MV Kikwete inazama?

Augustine Moshi,
Ama kweli kuna wakati chongo huitwa kengeza! Mimi sioni tafsiri ama maana nyingine ktk maneno hayo hapo juu! Ebu tusome tena upyaaaa!
Serikali ya awamu ya nne iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete (JK) imefanikiwa kujenga shule mpya za sekondari 381 nchini kote ndani ya kipindi cha miezi minne tu tangu Januari hadi April mwaka huu.

Sasa ikiwa waona ajabu na kutaka kumpa sifa Mkapa mbona mabaya wamwangushia JK?....
Iwapo pongezi za ujenzi wa shule hizi anastahili Mkapa kwa sababu unaamini zimejengwa toka wakati wa Mkapa ama ni moja ya sera zake basi hata kodi pia zinakusanywa na wananchi walewale aliowaajiri Mkapa ktk mfumo ama sera zilezile za ukusanyaji aliouacha Mkapa!

Augustine, Kuna issue moja kuhusu Elimu nataka sana kuizungumzia.
Wenzetu nchi za magharibi wanaposema ELIMU kuwa msingi wa maendeleo huwa wanamaanisha ELIMU kuwa kitovu cha uzalishaji! na wasomi ndio WAAJIRI... kwa maana hii huwezi kupata liseni Ulaya ya kuendesha hata Kigereji cha magari mabovu, ususi wa nywele na kadhalika kama huna cheti cha ELIMU ya ufundi huo. Karibu kila biashara inayohusiana na ELIMU lazima tajiri awe na ELIMU yake hata iwe udalali wa nyumba. Naposema Tajiri nina maana mtoa ajira sio utajiri wa fedha maanake hata jambazi linaloondoka solo linaweza kuwa tajiri vilevile.
Kwa hiyo kinachonishangaza mimi huko nyumbani biashara zote zinazotakiwa ELIMU zimeshikwa na mtu yeyote mwenye fedha! Hotel za kitalii, Hospitali nahata vyakula vya makopo maadamu huyo tajiri awe ameajiri wafanyakazi wenye elimu hiyo. Hapa fedha zimezidi nguvu kabisa ELIMU kwani msomi na elimu yake hana sauti kwa mwajiri hata kama elimu yake ndiyo inayoendesha biashara!.. hakuna deal linaloweza kuendeka hapa kati ya msomi na mwenye mali.
Kusema kweli sioni tunakokwenda na Elimu ikiwa hakuna sheria ama system ambayo itaweza kumtajirisha msomi (esp. University na College) ktk fani yake. Nachoona mimi watu wanasoma ili wapate kutafuta ajira inayolipa na sio kwamba serikali yetu imeandaa mikakati ambayo itamwezesha msomi mwenye record nzuri kuanzisha kimradi chake...Na matokeo ya kuajiriwa hasa kwa wasomi mara nyingi hayana tofauti na Ujamaa..msomi hukosa uchungu pale mali sii yake na mara nyingi utawakuta wakipiga mahesabu!.. kazi niifanye mimi anayetajirika mtu mwingine!
Kwa kuondoa vitu kama hivi wenzetu nchi za nje serikali zao zimejitahidi sana ktk kukuza biashara ndogondogo kwa kuwapa miyaji (kupitia benki) nafuu ya kodi pia uwezo wa kuendesha biashara za ufundi lazima ziwe na shahada laa sivyo kauze embe na kahawa sokoni!..
Ebu tujiulize ikiwa sisi tunapewa fedha na benki kuu ya dunia kwa sababu tu tunaonyesha uwezo mzuri wa kujenga nchi inakuwaje viongozi haohao wanashindwa kuona upande huu na kuelewa kwamba maendeleo ya nchi nzima huanzia kwa watu wake (wazawa) na sio kuwa na miradi mikubwa chini ya wageni!
 
