Zanzibar ni kama katoto kadogo kama alivyobainisha Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake. Mtu mzima unakapakata katoto halafu kanakunyea -eti lazima uendelee kukabembeleza kwa sababu ukikakoromea kidogo tu kataanza kulia myee, myee !! Hapa mie naona JMK yuko sahihi ingawa sina hakika kama ni kwa kudhamiria (kwani hekima hiyo hana). Zanzibar haina hata sifa ya kuwa mkoa lakini basi ni katoto - lazima kabembelezwe. Nchi ? My foot.
 
There is only one country called United Republic Of Tanzania. Zanzibar and Tanganyika ceased to exist in 1964 April 26th. Zanzibar maintains some Autonomy; but is not a country. All countries are recognized by United Nations; Zanzibar is part of United Republic of Tanzania. Therefore Zanzibar is NOT a country.

Unfortunately, nobody in the SMZ seems to now this fact.
 
Kumbe hata sheria ya taifa letu huijui, kwamba huwezi kuwa waziri katika serikali ya bara wla visiwani, bila kuwa mbunge either wa kuchaguliwa na wananchi au rais, either wa bara au visiwani?

Shamuhuna ni mbunge, ndio maana akawa waziri, kwa hiyo mahali muafakapa ye kutoa kero zake on mungano ni kwenye bunge la jamhuri ambako ana haki kisheria ya kuingia kama mbunge an waziri na hasa Deputy Waziri Kiongozi,

Kwenda kuongelea kero zake za muungano, kwenye Baraza la Wa Wakilishi ambako wabunge wa bara hawako mandated kuhudhuria kisheria ni tabia mufilisi ambayo ndio hasa tunayoikataa hapa.

Mkuu,
Hapa umeteleza kidogo. Shamhuna ni Muwakilishi na sio Mbunge. Hawezi kuingia kwenye Bunge la Muungano. Unajua wenzetu Znz majimbo yao yana muwakilishi na mbunge. Ninachokiona mimi labda kuwe na kautaratibu ka kuyakutanisha mabaraza haya mawili angalau mara moja kwa mwaka. Hili likitumika vizuri linaweza kutatua tofauti hizi ndogo ndogo nyingi tu.
 
Bora usife sisi wengine tumeoa bara!!

Huyu ndiye aliyesema ukweli. Tumeoleana, hakuna purity tena. Tunapowazungumzia wazanzibari tunawazungumzia wake zetu, wame zetu, shemeji zetu, ndugu zetu, rafiki zetu, wafanya kazi wenzetu, jirani zetu, wanafunzi wenzetu na ninaamini ni hivyohivyo kwa wazanzibari. Hili ndilo linalotuunganisha na si kikaratasi ambacho hakuna anayejua kilipo. Na ni hiki kitakachotufanya hata hapo mtakapoanza kukatana mapanga tuwape hifadhi.Ndiyo hali halisi.
 
mwiba!

usiwapoteee watu muda wana mambo engi na ya muhimu ya kuongelea na kuyafanyia kazi, tunajua kwamba Lowasa amenunua magazeti na waandishi wengi tu, na anaendelea kununua kila mtu anayeweza kumsafisha pale alipo,,

hofu yangu ni wewe kuizungumzia hoja ya mwakyembe na kumuangusha Lowasa, unaonekana kama vile umenunuliwa na unajaribu kumuosha lowasa wako, lakini umepotea njia wana JF wote wanamjua lowasa zaidi ya unavyomjua.

very pole bwana
 
Well, if that's the case, then this whole Katiba thing is totally messed-up! So ninachokiona hapa ni hiki: Mwl na Karume hawakuweka mambo mengi (yanayohusu Muungano) bayana. Perhaps walikuwa too excited kipindi walipokuwa wanafunga hii ndoa ("Oh, tunaungana..., Sasa Afrika yote itafuata..."). Therefore, hawakuchukua muda wa kufikiria kwa undani (wala kutazama mbali) na kutambua confusion zitakazojitokeza baada ya wao kuwa wameanza.

