.''Kila nchi inastaili yake ya kujiunga, hapa sisi tunaitambua Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania na wala si Tanzania au vinginevyo,'' alisema Dk. Migiro.
Kuna kitu ambacho tunapaswa kutenganisha, sovereign state na state. Zanzibar ni nchi ambayo haina soverignity yake binafsi. Sovereignity yake inapatikana kupitia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachodaiwa kwa mlango wa nyuma hapa ni sovereignity na si swala la Zanzibar kuwa nchi. Tupende tusipende muungano wa Tangznyika na Zanzibar umefikai mahali, kama ilivyo miungano mingine ya jinsi hiyo hufikia. Mathalani kunavuguvugu United Kingdom ambapo Wascot, kama Zanzibar, wanataka uhuru wao kamili ili wawe sovereign state.
Kuna mashabiki na wapinzani wa muungano huu toka zamani, itakuwa vema sasa tufikie mahali tuamue ki utu uzima bila aibu kutathmini kama kuna haja ya kuendelea kuungana au la. Potelea mbali hata kama wengi watataka tutengane turidhie. Nini kitkachotokea ndani ya kila nchi hapo baadaye itakuwa mambo ya ndani ya nchi husika. Tutafuata msahafu wa AU wa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Kuan kila aina ya vitisho kwa wachangiaji mbalmbali, kwa nini tusifuate njia ya Czechoslovakia? Tutngane tukiwa na mapenzi kati yetu. Tusikubali kuambukizwa chuki ya kuwa kuna upande mmoja unafaidi zaid au unambeba/unabebwa na mwingine. Kabla ya muunganotuliishibila matatizo, labda tu hayo Mapinduzi.
Hey East AFrica, Zanzibar is not sovereign. you, especially non tzs should get the constitution of the united Republic of tz and read it well. Zanzibar is neither a state not sovereign or whatsoever, its more or less a province of Tz like Arusha, Dar or Kilimanjaro. the thing which is happening here is that, the zanzibaris want to depart from Tanzania mainland because they think they are sufficient of themselves cuasue of discovery of oil in Pemba, so wanataka wayafaidi yale mafuta with exclusion of watz mainland. Na kweli kuna mafuta mengi sana kule na kama zanzibar wakiamua kujitenga na tz wakayachimba, kila raia wao atakuwa tajiri sana kwasababu utajiri wao utakuwa mkubwa kuliko uwingi wa watu. zanzibar is below 1 mil. population. it is not easy for them to be independent from Tanzania unless the constitution of the United Rep.of tz is amended to exclude it.
Mkuu Mbeba Maono,
Mimi binafsi, sikubaliani na usemi kuwa Zanzibar is a total sovereignty na vile vile sikubaliani na huo usemi wako kuwa Zanzibar ni sawa na mkoa wowote wa Tanzani. Na kama pana utata, waliosababisha utata huu ni waasisi, Wazee wetu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume.
Wakati, Mzee Nyerere, alikubali kwa niaba yetu kupoteza total sovereignty ya Tanganyika ndani ya Tanzania, Mzee Karume, aliusitukia mpango huo, akataka kwa niaba ya wenzetu, kubakiza sehemu kubwa ya sovereignty ya Zanzibar kwa Wazanzibar wenyewe na kiasi kidogo tu cha sovereignty yake ndio kiwe chini ya himaya ya Tanzania.
Mpango huu, kwa hakika haujapata kutokea popote duniani. Kwa nini waliukubali? Ni mpango ambao haueleweki kabisa. Na ndio maana Mzee Nyerere hakuweza kuzidisha yale mambo 11 ya Muungano wala kuunganisha TANU na AFRO-SHIRAZI mpaka baada ya Mzee Karume kufariki. Mzee Karume aliukataa Ujamaa mbele ya Mzee Nyerere. Na kama si Mzee Karume kufariki naamini Zanzibar mpaka kesho ingekuwa mwanachama wa IOC.
Na kama angekuwa bado yupo hai, kwa matamshi ya Waziri Mkuu Pinda ndio ingekuwa mwisho wa muungano wenyewe.