Ndugu Mtanzania,

Hakuna Mtanzania yoyote, not even Mzee Makamba, ameweza kujenga shule ya sekondari (form 1 - 4, au form 1 - 6) tangu mwanzo hadi ikakamilika, katika kipindi cha miezi 4. Huwa inachukua mwaka.

Kwa Mama Sitta kudai kwamba wamejenga shule za sekondari 381 katika kipindi cha miezi 4, sio kweli. Labda wamekamilisha ambazo ujenzi wake ulianza huko nyuma, au wamejenga darasa la 9 na kusema wamwekamilisha shule, au wamegeuza shule za msingi kuwa sekondari na kuhesabu wamejenga sekondari mpya.

Mkandara,

There are no short cuts to development. You can walk the route fast, but you must walk the whole route. It takes a critical mass of educated people to develop, and we do not have it yet.

Inabidi tupanue na kukuza elimu yetu by leaps and bounds. It is not time to be overly concerned about who gets to call the shots. Tunataka watu wawekeze tupate ajira. Kama hawajasoma (na nadhani wawekezaji wetu wazuri kama Azam wala sio wasomi wa kutisha) au wamesoma (kama Mengi), isikujalishe.

Kinajonijalisha sana mimi ni wingi wa Watanzania, hasa wa ukanda wa Pwani, ambao elimu yao ni ndogo kiasi kwamba hata interest zao zinaishia kwenye kusoma vijigazeti vya gossip kama Kashehe na mpira tu. Their world is extraordinarily small. They cannot be economic players on the global scene, for they are not even aware of the global scene. And, alas, the global scene is the only viable scene today, for everything is being globalized.

Augustine Moshi




Augustine Moshi
 
Naona Mtukufu Rais ametishia tena kuwafukuza kazi viongozi wa serikali za mitaa ambao wanakula fedha za uma. Sasa kama kweli anawafahamu viongozi wa aina hiyo, si atoe ripoti polisi wakamatwe?

Kosa la kuiba mali ya uma ni kubwa, na adhabu yake sio kufukuzwa kazi tu. Ni kushitakiwa na kufungwa. JK asiwape viongozi dhana kwamba wakiibia uma basi sana sana wataishia kufukuzwa kazi, waende wakafurahie hizo fedha za wizi.

Si vema Rais kutishia kitu kile kile zaidi ya mara moja. Atende, asiseme tu. Talk is cheap.

Augustine Moshi
 
Wajameni,
Nawasalimieni wote kwa mkupuo. Tangu jamvi letu livutwe chini ya miguu yetu kule BCS sikuwa na mahala pa kuvinjari. Nawaona wengi huku na mimi nafurahi kuungana nanyi. Kwa sasa niacheni ni "catch up" kwenye mijadala ndipo hapo baadaye walau nichangie. :D
 
Jasusi tumefurahi wewe kuungana nasi tena.....I'm glad you could find this site.

Hakuna kitu kinachonikera kwa serikali hii kama Mazingaombwe!!! Hivi mmesikia kiongozi yeyote kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi baada ya kuzama kwa MV Nyamageni na kuua watu 28 (au zaidi)? Kama Mhandisi na Mkurugenzi wa temeke waliohusishwa na kuangukwa kwa jengo lililouua mtu mmoja walisimamishwa kwanini hawa maafisa wa bandari za Musoma na Mwanza bado wako kazini? Zaidi ni kuwa JK amewataka wajiwajibishe wenyewe!!!

Kupiga watu mkwara "Mtaziona hasira zangu" haisadii kitu kwani baada ya mwezi mmoja hakutakuwa na mtu aliyefukuzwa, kusimamishwa etc. But I tell you this... muda si mrefu utasikia wafanyakazi wa ngazi za chini wakianza kufukuzwa wakati wakubwa wakiendelea kutanua!!!!

Iweje hadi leo hii wale walioingiza Tanzania katika mikataba bomu bado wako kazini?
 