Ni kweli Gustanza, maana kwa excitement aliyokuwa nayo mheshimiwa Karume, alifanya mapinduzi Unguja tu, hakukumbuka kupeleka watu Pemba hadi alipohimizwa na Nyerere, kuwa asipofanya hivyo, angepinduliwa na watu walioji mobilize Pemba.

Pili, siwalaumu kwa kushindwa ku foresee matatizo ya namna hii ukizingatia hali ilivyokuwa wakati ule na level of understanding ilivyokuwa. Cha msingi ni kukubali kurekebisha matatizo yetu.
 
Hivi kuna uwezekano wa kupiga kura zaidi ya mara moja kuhusiana na hili suala? Naomba nipige kura nyingine ya Ndio
 
There is only one country called United Republic Of Tanzania. Zanzibar and Tanganyika ceased to exist in 1964 April 26th. Zanzibar maintains some Autonomy; but is not a country. All countries are recognized by United Nations; Zanzibar is part of United Republic of Tanzania. Therefore Zanzibar is NOT a country.
Bora usome tu ,kwa maana naona unajizonga , hivi unafahamu maana ya United na kwa nini bada ya kuunganishwa na kuungana na kuwa Nchi moja kama unavyoona wewe isiitwe Tanzania ,tumeungana tumekuwa kitu kimoja nchi yetu itaitwa Tanzania ,au sivyo ? Wandugu Zanzibar ni Nchi ,tuache longolongo na kuukana ukweli.
Naona hiyo Katiba viraka makosa yake sasa yanaaza kuumbuka au kuibuka kosa lililopo walishindwa kuiwakilisha Zanzibar pale walipoandika Zanzibar ni sehemu ya Tanzania ,Hebu angalia Mkoa wa Mtwara ni sehemu ya Tanzania,Wilaya ya Handeni ni sehemu ya Tanzania ,sasa Zanzibar ni kitu gani ?
 
Jambo La Kusikitisha Na La Aibu Ni Pale Tunaposhuhudia Viongozi Wa Nchi Tena Wabunge Wenye Kutuwakilisha Sisi Wananchi Wanapo Kosa Maadili Yao Na Kujihisi Kama Wako Kijiweni ,tena Kijiwe Cha Wavuta Bangi. .zamani Ilikuwa Ni Aibu Kuwasikia Watoto Wanatupiana Matusi Mbele Ya Watu Wazima ,iweje Leo? .

Mbunge Kumwambia Mbunge Mwenzake Huna Adabu ? Kama Alikosa Adabu Kwa Kuitetea Nchi Yake Kama Anavyo Amini Mwenyewe ,nyinyi Si Mnavyo Vikao Vyenu Vya Chama Mnayo Kamati Yenu Ya Nidhamu Kwa Nini Msimwite Huko Mkashikishana Adabu ?

Kama Ni Kweli Tamko Au Agizo Alilotowa Waziri Mkuu Halipaswi Kujadiliwa Tena Na Mbunge ,na Kufanya Hivyo Ni Kukosa Adabu , Kwa Nini Wewe Ulikubali Na Kupokea Kumjadili Waziri Wako Mkuu Lowassa Na Hata Kufikia Kujiuzulu Yeye Na Baadhi Ya Mawaziri Wengine ? Jee Na Wewe Tukuite Vipi ?

Kuna Mambo Ambayo Yanahitaji Kabla Ya Kuyazungumza Hadharani Kwanza Myafikiri Na Ndipo Mutueleze Sisi Ambao Hatukusoma ,au Mtatuchanganya.

Nilifikiri Tumeweza Kujifunza Tabia Za Kuheshimiana Na Kukosoana Bila Ya Kutukanana . Lakini Leo Tunashuhudia Watu Wasomi Wenye Elimu Za Juu Mapr.o Na Phd Zao Wanaongea Kama Walevi Na Makuhani .nani Mwenye Haki Ya Kumtusi Mwenzake Ndani Ya Ccm ?

