Mvungi: Kafulila anashauriwa na 'shetani'

jamani swala la shetani alitumia kama mfano ktk lugha ya mazungumzo inakubalika.leo zito hajapost tena kichwa kichwa?
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa chama hicho, Dk. Sengondo Mvungi,
Alisema chama hicho kinasikitishwa na hatua ya mahakama kwa kuwa kinafahamu kuwa uamuzi huo umembomolea nyumba yake mwenyewe Kafulila huku kukiwa na ‘shetani' anayemshauri.

"Sisi tunasema aendelee kushauriwa tutafika tu," alisema Dk. Mvungi.

"Taarifa za agizo hilo tumezisikia kupitia watu wetu waliotupigia simu na wao habari hizo walizipata kwenye mtandao, sijui walimshawishi vipi Jaji, lakini sisi hili hatutashughulika nalo tena kwa kuwa amri hii imemuweka huyo Kafulila mwenyewe pabaya bila kujijua," alisema Dk. Mvungi.

::HabariLeo

David Kafulila anapoteza muda tu na tuwe na fikra chanya wakati mwingine...hivi hata kama amerudishiwa ubunge je kuna faida gani kwasasa? maana anakuwa mbunge wa Kigoma kusini kupitia mahakama na si chama chake tena...kwa maneno mengine kuna uwezo kano mkubwa wa huyu jamaa kufanya kazi kama mgombea binafsi,kwa kuwa hatapata msaada toka kwa chama hata chembe....sasa kwa hali kama hii hata kama tunapigania haki,kuna haki ukiipata inakuwa mzigo tena...ndio haya ya Kafulila,Je,atapata msaada kwa wabunge na wanachama wa NCCR kama mwanzo?

Kwa mtazamo wangu kuna hatua tunapaswa kuchukua maamuzi magumu bila kuendeshwa na watu wengine,kwi ukweli Kafulila anaendeshwa na kundi la watu wanaompotosha...na kesi ya Kafulila haitofautiani na kesi ya madiwani wa CDM Arusha...nadhani anachofanya Kafulila ni kama Dr anaejua kuna mgonjwa wa Cancer na atakufa lakini anampa dawa za kusogeza siku..na hii ndio inatokea kwa Kafulila kwasasa...

Ngoja tuone!!
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa chama hicho, Dk. Sengondo Mvungi,
Alisema chama hicho kinasikitishwa na hatua ya mahakama kwa kuwa kinafahamu kuwa uamuzi huo umembomolea nyumba yake mwenyewe Kafulila huku kukiwa na ‘shetani' anayemshauri.

"Sisi tunasema aendelee kushauriwa tutafika tu," alisema Dk. Mvungi.

"Taarifa za agizo hilo tumezisikia kupitia watu wetu waliotupigia simu na wao habari hizo walizipata kwenye mtandao, sijui walimshawishi vipi Jaji, lakini sisi hili hatutashughulika nalo tena kwa kuwa amri hii imemuweka huyo Kafulila mwenyewe pabaya bila kujijua," alisema Dk. Mvungi.
Wakati Zitto anatibiwa India, Mb Machali alimshutumu kuwa ndiye chanzo cha mgogoro huu wa NCCR. Sidhani kuwa ilikuwa politically correct kwa Zitto kuwa mtu wa kwanza kuujulisha umma maamuzi ya mahakama.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa chama hicho, Dk. Sengondo Mvungi,
Alisema chama hicho kinasikitishwa na hatua ya mahakama kwa kuwa kinafahamu kuwa uamuzi huo umembomolea nyumba yake mwenyewe Kafulila huku kukiwa na ‘shetani’ anayemshauri.

“Sisi tunasema aendelee kushauriwa tutafika tu,” alisema Dk. Mvungi.

“Taarifa za agizo hilo tumezisikia kupitia watu wetu waliotupigia simu na wao habari hizo walizipata kwenye mtandao, sijui walimshawishi vipi Jaji, lakini sisi hili hatutashughulika nalo tena kwa kuwa amri hii imemuweka huyo Kafulila mwenyewe pabaya bila kujijua,” alisema Dk. Mvungi.
Wakati Zitto anatibiwa India, Mb Machali alimshutumu kuwa ndiye chanzo cha mgogoro huu wa NCCR. Sidhani kuwa ilikuwa politically correct kwa Zitto kuwa mtu wa kwanza kuujulisha umma maamuzi ya mahakama.
 
Kwa nini unasema hivyo.

Mwanasheria anatakiwa a frame mambo in a secular frame ili ajenge argument kwa watu wote.

Kuna wengine ni secular humanists/ atheists hatuamini kuwapo kwa mungu wala shetani, tukisikia mwanasheria msomi anaongelea habari za shetani tunaona hajui issues/ kashindwa kujieleza.

