Mvuno moja unavyobadili maisha, Bangi inavyotengeneza baadhi ya Madoni hapa Bongo na jinsi wanavyo takatisha pesa zao wafanye fujo kihalali

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
Onyo" Biashara hii ni haramu kama ilivyo kujipatia mali kwa ujangili, adhabu yake ni miaka 30 Jela. maada hii ni kwa educational purposes only,
1707578502201.png

Bangi, Msuba, Cha Arusha, Mmea, Wida, n.k. hii kitu ina toa watu wengi sana.

Wapo madoni wanaopata pesa za mauza uza hasa mikoa ya nyanda za juu kusini lakini kuna madoni wanapata pesa za mkupuo moja kwa kuvuna mara moja tu hili zao haramu.

Demand ya bangi ni kubwa sana lakini supply yake ni changamoto, hali hii imefanya bangi iwe na bei kubwa sana, kwa wale tuliosoma market forces aidha form 5 ama chuoni nadhani tunalijua hili, uhitaji wa kitu ukiwa mkubwa na uwepo wake ukiwa mdogo basi bei hupanda.

Gunia la Bangi ni shilingi milioni 2 na nusu hadi milioni tatu ila kwa hesabu za hapa tuchukue dau la chini mbili na nusu.

Hekari moja inatoa gunia 10 sawa na shilingi milioni 25

Kwa wale ambao hamjui ukubwa wa Heka, ni sawa na nusu ya uwanja wa mpira uongeze kidogo kama pichani

1707581902218.png

Biashara ni faida inayopatikana baada ya kutoa gharama kwenye mauzo, gharama zinazoweza kuwepo ni ulinzi maana hili zao ni haramu, mfano mdogo tu wiki zilizopia huko Simiyu kuna mtu aliiacha Noah yake imejaza magunia ya bangi kuna uwezekano mkubwa alisanuliwa kwasababu anatoa rushwa apewe taarifa kabla,

1707578616729.png

kuna gharama za usafiri, kuna kutoa rushwa, n.k. gharama hizi zinaweza fika milioni 3 kwa heka lakini makadirio mazuri huwa ni kupunguza mauzo na kuongeza gharama hivyo tuongeze iwe milioni 5, lakini huwa inazidi kupungua kadri heka zinavyozidi, zinakuwa gharama za jumla sio reja reja.

FAIDA - Baada ya kujua mauzo na gahrama zake sasa waweza piga hesabu za faida,
  • Kwa hekari 1 faida ni takribani milioni 20
  • Kwa hekari 10 faida yakribani milioni 200 +
  • Hekari 50 faida bilioni 1 +

Kuna watu wanavuna mpaka hekari 300 huko na wanunuzi wapo hata uwe na hekari 1000.

Umepata bilioni 1 za chap chap unadhani utaanza kuzitumia kiholea ? OLE WAKO !!, hapo ndipo huwa inabidi kuzisafisha zionekane ni pesa halali MONEY LAUNDERING, Ndipo wengi huanza biashara rasmi utashangaa tu mtu kutoka bush anafika mjini na mtaji mzito,

Biashara iwe yenye kugahamika inachapisha pesa ili hata ukiwa don watu wasiwe na mashaka wakiunganisha biashara zako na kipato chako.

Mifano ya biashara ni kama Mabasi, Hotel, apartments, maduka ya hardware makubwa, n.k. yanatengenezwa mazingira ya kupewa mikopo mirefu kwa udhamini wa madon wengine ambao wametoboa, hivyo kunakuwa hakuna mashaka vyombo vikijua umekopwa, biashara hizi zinaanza kuingizia pesa kilaini kabisa tena hata zikiwa hazina wateja zinaweza kuchakachuliwa zionekane zina wateja ili kuondoa mashaka, pesa zinachotwa kwenye akiba zinaingizwa kwenye vitabu zionekane ni wateja, basi linaweza kuwa gerej ila vitabu vikaonesha limepiga trip na limejaza, zinachotwa pesa za akiba za bangi kuzigeuza ziwe halali.

Bangi ikiruhusiwa ilimwe iuzwe nje ya nchi watu watatajirika ? Watu wengi wakianza kuilima wapo wataoanza kuuza gunia kwa laki 1 sababu hata kwa hio bei kuna faida, wataopiga pesa kwa kuiuza nje ya nchi ni wahindi hawa wanaonunua madebe ya mazao kwa elf 10 wanaenda kuuza Uingereza hata kwa laki na zaidi, Mtanzania wa kawaida ni ngumu kufanya biashara ya kimataifa, hata maparachichi wakulima wanashindwa kutafuta masoko ya nje ni mpaka wakenya waje tena wanauziwa kwa bei rahisi sana ukilinganisha na bei wanazouza huko ulaya, wanatajirika sana.

........................
 
Irasimishwe kama pombe, sigara, serikali ipate kodi na kuuza nje na kuifanyia utafiti kwenye vyuo, hospitali faida zake kiafya kwa matumizi sahihi.
 
Ikirasimishwa inaweza kuwa bei sawa na tumbaku, kinachofanya iwe na bei kubwa ni uparokanaji wake umebanwa, wachache wanaoweza kujitoa muhanga kuilima

Yep, ikiuzwa nje ya nchi tutapata fedha za kigeni kama tunavyouza kahawa. Ikitumika kutafuta dawa kwa mfano za maumivu makali bado itakuwa jambo litakalipa serikali pesa.
 