Tunajuwa Suala La Zanzibar Limewaudhi Sana Watawala Wetu Na Wakoloni Wetu Na Wanataka Tusilijadili Hasa Mpaka Wamalize Kazi Walioachiwa Na Bwana Wao Nyerere . Lakini Tunasema Hilo Haliwezakani ,na Hayo Hayakuwa Makubaliano Na Karume .tukae Pamoja Kwa Kuheshimiana Sio Kutishana ,wakae Wasomi Kujadili Muungano Sio Kupeana Matusi Na Kejeli Na Dharau .haya Hayatosaidia Kujenga Umoja Na Undugu Ambao Upo Kabla Ya 54 Zilipo Anza Hizo Siasa Kabla Ya 49 Ilipoanza Hiyo Fitna


Kama Uganda Rai Wake Ni Waganda , Kenya /wakenya , Tanganyika Ni Watanganyika ,basi Na Zanzibar Watu Wake Watabaki Kuwa Ni Wazanzibar Msitufunike Gunia La Muungano Na Kusema Sisi Ni Waafric Hii Ni Kwa Ajili Ya Kuwapotosha Watoto Wetu Na Dunia Tu Kwa Maslahi Yenu.
 
Mwakyembe na Pinda, wameyasema kwenye kikao cha pande zote mbili, bunge la jamhuri linahudhuriwa kisheria na wabunge wa Zanzibar na Bara,

lakini kikao cha wawakilishi hakihudhuriwi kisheria na wabunge wa bara, kwa hiyo mahali muafaka kisheria na kisiasa pa kuhoji maswala ya muungano ni kwenye bunge la pamoja, yaani la Jamhuri ambako ndiko Pinda na Mwakyembe, walipotoa hoja zao, sasa kipi ni kigumu kuelewa hapa?

Mkuu hiyo usemayo wewe si sahihi kwani hata sheria inayotaka kupitishwa bungeni ihusuyo mambo ya Muungano hujadiliwa kwanza na Baraza la Wawakilishi. Nakupa mfano kuruhusiwa kwa tume ya haki kufanya Zanzibar kazi ilibidi ipitishwe kwanza Baraza la Wawakilishi. Suala la Bandari likwamishwa na Baraza la wawakilishi.
Kwa hili la suala la Zanzibar hata likiwa la Muungano linabidi lijadiliwe Zanzibar halitaki mtu aliyesoma kama wewe kufahamishwa liko obvious kuwa Wawakilishi wa Zanzibar wana haki ya klijadili suala la Muungano na hata kwa Chama si kuna kamati maalum ya Chama Zanzibar inayokaa na kujadili mambo ya Zanzibar na baadae kupelekwa DODOMA kwa nguvu ya utekelezaji.
Kama zilizoungana ni sehemu mbili kila mmoja ana haki ya kuangalia intrest zake,jamani hata hilo mtu mbumbumbu kama mimi nikufahamishe, Mwalimu wangu?
 
Nafikiri kwa mawnazo yangu ya kukosa elimu, tungekuwa Wastaarabu na tukakubali kuwa Muungano wetu una matatizo na tusitumie kigezo cha kuwa upo kwa miaka 44 kuhalalisha kuwa hauna matatizo.
Matatizo ya Muungano yapo pande zote mbili lakini kwa bahati mbaya tofauti ya ukubwa wa nchi zetu zinaashiria namna ya athari na uwezo wa kuhimili athari za mapungufu ya Muungano huu. Kila mmoja ana haki ya kudai namna anavyoumizwa na muundo wa Muungano huu lakini inapobidi kusema ukweli basi tuseme ukweli ili tutatuwe tatizo.

