

Kinachowafanya kudharaurika ni kuomba omba na kusema sisi ni masikini wakati kila kitu kimejaa bongo madini mpaka mnyama kakakuona. Wabunge wakitaka kutodharaulika watunge sheria za kulinda hadhi kwa taifa, sheria zikulinda umoja wa kitaifa, sheria za kulinda maliasili na malaghafi kwa taifa, sheria za kuwapendelea watanzania. Na wakati huo huo wasizisimamie sheria na kuziheshimu.

Vingenevyo hata ukipiga suti kali na kiatu chako kikali na kuongea lugha ya mkoloni kwa madaha yote bado utadharaulika tu, tena watakuonyesha kwenye tv zao ulivyopiga viwalo vyako na hapo hapo wanaonyesha watu wanavyoishi kwenye vinyumba vya msonge inzi wakiwatapakaa machoni na mdomoni na watu hao hao hawana chakula. Tena ni bora ukienda umevaa kimasai utaheshimika zaidi.

Well said mkuu!Like
 
Amechemka, huko nje tunadharaulika kwa ujinga wetu wa kutokujua kusain mikataba, Rushwa ya nje nje, na viongoz kushindwa kujenga hoja za kuondoa umaskin wetu hasa wanapoomba misaada. Zama za kuheshimika kwa mavazi, zilishapita kitambo.
 
Je wale viongozi au wabunge wanaovaa suti za kuhongwa nao wanamaana yoyote mbele ya wa-Tanzania au jumuiya ya kimataifa ?
Jamiiforums ina mtahadharisha Mh. Mwakyembe awe mwangalifu na kauli zake, maana ni bora kuwa na mbunge mzalendo mfia-nchi aliyevaa suti na raba alizolipia mwenyewe kuliko yule anayehongwa hata mavazi kama ndiyo bei nzuri ya kuuzia rasilimali za nchi

[h=1][/h]
 
Mwakyembe ni limbukeni mno.Nje ya Nchi mikutano kadhaa wazungu mnao wafuata huwa wamevaa kawaida tu na pia wakija hapa mara nyingi wanavaa kawaida sasa ubaya uko wapi .Kuvaa suti kunasaidia nini

Kasumba inatusumbua mno. Nyerere alishaliona hili na kuamua kuachana na suti za wazungu tangu miaka ya 62-64. Tunafikiri kuvaa suti za kizungu ndio kuendelea kwa kuuenzi utamaduni wa magharibi na kudharau utamaduni wa Kiafrika.

Unaweza kushangaa waafrika wengi hasa wafanyakazi serikalini wanapopata nafasi ya kusafiri nje ya nchi kikazi, kwani hakuna mapokezi ya pekee ambayo wanahitaji to show up huko waendako, utawakuta wanavyohangaika na makoti mazito na mengineyo, wakati wazungu wenyewe wenye utamaduni wao wanaposafiri wanavaa kaputula tu na vulana.

Wengine tunaposafiri tunapendelea kuvaa viatu vya wazi ambavyo ndani ya ndege upo na nafasi ya kukichomoa kiurahisi na kukivaa unapokihitaji unapoenda msalani. Basi si kosa lao. Waafrika wanakawaida ya kufikiri utamaduni wa wazungu ndio ustaarabu kwa dunia nzima.
 
Back
Top Bottom