Augustine,
Nakubaliana na wewe kwa kina fulani... na hasa nikizingatia mazingira na tamaduni zetu. Lakini tunaposema tunahitaji wasomi wengi ndipo tuweze kuweka sheria na utaratibu sidhani kama hilo litawezekana kesho wala kesho kutwa. Kumbuka vijana wengi wanaacha shule kwa sababu kama hizo.. kutoona mafanikio ya elimu mbele isipokuwa kiza, misheni town babu kubwa kuliko elimu maana mfanyakazi msomi hutegemea pato la mwezi zaidi ya hapo hana maendeleo kama hana ajira..Labda awe mwizi na mla rushwa! (Yote haya ndiyo hali yetu halisi)
Na ELIMU tunayojifunza ni Elimu ya wageni yaani wazungu wenye taaluma ya mambo yote, na Elimu hii imewekwa kwa makusudio ya UFANISI ktk kila kinachohusu elimu hiyo. Ndio maana wao wamefuata taratibu za elimu hiyo tunayojifunza sisi. Kifupi tunajifunza elimu yao kwa malengo tofauti kama vile tunavyokumbatia hiyo demokrasia yao.
Sasa ikiwa Azam kweli hakusoma uchanganyaji madawa ya chakula kuweza kuitengeneza hiyo Ice cream, kweli hapa kuna hakika gani ya afya ya wananchi ambao ndio wafanyakazi na wazalishaji. Na vile hana elimu hata kama kuna uzidishaji wa madawa yenye kuleta athari vigumu kumshitaki kwa sababu hata yeye anababaisha tu kupata fedha!..Na kwa vile hakuna sheria inayoambatana na elimu huyo msomi atapata lini nafasi ya kufungua mradi wake kama tutasubiri hadi Tanzania ajae wasomi. Na utaweza vipi ku-control utajirisho pale robo ya population nchini wamesoma!..)nadhani kufikia wakati huo wasomi watakuwa millioni 30), fedha itoke wapi?
Hii ni hadithi ndugu yangu haiwezekani kabisa! Leo tunashindwa kuwatajirisha wasomi wachache kwa sababu ya umaskini na mengine chungu nzima itakuwa hao mamillioni ya wasomi na huyo mrithi wa Azam utamnyang'anya liseni hali kampuni imekuwepo kwa karne nzima?

Mzee Mwanakijiji,
Swali lako zuri sana, inaonyesha tanzania ni Dar-es-Salaam lakini kumbuka kitu kimoja sisi binadamu huwezi kabisa kuchukua hatua pale maafa yamesababishwa na meli yenyewe ama mmoja kati ya wafanyakazi ambaye nae yupo ktk hesabu ya waliokufa!... Hili swala linahitaji upelelezi kabla ya kutoa hukumu tofauti na nyumba iliyoporomoka kutokana na ujenzi mbaya. Ni matumaini yangu swala hili linafuatiliwa kwani huyu mshirika halali.. Na nakuhakikishieni watanyooka! Baada ya usafi kazi moja tu KULIJENGA TAIFA!
 
