Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Ushauri wangu kwa SMZ wanapopinga Muswada wa Katiba pamoja na kuukataa muungano, iwapo kweli wana nia ya kujitenga kama nchi kamili na nia thabiti, watusaidie yafuatayo:
1. Wawaite Wabunge, mawaziri na viongozi wengine wa Zbr wote walio ktk Jamhuri ya Muungano waachie nyadhifa zao na kurudi Zenji,
2. Waitishe mjadala/maandamano ya kupinga/kujitoa ktk muungano,
3. Watoe tamko kama SMZ kuwa wao kama nchi kamili kuanzia sasa wanauvunja muungano na UN iwatambue hivyo.

Kwa kufanya hivyo mtaturahisishia sana na tutawaheshimu kuliko kutishia nyau!
 
Si tuulizwe sisi wananchi kama tunautaka huu muungano au la, Sidhani wengi wetu tutaathirika kama muungano ukivunjwa.
 
Nachelea kusema mtoto akililia wembe mpe, kwa kuwa baada ya muungano kuvunjwa hata znz itavunjika moja kwa moja, yaani sambamba na muungano na yatakayofuata ni mauaji ya kimbari.Waznz wenye akili timamu hawaombi muungano kuvunjika,wanadai muungano kuvunjika ni waznz wachache ambao wanatamaa ya kupata post tu kushibisha matumbo yao, basi. Nyerere alisema nje ya muungano hakuna zanzibar, kuna unguja na pemba, kama mnafikiri maneno yake ni ya kipuuzi vunjeni muungano muone, maana hapo mtabaini kweli nyerere alikuwa ni nabii , hakuwa mtu wa kawaida kama tulivyo sisi.
 
Suala zuri kabisa. Sisi wazanzibari tunakwetu tutarudi na nyinyi watanganyika muna kwenu murudi. Sasa, kwa kuwa kuna demokrasia, watu wataamu wanapotaka kuishi. Sisi wazanzibari hatuwafukuzi binaadamu kuishi zanzibar. Hatuna chuki na raia. Matatizo yetu ni kuburuzwa na watawala. Wananchi hawatuletei matatizo yoyote bali muungano na viongozi wake ndio tatizo.

nyie wazanzibar ndo mrudi kwenu , sisi watanganyika tupo TANGANYIKA na tutaendelea kubaki TANGANYIKA
 
AHAA sasa zanzbar ukija lazima owombe visa tena iyambatane na barua ya mualiko ya mzawa wa zanzibar akupatie,na visa itakuwa dola 100,ila lazima uwe na bank statement inayoonyesha una kiwango cha dola kuanzia elfu40,tutakusumbua kama ubalozi wa america na uk,suala la barua sijui mzanzibari gani atakupatia.

likewise
 
mtoto akililia wembe mpe.
hivi bara tunafaidi nini cha msingi kiasi cha kuwashikilia zenji namna hii?
 
CUF bara wataendelea kuwa imara sana maana mpaka sasa kinachowaharibia ni siasa za Upemba na Uunguja
 
Ndugu yangu, si afadhali ya hao WATANGANYIKA na WAZANZIBAR wananchi zao ambazo ni TANGANYIKA na ZANZIBAR na Sisi WATANZANIA je? Ambao ni ZAO kati ya mtz na mznzbr,TUTAKWENDA WAPI?
NZURIPESA.
Hili ulisemalo hapa si tatizo, pale ulipozaliwa, au ulipofanya makaazi yako ndio itakuwa nchi yako.
Wala huu wasiwasi wa watu watakuwa nani au wataishi vipi si tatizo kama mchakato utakuwa ni wa majadiliano na ridhaa na sio vita.

Bila shaka yoyote tayari kuna sheria za kimataifa zinazohusu muungano unapovunjika na haki za wananchi au raia.
Pia kuna sheria za stateless people.

Tusiingiwe na woga au kujitisha.
Warundi na warandwa wamepewa uraia wa Tanzania hivi karibuni kwa maelfu na malaki. so that is not an issue.

kama muungano uvunjwe, basi iwe kwa kupiga kura ya maoni, ambayo ni njia ya salama na kidemokrasia.

Na kila hatua huwa imewekewa wakati maalumu... fuatilia Sudan ya kusini....
 
Suala zuri kabisa. Sisi wazanzibari tunakwetu tutarudi na nyinyi watanganyika muna kwenu murudi. Sasa, kwa kuwa kuna demokrasia, watu wataamu wanapotaka kuishi. Sisi wazanzibari hatuwafukuzi binaadamu kuishi zanzibar. Hatuna chuki na raia. Matatizo yetu ni kuburuzwa na watawala. Wananchi hawatuletei matatizo yoyote bali muungano na viongozi wake ndio tatizo.

Hivi mwanzisha mada ni Mtanganyika?
 