Tukae chini turudi ubaoni, tuupange sawasawa muungano wetu huu. Ingawa hatupendi kusikia, lakini bila ya kusikilizana na Wazanzibar, muungano huu utakwenda alijojo, mafuta or no mafuta. Muungano wa 2-10 hautawezekana.
Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania. Hicho kinachoitwa sehemu ni nchi, hata kwa jina gani lingine. Kama vile Tanzania Bara ni Tanganyika tu, hata ukitamka kwa mung'unya. Na tanganyika ni nchi hata kama si sovereign.
Dk. Migiro either ameboronga au amekuwa misquoted.
Nchi haiwezi kuwa mwanachama wa UN kama nchi hiyo si nchi sovereign, that is true.
Lakini at the same time kutokuwa mwanachama wa U.N hakumaanishi kwamba wewe si nchi sovereign. U.N ni taasisi ya kimataifa kama nyingine nyingi, kuna nchi sovereign kama Switzerland ambazo kutokana na principles zake za neutrality na interests zake za banking zimeamua kutokuwa member wa U.N and many international organizations such as the E.U, NATO, SHENGEN and what not.Hii ni kwa sababu wa Swizi hawataki mikataba ya taasisi hizi iwafunge, hawataki ku abide to U.N resolutins ambazo zinaweza kuwa na implications kwenye banking industry yao na vitu kama hivyo.
Kwa hiyo kuleta issue ya uanachama wa U.N, which insinuates that as a criteria ya ku determine kama Zanzibar ni nchi au siyo at best ni upotoshaji.
Mwandishi anaruka left right and center lakini haja address swala muhimu, nini kinafanya nchi kuwa nchi?
Kuwa nchi sio lazima itambuliwe na UN au sovereign. Tanganyika ina sovereignty na Zanzibar ina sovereignty ndani ya sovereignty ya Tanzania.
nimeangalia kwa muda mrefu sana nimesoma waandishi wote walio changia mada ya zanzibar inchi au sio nchini nimegundua kuwa wote walio changia wanataka muungano wengi wao ni watu wa upande wa bara kwa upande wa visiwani naona wao hawautaki muungano sasa iweje upande wa bara wang'ang'anie muungano inaonyesha kweli kuna kuibiana tangu lini mtu mzima akafanya ushirika na mtoto hapo si kutaka kumuibia tu hakuna sheria yoyote duniani inayo sema nchi kubwa kuungana na nchi ndogo lakini madhali mumeungana huyu katoa chake na wewe umetoa chako usiangalie udogo au ukubwa kuwa wewe ni mkubwa ndio uchukue kila kitu tugawana sawasawa kwahiyo watu wa bara wao ndio wanao utakla muungano ili wazidi kuwanyonya
SAKATA la hadhi ya Zanzibar kama ni nchi au la, limezidi kupamba moto baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Asha-Rose Migiro, naye kujitosa katika mjadala huo kwa kusema nchi inayotambuliwa na Umoja huo ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na wala si Zanzibar.
Huu ni msimamo wa UN, hauna uhusiano na anything na mjadala unaoendelea bongo sasa hivi kwa maoni yangu, wacha this local mjadala uendelee ili labda tutapata permanent solution ya this nonesense muungano thing!
Mkuu unless kuna something missing hapa, Mama ambaye ni katibu mkuu wa UN, Tanzania kama nchi lakini haiitambui Zanzibar kama nchi ninaweza nikaamini kuwa anasema ni represented ndani ya part of nchi Tanzania, kama mkoa sioni tatizo na huu usemi kwa sababu haungiliani kabisa na mjadala unaoendelea Tanzania sasa hivi
Huyu mama alitakiwa kunyamaza tu kuhusu hii issue, ama sivyo atajua Tanzania watu hawana akili au adabu, bahati yake hawajaidaka hii.
naomba mtu anipe: (akitenganisha bara na visiwani)
1. faida/hasara za muungano huu
2. faida/hasara za kuuvunja
Naomba legacy ye nyerere isiwe mojawapo ya vigezo.