Onyo" Biashara hii ni haramu kama ilivyo kujipatia mali kwa ujangili, adhabu yake ni miaka 30 Jela. maada hii ni kwa educational purposes only,
View attachment 2899855

Bangi, Msuba, Cha Arusha, Mmea, Wida, n.k. hii kitu ina toa watu wengi sana.

Wapo madoni wanaopata pesa za mauza uza hasa mikoa ya nyanda za juu kusini lakini kuna madoni wanapata pesa za mkupuo moja kwa kuvuna mara moja tu hili zao haramu.

Demand ya bangi ni kubwa sana lakini supply yake ni changamoto, hali hii imefanya bangi iwe na bei kubwa sana, kwa wale tuliosoma market forces aidha form 5 ama chuoni nadhani tunalijua hili, uhitaji wa kitu ukiwa mkubwa na uwepo wake ukiwa mdogo basi bei hupanda.

Gunia la Bangi ni shilingi milioni 2 na nusu hadi milioni tatu ila kwa hesabu za hapa tuchukue dau la chini mbili na nusu.

Hekari moja inatoa gunia 10 sawa na shilingi milioni 25

Biashara ni faida inayopatikana baada ya kutoa gharama kwenye mauzo, gharama zinazoweza kuwepo ni ulinzi maana hili zao ni haramu, mfano mdogo tu wiki zilizopia huko Simiyu kuna mtu aliiacha Noah yake imejaza magunia ya bangi kuna uwezekano mkubwa alisanuliwa na watu anaiwalipa wampe taarifa

View attachment 2899856

kuna gharama za usafiri, kuna kutoa rushwa, n.k. gharama hizi zinaweza fika milioni 3 kwa heka lakini makadirio mazuri huwa ni kupunguza mauzo na kuongeza gharama hivyo tuongeze iwe milioni 5, lakini huwa inazidi kupungua kadri heka zinavyozidi, zinakuwa gharama za jumla sio reja reja.

FAIDA - Baada ya kujua mauzo na gahrama zake sasa waweza piga hesabu za faida,

  • Kwa hekari 10 faida ni takribani milioni 20
  • Kwa hekari 10 faida yakribani milioni 200 +
  • Hekari 50 faida bilioni 1 +

Kuna watu wanavuna mpaka hekari 300 huko na wanunuzi wapo hata uwe na hekari 1000.

Umepata bilioni 1 za chap chap unadhani utaanza kuzitumia kiholea ? OLE WAKO !!, hapo ndipo huwa inabidi kuzisafisha zionekane ni pesa halali MONEY LAUNDERING, Ndipo wengi huanza biashara rasmi utashangaa tu mtu kutoka bush anafika mjini na mtaji mzito,

Biashara iwe yenye kugahamika inachapisha pesa ili hata ukiwa don watu wasiwe na mashaka wakiunganisha biashara zako na kipato chako.

Mifano ya biashara ni kama Mabasi, Hotel, apartments, maduka ya hardware makubwa, n.k. yanatengenezwa mazingira ya kupewa mikopo mirefu kwa udhamini wa madon wengine ambao wametoboa, hivyo kunakuwa hakuna mashaka vyombo vikijua umekopwa, biashara hizi zinaanza kuingizia pesa kilaini kabisa tena hata zikiwa hazina wateja zinaweza kuchakachuliwa zionekane zina wateja ili kuondoa mashaka, pesa zinachotwa kwenye akiba zinaingizwa kwenye vitabu zionekane ni wateja.

........................
Hatari sana
 
Yep, ikiuzwa nje ya nchi tutapata fedha za kigeni kama tunavyouza kahawa. Ikitumika kutafuta dawa kwa mfano za maumivu makali bado itakuwa jambo litakalipa serikali pesa.
Wabongo bado hatuna uwezo wa kufanya biashara za kimataifa, Hata hii mihogo ikifika uingereza inauzwa laki 2 kwa debe lakini wanaofikisha huko ni wahindi wanaonunua vijijini debe moja kwa elf 10.

Hata bangi ikirasimishwa waweza kuta gunia likashuka mpaka laki 1 sababu watu wengi watakuwa wanailima, wataofaidi ni wenye connection nchi za nje hasa wahindi,
 
maduka ya hardware makubwa, n.k. yanatengenezwa mazingira ya kupewa mikopo mirefu kwa udhamini wa madon wengine ambao wametoboa, hivyo kunakuwa hakuna mashaka vyombo vikijua umekopwa, biashara hizi zinaanza kuingizia pesa kilaini kabisa tena hata zikiwa hazina wateja zinaweza kuchakachuliwa zionekane zina wateja ili kuondoa mashaka, pesa zinachotwa kwenye akiba zinaingizwa kwenye vitabu zionekane ni wateja.
nimecheka sana kwa kuwa umeamua kumwaga moga yetu mzee umefikiria nini lakini usisanue kijiji bwana.
 
nimecheka sana kwa kuwa umeamua kumwaga moga yetu mzee umefikiria nini lakini usisanue kijiji bwana.
Na inabidi umakini uwepo, Pablo alikuwa anaingiza bilioni 10 kila wiki, hakwenda shule akaamua kununua viteksi vyake vitatu visafishe hio bilioni 10, yaani teksi zake zikafanywa zionekane zinaingiza bilioni 10 kila wiki,

sijui aliizimaje hio ishu lakini ilikuwa ni sawa na kumpenyeza ngamia kwenye tundu la sindano,
 
Back
Top Bottom