Hee,kumbe muungano bado upo?Mi nilijua umeshavunjika kitambo tuu!!

Mkuu.
Muungano upo kinadharia na kimabavu..lakini Muungano kisheria haupo tena. Kwa sababu mambo mengi yamefanyika kimakosa ambayo yanaufanya Muungano kisheria uwe haupo tena.

Haya ni baadhi ya makosa yanayofanya muungano kisheria haupo.
-Kupotea kimiujiza kwa jina la mmoja wa mwazilishi wa Muungano na vyombo vya mamlaka yake.
-Kukosekana kwa majadiliano endelevu ya pande mbili zilizoanzisha muungano huu.
-Bunge la Muungano kujikombea uwezo bila ya kupewa na wabia wa muungano.
-Kumuondoshea Rais wa Zanzibar ambaye ndie kiongozi wa wazanzibari nafasi ya Umakamo wa Rais wa Muungano.
-Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ambayo hayaendani na Katiba ya Muungano.

Ukiangalia makosa haya yote yametokana na kosa la mwanzo. Kwamba hakuna majadiliano ya wabia wa Muungano ambao ni Tanganyika na Zanzibar.

Kwa hiyo ,mkuu, muungano upo kiusanii na kimabavu tu.
Na ndio sababu Mswada huu wa Katiba mpya umetaka Muungano uwe off-limit! Usiguswe.Usijadiliwe.
 
WakatiTaifa la Tanzania likiwa limetawaliwa na mijadala ihusuyo katiba mpya ya Jamuhuri, kumeibuka sura mpya juu ya mijadala hii! Muda mfupi baada ya serikali kuibuka na Muswada mbovu wa sheria marekebisho ya katiba tena kwa hati ya dharura kumeibuka hisia kali juu ya mambo yahusuyo mustakabali wa jamuhuri ya Muungano wetu.

Wakati wananchi wa upande wa bara waki "doubt" udhati wa dhamira ya serikali ya CCM katika kufanikisha mcahakato wa Upatikanaji wa katiba mpya itakayo tokana na wananchi kwa mara ya kwanza, wananchi wa upande wa pili wa muungano (Zanzibar) wamefika mbali zaidi kwa kufufua hoja ya kutoutaka muungano ambayo imetamalaki miongoni mwa wakazi wa visiwa hivi vya karafuu kwa muda mrefu sasa.

Kwa mtu aliepata kuishi katika visiwa hivi atakubaliana na mimi moja kwa moja kwamba wakazi wa zanzibar huuona muungano kuwa na manufaa kwa viongozi tu ambao ndio wanautetea kwa nguvu zote, wananchi hawaoni tija ya muungano huu. Tatizo limekuwa ni jukwaa la kuwasilisha hoja kama hizi ambazo ni mwiba wenye sumu kali kwa viongozi wanaoneemeka kwa kuwepo kwa muungano huu.

Hali kidogo iko tofauti kwa wakazi wengi wa Tanzania Bara ambao niniweza kusema hawaelewi mengi kuhusiana na muungano mbali na kuona umuhimu wa muungano huo katika maisha yao.

Kimsingi mimi nachelea kukubaliana na dhana kwamba mpaka wakati huu ni viongo wachache ndio wanafaidi zaidi matunda ya muungano japo siamini kama muungano hauna manufaa yoyote kwa wananchi wa Jamuhuri hii. Changamoto inabakia kwa viongozi kuweka mslahi binasfi kando na kuanza kushughulikia matatizo ya wananchi ili kuufanya muungano uwe na tija na hapo hata katiba tarajiwa itapata heshima ndani na hata nje ya nchi hii.
 
:yield:

Ukweli kwa yanayotokea Zanzibar ni changamoto mpya kwa serikali ya CCM na CCM yenyewe......ni changamoto kubwa sana zaidi ya wanavydhani

Swali kubwa ni kuwa, Je CCM na serikali ya Kikwete watakuwa tayari kuwapa Wazanzibar hitaji lao la kuwa huru kutoka Muungano kama ambavyo wengi (sio wote) wao wanatamani?

Ninachojua ni ngumu kwa CCM kukubali kupoteza hodhi ya chama chao kwenye serikali ya Zanzibar na hakuna atakaekubali kati yao kuweka historia ya Muungano kufikia tamati mikononi mwao.....


Hapo ndipo ninapoiona nia ya JK ya kutaka suala la Muungano kutokuzungumzwa kwenye mapendekezo ya Katiba mpya.
 
CCM na serikali wameshikwa pabaya mwaka huu!
Kushoto yuko Slaa..kulia wapo wazanzibari. Mbele kuna nguvu ya umma, nyuma kuna ukuta.

Kweli ni changamoto na hapo ndio uwezo wa mtu ailyetamba kujitayarisha kuchukua uongozi kwa miaka kumi atakapojulikana kama ni kiongozi.
 
Back
Top Bottom