Ndani ya Muungano wetu kuna mambo makubwa mawili yanayokwenda pamoja ambayo ndio chanzo cha malalamiko na kutofamiana huku. Mambo mawili hayo ni Utegemezi na Kubanwa. Utegemezi unakuja pale Zanzibar haitowi mchango unaoonekana kwenye shughuli za Muungano. Naomba pande zote mbili msinifikirie vibaya lakini hii ndiyo kweli ninayoiona. Kuna sababu, lakini ni hali halisi kuwa Zanzibar haitowi mchango unaoonekana kwa Muungano na hii imesababisha kuwa Wadhaifu katika Muungano na hivyo kuonekana kuwa upande mmoja tu ndio unaoexist. Kwa mfano wakati wa Bunge tungeambiwa kuwa Karafuu au mafuta kutoka Zanzibar yametowa asilimia fulani katika Bajeti basi wengi wangetambua kuwa Zanzibar inaexist. Sio wengi na inataka uelewa kujua kuwa Zanzibar inahitaji kichache inachopata ili kjiendeleza.
Hili suala la kupata kichache kisichotosheleza hata kwa Zanzibar yenyew ndio ina youunganisha Jambo la Pili liliopo ndani ya Muungano wetu. Nchi duniani zimejaaliwa njia tofauti katika kujipatia mapato yake na kwa upande wa Zanzibar haikujaliwa njia sawa na mwenzake Tanganyika. Zanzibar haina maliasili wala ardhi ya kutosha kulima mazao ya Biashara na badala yake imekuwa sehemu ya Biashara hata hapo zama za Kale. Zanzibar ilihitaji kuwa huru katika kutafuta mbinu za kujipatia mapato lakini sijui kwa makusudi au kutoelewa Serikali ya Muungano imekuwa ikiibinya na kuinyima uhuru wa kiuchumi kwa kisingizio cha Sovereignity. Biashara ni kuwasiliana na watu na mataifa mbali mbali na inapofikia kuwa Zanzibar hawawezi kufanya hivyo kwa kisingizio cha Muungano ule mchango unaohitajika hauwezi kupatikana. Kwenye dunia yetu hii tumeshashuhudia baadhi ya watu wakiamuwa kubaki kwenye kutawaliwa kwa kuangalia maslahi. Kwa upande wa Muungano wetu nafikiri ndoto za Wazanzibari kutaka kujinasua ili wakatafute maendeleo zisingekuwepo kama kusingekuwa na kushindw kwa SErikali ya Muungano kuwahakikishia Wazanzibari maisha Bora. Itakuwaje kumzuiya mtu asitafute kipato kwa maisha yake nawe huna uwezo wa kumuhudumia. Tunataka kuona kuwa Zanzibar si nchi lakini tunasahau kuwa kuna Wananchi wanaotaka kuhudumiwa ndani ya hiyo tunayoiita sehemu ya Muungano, lakini hatuna nia wala uwezo wa kuwahudumia. Dawa ni kuwaacha wajitegemee wenyew na njia yao ni kuwasiliana na watu wengine kibiashara basi na waruhusiwe.
Tukirejea katika suala la utegemezi tutagunduwa kuwa utegemezi huo ni wakutengeneza na wala hauna haja ya kuwepo. Kwa nini Serikali ya Muungano ipoteze fedha nyingi kwa Zanzibar wakati mambo ya muungano ni machache na sehemu ya Zanzibar ni ndogo sana sana ndani ya Muungano . Mfano kwa nini wabunge kutoka Zanzibar wanakaa kwenyw vikao kwa mambo ya wizara zisizokuwa za Muungano na kupoteza mapesa bure? Kwa nini Serikali ya Muungano inaweka vikwazo vya kuundwa Taasisi zitazokuwa chini ya ufadhili wa SMZ kama Taasisi za elimu na nyenginezo. Kwa nini tunapoteza pesa kwa mambo ya vyama na visiwe kwa pande tofauti?
Si jambo la kubisha kuwa mwananchi wa kawaida hanufaiki na utegemezi uliotengenezwa kwani ni wachache wanaokula matunda ya Muungano. Sitoacha kutowa mifano ya namna Serikali ya Muungano huwa haifanyi jambo kwa Wazanzibari wakati wa shida.
Wale tunaopiga kelele na ufisadi basi hatuna budi kulizungumza hili la Muungano ili wananchi wa kawaida wanufaike na huu Muungano.
 