Napenda kumfahamisha ndugu yangu Augustino Moshi kwamba uchumi wetu kudidimia unatokana na kudidimia kwa uchumi wa marekani ambao sisi ndio uchumi tunaoutegemea kwa kipindi hiki cha mpito.Kumbukeni kwamba bado tunanafasi kubwa sana ya kuukuza uchumi wetu kama JK ataweza kutumia kipindi chake vyema kufanya deal na wachina ambao hivi sasa ndio nguvu kubwa ya uchumi duniani,kama mnataka kuelewa nini ninazungumzia hapa angalieni mfano wa Nigeria ambao ndiyo nchi ya kwanza Africa kutangaza kumaliza madeni yote iliyokuwa inadaiwa ,vilevile sisi tunaouwezo nawa kufanya hivyo through rafiki zetu wakubwa china.
Vile vile napenda kumkosoa kidogo ndugu yangu Moshi kuhusu watu aliowataja kama ndio wana uwezo wa kumsaidia JK katika kuurudisha uchumi wetu na kuuendeleza ,nafaikiri Moshi amesahau na labda hana taarifa za mzimu Idd Simba ambao ninaamini mzimu kama yeye unaweza ukatupeleka mbele sana kiuchumi kutokana na uwezo wake kiuchumi ,kumbukeni huyu aliwahi kukiongoza chombo kimoja cha uchumi wa AFRICA ADB ni mtu mwenye strategy nyingi sana kiuchumi ambaye kutokana na uwezo wake mkubwa ninaamini JK ataweza kujitengenezea jina zuri sana kama ataweza kumhusisha mkongwe huyu katika masuala ya kiuchumi nchini,na mwingine ni mzee Mengi wa IPP media naye anauwezo wa kuleta maendeleo kwa taifa letu changa lenye resources nyingi .
KUmalziaa ni kwmba Mimi sina tatizo kabisa na kazi aliyoifanya Mkapa ,ni kazi nzuri kwa kweli alijitahidi kwa kiasi kikubwa sana kuliendeleza taifa letu kiuchumi.Kwa hilo ninampa hongera zangu nyingi na ninmpatia B++ kwa kazi yake safi sana.
peace!!!
Willo
 
Ndugu zanguni,
Amani iwe kwenu.
Nabisha hodi, baada kuona BCS imeyeyuka bila kujimwaga, nimeona sasa niwakti bora wa mimi kuanza kutoa kile nilicho nacho, hivyo nitakuwa nanyi hapa kwenye ukumbi huu.

wasalam
Makengeza
 
Mwalimu Moshi, kuna kila dalili ya Mv Kikwete kuzama, ili kukinusuru chombo kuzama nahodha[jk] anatakiwa kutupupa baadhi ya mizigo baharini ili chombo kifike salama pwani

Akichelewa kuchukua maamuzi mdhara yake yaweza kuwa makubwa
 
kppnu1.jpg


Credit: Michuzi blog
 
Hebu tuisome tena hii thread tufanye marejeo. Huko nyuma ilipoanza hii thread ilikuwa inahitaji uwe mwendawazimu kumkosoa JK, hadi bob Mkandara naye alikuwa.... Lakini sasa naona kumbe Mwalimu Moshi aliona mbali. Yake aliyoyaandika miezi miwili tangu JK aingie madarakani na wengi wetu hapa mkambishia ndio haya yametokea leo na kila mtu sasa anamtolea mimacho JK wakiwemo wale waliokuwa watetezi wake wakuu! Hongera Moshi kwa kuona mbali!
 
addda7lk6.jpg


Credit: Mjengwa blog.

Hazina sasa kunaanza kuwa kweupe tunabaki kama huyu jamaa. Omba omba wa kimataifa.
 
Mwelekeo wa uchumi wa Tanzania baada ya miezi 3 ya utawala wa Rais Kikwete ni mbaya kuliko tulivyohofia! Quartely Econmic Review iliyofanywa na BoT pamoja na wanauchumi wengine wa Afrika Mashariki inaonyesha hali ya umbio wa kudorora uchumi ambao kasi yake ni zaidi ya mategeo ya watu wote.

JK hana dira ya kupambana na energy crisis iliyojitokeza. Athari zake bado zinaongezeka, na haelekei kujihusisha kikweli na kutafuta jibu.

JK alipokea nchi ambayo uchumi wake ulikuwa unakuwa vizuri, na kasi ya kukua kwake ilikuwa inaongezeka kila mwaka, hata kukiwepo ukame. Alikabidhiwa taifa lenye GDP growth rate ya 7% na ambayo ilikadiriwa kufikia 7.2% mwaka huu. Chini ya uongozi wake, GDP growth rate hiyo imeshuka hadi kufikia 5.8%, na inazidi kushuka.

