Muungano wa Malawi na Tanzania: Pendekezo

Wakuu,

Naamini sote tunaendelea kufuatilia kwa makini mgogoro wa Mpaka kati ya nchi yetu na majirani zetu Malawi. Tumesikia mengi hadi sasa. Yapo yaliyo dhahiri, matharani, Malawi hawako tayari kwa namna yoyote ile kubadili mtazamo wao, nasi kwa upande wetu hatuko tayari kwa lolote lililo kinyume na msimamo tulionao kwamba mpaka wa ziwa Nyasa uko katikati ya ziwa tajwa.

Japo kwa sasa, pande zote mbili zinadai mazungumzo ya maelewano ndio dawa (sijasikia yanafanyika wapi), yawezekana kabisa mazungumzo hayo yasizae matunda. Wawakilishi wa Malawi watapata wapi ujasiri wa kurejea kwao na kutoa taarifa kwamba wameafiki, mpaka uko katikati ya ziwa? kadhalika wawakilishi wetu wataanzia wapi kutueleza kuwa wamekubali ziwa lote (isipokuwa ile sehemu ya Msumbiji) ni eneo la Malawi?
Matokeo ya kushindwa kuelewana yanaweza yakawa ni pamoja na kupelekana katika mahakama za kimataifa. Hata katika hilo bado kuna maswali, ni serikali gani itakuwa tayari kutoa taarifa kwa wananchi wake kwamba imeshindwa kesi mahakamani?

Kadhalika kushindwa kuelewana kutatupeleka katika lile ambalo wengi wamekwisha kulishabikia, ikiwa ni pamoja na viongozi wetu, yaani option ya vita. Hii ni option nzito na mbaya kabisa kwa mataifa mawili yenye uchumi duni. Yamkini Malawi au hata sisi, twaweza kusema tutashinda vita, lakini hilo haliondoi uwezekano kwamba matokeo yanaweza kuwa kinyume na matarajio. Aidha, japo upande wowote waweza shinda pambano la sasa, lakini ikawa ndio mwanzo wa vita itakayodumu vizazi na vizazi, hata ikawa kwamba mataifa haya mawili yatakuwa yametumbukia katika vilindi vya ufukara ambavyo kamwe hayatajinasua.
Katika mazingira haya, tunapaswa kufikiria option nyingine. Tutakapotafakari zaidi na kukumbuka kuwa si mmalawi wala si mtanzania aliyechora mstari huu unaotaka kutupeleka kubaya, tunaweza kusema; 'wait a minute', sisi ni ndugu, tena hilo halina ubishi, sisi sote tunaamini Afrika ni moja (rejea dhana ya panafricanism), kwa nini tusifute hiki kimstari cha mkoloni?

Tukikubaliana hilo, jambo baya la kugombea mpaka litatuzalia jambo zuri la kuingia sasa katika mazungumzo (no matter how long maungumzo hayo yatachukua) ya kuziunganisha jamhuri zetu mbili. Hatimaye tukawa na taifa moja; MUUNGANO WA MALAWI na TANZANIA.

Wawakilishi wetu kama mnanisoma tafadhali ...


Wazanzibari wanapigania kujitoa kwa uhuni wa muungano huu, alafu Malawi ijitie kwenye pori hili, never never never never never never never never never never never never never never!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Wazanzibari wanapigania kujitoa kwa uhuni wa muungano huu, alafu Malawi ijitie kwenye pori hili, never never never never never never never never never never never never never never!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkataba,
Kwa hiyo kwa mtazamo wako, ni nini iwe suluhu ya mgogoro uliopo? Aidha, naomba kutofautiana na wewe, muungano sio uhuni.
 
Mazungumzo yapo na hata kuna hiki kikao kitakachofanyika trh 20/08/2012 huko Malawi Kaskazini katika mji wa Mzuzu....Tuombe Mungu haya yaishe kwa mazungumzo na inawezekana kabisa kuisha bila hata kwenda mahakamani...
Mkuu Dickson,
Unauonaje sasa mwelekeo wa mazungumzo?
 
Mkuu Dickson,
Unauonaje sasa mwelekeo wa mazungumzo?
Mkuu George Kahangwa, kiukweli mazungumzo hayakwenda vizuri coz hakukuwa na maafikiano au maridhiano, hata hivyo bado yanaendelea so tuwe na subira na tuombe Mungu mambo yaende vizuri...Ila kama tutakubali kuwekewa viburi kwa maana ya Tanzania na Malawi basi mwisho wake hautakuwa mzuri..ndugu yangu George, kama ujuavyo, licha ya kuwa pale na resouces kama ardhi, maji na viumbe wake lakini vile vile panasadikika kuwa na mafuta mengi..Na haya yanatakwa na hayo mataifa makubwa so unawezakuta tunapewa viburi na hao wakubwa ili tusifikie muafaka na wao wapate nafasi ya kuyachota kirahisi...Leo nilikuwa naongea na mheshimiwa mmoja na akaniambia kuwa n vema hayo mazungumzo yakawa na msimamizi yaani atakayewapatanisha, so akashauri kuwa atafutwe mediator ambaye anakubalika na pande zote mbili ambaye atasaidia katika kufikia hitimisho...Hizi tambo za wanasiasa za kwenda mahamani ziwe ni za mwisho na si sasa....
 
Mleta mada umenkosha mtu wangu kidogo! Umeanza vizuri afu mwisho umekuja kutoa opinion ya jambo lisilowezekana kabisa, opinion ambayo ukipendekeza ndo kabisa haitakubaliwa, sasa mstari ufutwe ziwa litakua letu sote? Free movement itakuwepo, je kama kuna mafuta na gesi, mahela yataenda wapi? Tz au Ml? Ikiwa wanakataa tu share nusu ya ziwa watakubali tufute mstari kisha tutumie sote tu? Tusahau muungano na malawi
 
Mleta mada umenkosha mtu wangu kidogo! Umeanza vizuri afu mwisho umekuja kutoa opinion ya jambo lisilowezekana kabisa, opinion ambayo ukipendekeza ndo kabisa haitakubaliwa, sasa mstari ufutwe ziwa litakua letu sote? Free movement itakuwepo, je kama kuna mafuta na gesi, mahela yataenda wapi? Tz au Ml? Ikiwa wanakataa tu share nusu ya ziwa watakubali tufute mstari kisha tutumie sote tu? Tusahau muungano na malawi
Mkuu Chilubi,
Kwa maoni yako, je, kuna matumaini kwamba upo upande utakaokubali kuachia madai yake? Na kama suluhisho ni kufikia makubaliano ambayo yana manufaa kwa pande zote mbili, unaweza kupendekeza suluhisho hilo liwe la namna gani/liwe ni lipi? (Option niliyoitoa ni moja, pengine zipo nyingine zinazofaa zaidi au nyepesi kutekelezeka, tunapojadiliana, ni vema tukazitaja)
 
Back
Top Bottom