Ninyi watu... record unataka upewe film na ITV/TVZ/Chanel 10? Are you saying kuna mabadiliko ya katiba hayakwenda Dodoma na kupitishwa na bunge? Ama kweli... ninyi mnapenda chokochoko.

Achani choko choko... fanyeni kazi... tatizo la Zanzibar ni uchumi... sio kuitwa nchi huru!!!

Je baada ya Zanzibar kuwa nchi huru what will hapen... zaidi ya kuwa na matumizi zaidi ya kuwa na jeshi lenu zaidi, kufungua balozi nyingi etc.... kwa ajili ya kujilinda... na wengi zaidi... Kenya... Tangampya.. etc. etc....


Fanyeni kazi... achaeni politics

Umesikia wapi baba akashindwa na familia yake? Kwani Bush hayuko? kwani emirates, Japan na konoike yake hayupo? Mnachofanya nyie sasa na kuiendeleza Tangabyika basi Znzibar itafanya.
 
Ngekewa,

Usitafune mawe hapa! Kama Wazanzibari wameuchoka Muungano kwa nini wasijitoe? mbona mwanyoosha vidole ati?

Kama mmedhulumiwa na kudhalilishwa, kinaashinda nini kuamka sikumja na kusema Muungano sasa basi na kutoa talaka? kwa nini ubabaishaji wa maneno?

Wazanzibar wamekuwa wazi kila siku.1984 walitaka White paper nyerere akawafunga kina Seif, waza nzibari walitaka serikali tatu 1984 Jumbe akatolewa madarakani, Sa wanataka Muungano unaiitambuwa kuwa zanzibar ni nchi. Mwenzangu bado hujafahamu wanachotaka Waznzibari.Iwapo hamtaki kuwapa wanachotaka na ufumbuzi ni kuuvunja muungano basi na iwe hivyo. Nafikiri umepata wanachotaka.
 
Safi sana muungano ukifa. Jinsi mlivyo wavivu lazima mtakufa njaa tu!

Ngekewa,

Anatakiwa kutuambia kwamba kukiwa na serikali tatu! au kukiwa na Zanzibar kama nchi ni faida gani? ataipata mwananchi wa kawaida.

Hivi mnashindwa kujua hii ni agenda tu ya viongozi maana wanajua nafasi za kisiasa na kiouongozi zitakuwa bwerere?

Alafu unafahamu kwamba mkiachiwa huru mtachinjana... do you know this?
 
Ni kweli Gustanza, maana kwa excitement aliyokuwa nayo mheshimiwa Karume, alifanya mapinduzi Unguja tu, hakukumbuka kupeleka watu Pemba hadi alipohimizwa na Nyerere, kuwa asipofanya hivyo, angepinduliwa na watu walioji mobilize Pemba.

Pili, siwalaumu kwa kushindwa ku foresee matatizo ya namna hii ukizingatia hali ilivyokuwa wakati ule na level of understanding ilivyokuwa. Cha msingi ni kukubali kurekebisha matatizo yetu.

Mbalamwezi: Careful when you say karume did the coup. The coup, and eventual "Revolutionary Government" is still a controversy, the group that did the Revolution, is not the one ended up ruling. And this happened during the peak of the Cold War (do you see images of the Americans, Soviet, Cuba, China... and Zanzibar was in the middle of these giants...)...Forget what you know from our primary school history lessons, that's all cooked. And this to me, is perhaps the root of the fuss we have today. The people in Pemba know this for a fact, and they are wondering why they are being forced into a revolutionaty govt that is not the one.

Zanzibar was never to escape this situation, it was just a matter of "who is the better devil" for a bedfellow. Zanzibar is still searching for its footing. Zanzibar wants to be finally free. Remember, as a country, it only lasted for only two months before joining Tanganyika, and well, you know the rest. Trust me, this was the longest time it could stay independent, many other "interested groups" were already closing in.