Ni sawasawa na Kikwete kwenda kwenye maafa ya mgodi umefukia watu Mererani anasema "Kazi ya mungu". Either anawapa watu false therapy au hajui ku frame mambo in the framework of quality control and disaster prevention.

Shetani/ mungu ni singularities zinazotumika na wanasiasa kupiga changa la macho.

Shetani hatambuliki katika framework ya sheria, kama angetambulika kila mtuhumiwa angesema "nimeshauriwa na shetani" kesi inaisha.

Mvungi anatakiwa atupe mambo kutoka a secular perspective. Habari za shetani aachie wachungaji na ma shehe.
 
Wakati Zitto anatibiwa India, Mb Machali alimshutumu kuwa ndiye chanzo cha mgogoro huu wa NCCR. Sidhani kuwa ilikuwa politically correct kwa Zitto kuwa mtu wa kwanza kuujulisha umma maamuzi ya mahakama.
Zitto won't run out of the sphere, remember apart from being the 1st to announce the court decision to public he was also the one who called police to intervene the NCCR-NEC meeting.
 
Wakati Zitto anatibiwa India, Mb Machali alimshutumu kuwa ndiye chanzo cha mgogoro huu wa NCCR. Sidhani kuwa ilikuwa politically correct kwa Zitto kuwa mtu wa kwanza kuujulisha umma maamuzi ya mahakama.

Zitto ana foolish swagger fulani ambayo mwenyewe anafikiri ni sticking to principles.
 
Mwanasheria anatakiwa a frame mambo in a secular frame ili ajenge argument kwa watu wote.

Kuna wengine ni secular humanists/ atheists hatuamini kuwapo kwa mungu wala shetani, tukisikia mwanasheria msomi anaongelea habari za shetani tunaona hajui issues/ kashindwa kujieleza.

Ni sawasawa na Kikwete kwenda kwenye maafa ya mgodi umefukia watu Mererani anasema "Kazi ya mungu". Either anawapa watu false therapy au hajui ku frame mambo in the framework of quality control and disaster prevention.

Shetani/ mungu ni singularities zinazotumika na wanasiasa kupiga changa la macho.

Shetani hatambuliki katika framework ya sheria, kama angetambulika kila mtuhumiwa angesema "nimeshauriwa na shetani" kesi inaisha.

Mvungi anatakiwa atupe mambo kutoka a secular perspective. Habari za shetani aachie wachungaji na ma shehe.
Mvungi ni mwanasiasa kwa hiyo anafit kulitumia?
 
Zitto ana foolish swagger fulani ambayo mwenyewe anafikiri ni sticking to principles.

Kiranga,

Aisee hiyo description yako ya Zitto ni kweli kabisa. Zitto is not humble and sadly has a know-it -all attitude.
 
Mvungi ni mwanasiasa kwa hiyo anafit kulitumia?

I thought of that, ningetegemea mwanasiasa asiye na uelewa wa kisheria aseme hivi. Ukisema habari za shetani unaleta element za dini katika siasa na wengine tusioamini dini, na tunajua wewe Mvungi mwanasheria you know better in terms of which framework this is in (mwanasheria anajua suala la framework na jurisdiction/ jurisprudence siasa haiko katika jurisdiction ya shetani, shetani jurisdiction yake ni dini kwa watu wanaoelewa kufikiri), tunakuona unaleta habari za lowest common denominator za wabongo wengi, tunaona distraction.

Mimi ningependa kuona Mvungi anaongelea facts, hizi habari za Kafulila kushauriwa na shetani si fact, ni distraction from facts.

Tupeni secular and reason based politics, longolongo zenye religious connotations, especially kwenye contentious dispute ziacheni makanisani na misikitini.

What's next? Atatuambiwa yeye anashauriwa na mungu na hivyo tumsikilize yeye kwa sababu hiyo? Ndicho anachomaanisha ukiangalia deeply hapa.

Kama nilivyosema, kutumia hilo kwa mwanasiasa anayejua better ni kupiga watu changa la macho.
 
Wednesday, 28 December 2011 21:56
nccr-kafulila.jpg
Mkuu wa Idara ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kesi iliyofunguliwa na mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kupinga maamuzi ya chama hicho. Kulia ni Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama hicho, Danda Juju. Picha na Fidelis Felix

YAITISHA MKUTANO KUFAFANUA AMRI YA MAHAKAMA, HAMAD RASHID MAMBO BADO MAZITO CUF
Waandishi wetu
AMRI ya Mahakama Kuu iliyozuia utekelezaji wa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila imeonekana kuuchanganya uongozi wa chama hicho ambao jana ulilazimika kutoa ufafanuzi wa hatua hiyo ukisema haujatengua uamuzi wake huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa chama hicho, Dk Sengondo Mvungi alisema kabla ya kupokea hati ya Mahakama Kuu juzi juu ya amri hiyo, simu za wanachama wake mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii imekuwa ikiandika habari kuwa mahakama hiyo tayari imempa Kafulila ushindi katika shauri lake dhidi ya chama hicho.