JK alikabidhiwa taifa lenye inflation rate ya 4%, na kwa kipindi kifupi tu ameiacha ikapanda hadi kufikia 5% sasa, na mwelekeo ni kuongezeka siku za karibuni hadi 6%.

Baraza kubwa la mawaziri wa JK na matumizi yao mabaya yameongeza quartely government spending kwa kiasi cha sh. 157 billion. Hizo ni fedha nyingi sana kwa nchi kama yetu.

Interest rate za Treassury bills zilikuwa 10.4% wakati JK anachukua nchi. Sasa zimefika 14.8%. Hii ni rate kubwa sana (linganisha na Kenya ambapo interest rate on Tbills ni 6.7% only).

Serikali ya JK imetumia fedha nyingi sana, lakini wakati huo huo imepunguza matumizi kwenye vitu muhimu kama mikopo ya wanafunzi! UDSM watoto wanahaha njaa kutokana na kutopewa mikopo.

Kinachoogopesha zaidi ni ukweli kwamba hadi sasa, JK amekuwa na maneno mengi lakini matendo hakuna. Anatoa ahadi kibao, lakini maswala muhimu kama mikakati ya kushughulikia tatizo la umeme (and energy as a whole), na inflation, hana muda nayo.

Ndege ya JK ni nzuri, lakini sio lazima aruke nayo kila siku. Atulie ofisini kidogo ajenge VISION ya namna ya kuongoza nchi.

Kwa maoni yangu, JK angepashwa kuendelea kuwategemea Kigoda na Mramba waongoze uchumi wetu. They have a vision while he doesn't. Hao Waswahili anaoambatana nao hawana dira ya maendeleo! Wanatupeleka kwenye umasikini zaidi na zaidi.

Augustine Moshi[/b]

Wow!! Kila kitu alichoongea Mwl. Moshi hapa ni ukweli mtupu na kinaonekana leo hii.
 
Msimlaumu JK kwani meli aliyoachiwa ilikuwa na matundu mengi sana na sasamaji yameanza kuingia ndani ,siwezi kushangaa kama meli hiyo itazama na kama kweli akitaka meli hiyo izame basi awarudishe akina KIgoda na Mramba ambao ndio wahusika wakubwa katika kutoboa matundu katika meli yetu.Msiwe na wasiwasi na statistics hizo lengo lake nikupunguza kasi ya JK katika kupambana na majambazi walioiibia serikali yetu na kujilimbikizia mali hali inayojitokezandio matunda ya ujambazi uliofanywa na administration iliyopita .Tusimlaumu JK kwahaya kumbukeni kwamba natural gas itambeba vizuri sana .
Hongera JK endelea na kupambabana na wezi na walioiba mali yetu wote wachukuliwe hatua za kisheria na warudishe mali zetu zote walizoiba kutoka kwetu.Augustine kazungumzia kuhusu wanafunzi kukosa mikopo lakini amesahau kwamba pesa zote zilichukuliwa na baadhi yawatu walioukuwa katika uongozi wa juu na ni watoto wao ndio wanaosomeshwa nje ya nchi,wengine tunakutana naoviwanjani .JK atawanyamazisheni midomo kama ilivyotokeakwenye mbio za urais.

peace!!!

It is true that JK is failing, Agustino aliyonena ni kweli. Huyu jamaa kakuta hali ya uchumi ni nzuri mno kiasi kwamba tulitegemea meli yetu inge sail hata katika dhoruba kali. Cha ajabu yeye ndiye kaiongezea matundu makubwa, ndiyo ilikuwa na matundu lakini sio makubwa kama haya aliyoyatengeneza JK.

Willo nafikiri umesahau mazuri aliyoyafanya Mkapa, nitaendelea kumtetea Mkapa na kumuenzi kwa kuufikisha uchumi wetu sehemu nzuri. Mkapa alikuwa na udhaifu wake na mapungufu makubwa tu, lakini hauwezi kulinganisha na usanii huu tunaoushuhudia sasa. Kila kitu kinakwenda kombo kiasi kwamba wananchi wanapoteza imani na watawala jambo ambalo ni baya sana. Ogopa sana mtu ambaye anaweka matumaini kwako akakupa support ya kufika mahali kisha unamtosa, he/she's going to loose confidence with you.