And who knows the secret between Karume and Nyerere? Even most Zanzibaris do not know. I dont know, and I can bet many in the government=CCM don't know either. Sources say the two were "very close friends". Their friendship brought us the goods and the bads.

The continued hesitance to deal with "bads" has taken us to this rough terrain.

With the now blunt Cold War (it never ended) focused elsewhere, and Tanganyika no longer adhering to socialism=communism, I don't see why the powers that be are holding up Zanzibar.

Let the Isles Loose... I have repeatedly said that Tanganyika has enough problems to focus on, this background noise is just diverting attention on core business.
 
Kasheshe,Kichuguu,FairPlayer,Fundi Mchundo,Gustanza,...

..Muungano ni wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar.

..wa-Zanzibar wakiamua Muungano basi, Tanzania haipo tena. i think that reality hasnt sank in yet, especially to the Zanzibaris. bado wanafikiri wanahitaji Watanganyika kujiondoa kwenye Muungano.

..mimi nadhani kisichoeleweka ni mamlaka na madaraka ya serikali ya SMZ. lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba Tanganyika na Zanzibar ndiyo ziliounda Tanzania.

..nisichokubaliana nacho ni madai kwamba Muungano, au Tanganyika, unaidumaza Zanzibar kimaendeleo.

..Zanzibar ina serikali[raisi na baraza la mawaziri], baraza la wawakilishi,mahakama, revenue board, kmkm, etc etc, na mamlaka kamili ya kuendesha mambo, na kujipangia mipango yao, bila kuingiliwa ama kubugudhiwa na Muungano/Tanganyika.

..mimi nadhani tukae pamoja na kuangalia uwezekano wa kuuvunja huu Muungano kistaarabu. it is time to move on jamani.

..after all tunaelekea kwenye Muungano wa EAC na baadaye SADC. kama Rwanda na Burundi wanajiunga kama mataifa kamili sioni kwanini ZNZ wajiunge ktk kivuli cha Tanzania.

NB:

..katika mashindano ya soka ya Afrika Mashariki bendera ya ZNZ hupeperushwa, sioni kwanini tukija kwenye suala la Jumuiya wafichwe ndani ya Tanzania.
 
..nisichokubaliana nacho ni madai kwamba Muungano, au Tanganyika, unaidumaza Zanzibar kimaendeleo.

..Zanzibar ina serikali[raisi na baraza la mawaziri], baraza la wawakilishi,mahakama, revenue board, kmkm, etc etc, na mamlaka kamili ya kuendesha mambo, na kujipangia mipango yao, bila kuingiliwa ama kubugudhiwa na Muungano/Tanganyika.

Unaweza kusema- bila kuingiliwa au kubughudhiwa- Sijui kama ni hivyo. Lakini la kweli ni kuwa wanawakewa vipingimizi some times openly na most of the time technically, kutekjeleza hayo wanayoyapanga na kuyaamua kupitia vyombo vyao halali. Sasa hii ndiyo inayowakwamisha na wanayolalamikia zaidi, iliyobaki ni bla bla tu. Vikwazo na viregezwe ikiwezekana viondoshwe kwa manufaa ya wadau wa pande zote mbili.
 
Muda mfupi Seleli kamaliza yote,

Kwa ufupi amesema kuwa Zanzibar tukivunja muungano nao watajiingiza kwenye VITA na kuuwana wenyewe kwa wenyewe.

Au tuvunje serikali ya Zanzibar ibakie serikali moja tu!

Mi nakubaliana na hili la pili, TUWE NA SERIKALI YA MUUNGANO TU
 
Muda mfupi Seleli kamaliza yote,

Kwa ufupi amesema kuwa Zanzibar tukivunja muungano nao watajiingiza kwenye VITA na kuuwana wenyewe kwa wenyewe.

Au tuvunje serikali ya Zanzibar ibakie serikali moja tu!

Mi nakubaliana na hili la pili, TUWE NA SERIKALI YA MUUNGANO TU

..kwahiyo zanzibar iwe mkoa?. ngoja wakusikie!
 
Back
Top Bottom