"Msimamo wa chama kwa sasa ni kwamba maamuzi yake ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Desemba 17, mwaka huu bado hayajatenguliwa wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Isipokuwa kwa sasa tumepokea amri ya Mahakama Kuu ikizuia chama kisiendelee na hatua zaidi dhidi ya Kafulila na wenzake walioshiriki kushtaki chama kwenye kesi namba 218 ya mwaka 2011 mpaka shauri la msingi litakapoamuriwa," alisema na kuongeza:

"Ufafanuzi wa kilichoamriwa na mahakama ni kuhusiana na yale waliyoyaomba ambapo hakuna hati yoyote inayoonyesha maombi ya kubatilisha maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (ya NCCRR-Mageuzi). Suala la kuamuru upande katika kesi usifanye jambo zaidi ni katika mamlaka ya mahakama ambalo chama hakina tatizo na suala hilo."

Hata hivyo, Dk Mvungi alisema hakuna amri yoyote ya mahakama iliyotolewa ya kuwabakiza waliovuliwa uanachama katika chama huku akisema suala la ubunge wa Kafulila lipo mikononi mwa Spika wa Bunge na kwamba wao kama chama nguvu yao inaishia katika kumvua uanachama.

Kauli ya Bunge

Akizungumzia suala hilo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliliambia gazeti dada la Mwananchi, The Citizen kwamba mahakama haiwezi kuiandikia barua Bunge kulitaka lisitoe uamuzi kuhusu Kafulila.

Alisema Mahakama inaweza kuiandikia barua NCCR na kuitaka iliandikie Bunge barua kusitisha utekelezaji wa suala lake.

Alipoulizwa kama Bunge litaendelea na taratibu za barua ya NCCR ya kumvua uanachama Kafulila, Ndugai alisema: "Bunge litaendelea na taratibu zake kama kawaida."

Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilimvua uanachama Kafulila, Desemba 18, mwaka huu, siku 10 baada ya kumwengua kwenye nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama hicho kwa tuhuma za kutoa siri za chama.

Baada ya uamuzi huo, Kafulila aliandika barua kwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia akiomba kikao cha Halmashauri kuu kiitishwe tena kurejea uamuzi wake na baadaye kuwasilisha malalamiko yake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye alikiandikia chama hicho barua kutaka ufafanuzi wa malalamiko ya mbunge huyo kisha alikwenda Mahakama Kuu kuomba amri ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi dhidi yake baada ya kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama.

Hamad Rashid mambo bado mazito CUF
Katika hatua nyingine, Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kitendo cha Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed kugoma kuhojiwa juzi, imelenga kupoteza muda tu kwani hakiondoi msimamo wa chama kumshughulikia kwa mujibu wa katiba yake.

Juzi, Hamad aligoma kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu tuhuma za kuvunja katiba huku akiibua tuhuma nzito kwamba amenasa waraka wa siri wa viongozi wawili waandamizi wa chama hicho waliokuwa wakipanga njama za kumfukuza.Mbunge huyo alitoa sababu tano za kugomea wito huo ambazo ni pamoja na kutoeleza tuhuma zake hasa vifungu vya katiba alivyodaiwa kuvikiuka na mamlaka ya kamati hiyo kikatiba.

Hata hivyo, jana Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema madai hayo ya Hamad hayana msingi zaidi ya kupoteza muda akisema kamati hiyo ipo kikatiba kwa kuwa iliundwa na Baraza Kuu la chama hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadili, Abdul Kambaya alisema wanachama wake saba wamekwishahojiwa hadi sasa na wote wamekubali tuhuma wanazokabiliwa nazo za kuvunja katiba ya CUF na wameomba vikao vya juu vitakavyokaa kufanya maamuzi kwa kutumia busara ya hali ya juu.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, Hamad alisema anagomea kikao hicho hadi atakapopewa kanuni zitakazotumika katika kuendesha shughuli nzima ya kujibu tuhuma hizo na kupewa katiba iliyotumika ambayo ameivunja.

Alisema kati ya wajumbe wanane, hana imani na wajumbe watano kwa sababu wamekuwa wakimtuhumu hadharani: "Hawa wajumbe sina imani nao uamuzi wao hautakuwa wa haki kwangu."

Jumatatu wiki hii Hamad na wenzake 13 waliitwa na Kamati na Nidhamu ili kujibu tuhuma za kuvunja katiba ya hicho baada ya kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu kati yake na Katibu Mkuu Maalim Seif Shariff Hamad.

Habari hii imeandikwa na Fidelis Butahe, Raymond Kamnyoge na Taus Ally.

Back
Top Bottom