Kikwete amekuwa akizunguka tu, siasa ndio kipaombele, michezo cha pili. Usalama wa raia ni wajibu wake, kwani ameapa kuwa atahakikisha kuwa sisi na mali zetu tutakuwa salama na tunamlipa hela zetu za kodi kwa hilo, kwa hili hawezi kujisifu, hii ni sawa na baba katika familia yako, hauwezi ukajisifu kuwa familia yako imekula na wanamahali pa kuishi kwani ni wajibu wako, labda uwe mwendawazimu usiyejua wajibu ndo utajisifu.

Ni lazima serikali hii ijue vipaombele vyake, sio kukimbilia kununua mashangingi kwa bei zilizobebeshwa 20% kickbacks na kuzungunguka kuelezea mikoani kuelezea uzuri wa bajeti, pale bungeni kwa kipindi cha miezi miwili mlikuwa mnafanya nini na wawakilishi wetu. Kuna haja gani ya wabunge kwenda bungeni Dodoma ikiwa mnaweza kuja kutuelezea bajeti moja kwa moja sisi wananchi mikoani. Haya ni matumizi mabaya ya Kodi zetu. Hospitali hazina madawa na vitanda, shule hakuna madarasa na madawati, walimu wana mishahara duni, barabara vijijini kwa ajili ya kusafirisha mazao ya wakulima hazipo na hakuna anayejali mmebaki kuzunguka tu na kupiga siasa.

Natamani hizi siasa zisingekuwepo mnamweka mtu kuongoza na wawakilishi wa kumchunguza, pia asiwe mkuu wa majeshi. Ingependeza sana
 
mv kikwete inazama na inazama kwa kasi kubwa. ila tatizo kubwa zaidi sio kwamba hana nia ya kuendeleza nchi, tatizo lake ni kuwa hana vision. mambo ya uchumi sio fani yake, anashindwa kupambana nayo kwa vile hana msaidizi.

angejaribu kuweka mawaziri wapya akaona ingekuwaje, sio kung'ang'ania kitu ambacho tayari anajua kuwa hakina maana kwake na kwa wananchi wote
 
mv kikwete inazama na inazama kwa kasi kubwa. ila tatizo kubwa zaidi sio kwamba hana nia ya kuendeleza nchi, tatizo lake ni kuwa hana vision. mambo ya uchumi sio fani yake, anashindwa kupambana nayo kwa vile hana msaidizi.

angejaribu kuweka mawaziri wapya akaona ingekuwaje, sio kung'ang'ania kitu ambacho tayari anajua kuwa hakina maana kwake na kwa wananchi wote
Uchumi siyo fani yake au ni Fani yake ? Si Kiongozi Bora kwani Usimamizi na utekelezaji mbovu wa sera za kiuchumi za chama chake kupitia serikali aliyoiunda umebakia kwenye makabrasha pamoja na kuwa uchumi ni taaluma na fani yake!
 
JK atawapiga dafrau wahusika wote wa ufisadi akitumia cheo chake Cha Uraisi pia kama Jemedari Mkuu ,mimi nawashauri mafisadi kama wakipata nafasi wakimbie kusiko julikana ,lakini hii kupita pita mitaani resi na magari yao kuonyesha jeuri na kugonga watu itawatokea puani mida si mrefu ,nawambia tena ondokeni na tafuteni safari ikiwa pasi zimezuiwa basi japo punda pandeni mkorosi boda.

WaPemba wanasema Ng'ombe mkali amekwisha kata kamba ,mnao sali uwanjani mchague kama mwaitaka jela endeleeni kuswali la mwaitaka dunia basi kimbieni.
 
Back
Top Bottom