Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano.

Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

===========
June 2013:

Ewe Mtanzania, Sema "Hapana Serikali Tatu"; Sema "Ndiyo Serikali Moja!"

Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?

Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi....

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
 
huo ndo maana ya muungano..tatizo la wenzetu tumeshawapatia/wamejipa vielelezo vingi vya kujitambua kama taifa huru..ni kiasi cha wao kujitangaza kama nchi tu basi.. Hapo ndio ugumu wa kuwaambia tuunde serikali moja unapokuja kwani wameshaonja tamu ya madaraka mjj
 
Tuwaulize watanzania na wazanzibari kwa kura ya maoni wantaka muungano wa namna gani. Hakuna lisilojadilika wala lisiloweza kubadilika. Mimi ningependelea serikali moja. Pia sijui kwa nini tunadhani serikali tatu zitakuwa na gharama, sio lazima. Inategemea tutakavyogawa madaraka na ukubwa wa vyombo tutakavyoviweka. Jamani hii ni nafasi ya kumaliza hili suala. Tutaendelea na mijadala ya kero za muungano hadi lini. Tuwe wakweli na wawazi. Hata kuvunja huu muungano sio tusi kama kama lengo litakuwa kuanza upya na kuwa muungano wa maana zaidi. Au kuwa na nafasi nzuri ya muungano wa eneo kubwa zaidi ulio imara EAC
 
Kwanza Mzee Mwanakijiji Muungano wa serekali tatu ni wazo la kinafiki kwa wasioutaka huo muungano kwa dhati kwani si tu gharama zitaongezeka bali tutakaribissha mivutano isiyokwisha na serekali ya muungano itakuwa inaelea tu juu kwa juu...

I support you kuwa muungano wa kweli ni wa serekali moja....lazima kila mmoja akubbali kupoteza autonomy ndiyo sacrifice ya muungano vinginevyo ni kichekesho cha serekali mbili kitaendelea....moja ya wote na nyingine ya wachache....Umefika mda watanganyika tuamke sasa na tusimamie hili...ama serekali moja au kila mtu akusanye kilicho chake
....
 
Mkirua hata mimi nakuunga mkono, hapa hakuna cha serikali mbili wala tatu zitatuchanganya tuu, iwe serikali moja, kama haiwezekani basi Tanganyika ifufuke na Zanzibar waendelee na nchi yao
 
Serikali tatu mantiki yake ni nini hasa? Mgogoro utarudi tena juu ya nyadhifa katika serikali ya Muungano tena kwa kasi na muungano ndio unajifukia kaburini. Mi nadhani tuendelee na serikali mbili ila marekebisho makubwa katika mambo ya yautengenezao huu muungano.

Kuna kero, ila kumbukeni hakuna serikali ya Tanganyika. Iundwe kwanza ili kuivunja serikali ya muungano kwani kwa sasa muungano upande wa Tanganyika ilibidi kuua serikali ya Zanzibar na kua na serikali moja tu kama Nchi moja. Hii haiingii akilini kua kuna SMZ na Muungano, huu muungano ni wa chi zipi? Currently ni SMS Vz Jamhuri? Did jamhuri exist befor muungano? SMZ existed and it exits, now where is Tanganyika?

Kuwe na serikali MOJA tu ja MUUNGANO na si vinginevyo, au la Tanganyika kwanza.....
 
Kwa hilo Mwanakijiji nakuunga mkono...... Nisingependa kuona serikali tatu maana mbali na mzigo ni matatizo, migogoro na kero kila kukicha.... Hapo ni swala moja tuuu.. Muungano nchi moja (Tanzania) au kila mtu kivyake (Tanganyika & Zanzibar) full stop!!!!! no more... no less....
 
Serikali moja, Nchi moja, Taifa moja.
Na hakuna maana nyingine ya MUUNGANO ZAIDI YA HIYO! Vinginevyo ni UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI MTUPU! Mianya ya migogoro kati yetu chanzo chake kikubwa ni kuwepo kwa "Union Affairs against Non-Union Affairs" sasa tuifute kabisa hii aidha kwa kuwepo kwa serikali moja, ama kuvunja kabisa kamuungano kakinafiki tulichonacho, No More Options! Tatizo tunanakilishwa kila kitu na wazungu, tuwe na namna yetu katika kuchambua na kufanya maamuzi yetu binafsi.
Mungu wetu anaita!
 
tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (ccm na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie zanzibar watoke kwenye muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

Say no to serikali tatu!!

Iambie tume ya warioba - hatutaki serikali tatu!!

sioni mantikia ya hoja hii. Wabara karibu watapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Washaanza chadema vs ccm.zanzibar hali shwari tusitake kuwaingiza zanzibar matatizo
 
Naomba na sisi tusioutaka muungano tupewe nafasi.

Muungano ni ridhaa ya watu wahusika. Kama hiyo ridhaa haijawekwa hadharani kuwa tuliridhiana kuwe na Muungano basi ni batili.

Kama hali ndiyo hiyo ya wimbo wa waasisi wa muungano, ipo nafasi nzuri tu ya kuyarejea hayo maridhiano na kuyatakari kama yanafaa au hayafai. Mara nyingi it is better to start from the beginning when and where there was Tanganyika and Zanzibar.

Ni gharama nafuu sana kwa kila nchi kuwajibika na watu wake na rasilimali zake. Itatujengea kuheshimiana

SAY NO TO IMPOSED MUUNGANO AND DISMENTAL IT.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji hoja yako ni ya msingi sana lakini itakuwa ngumu sana kuietekeleza. nasema hivyo kwa sababu tumeshuhudia siku za karibuni watu wakiacha kazi za ujuzi na taaluma wakijiingiza kwenye siasa na hii yote si kwa sababu kwamba ni wazalendo sana bali walifanya hivyo kwa ajili ya matumbo yao (ni kazi inayoongoza kwa maslahi makubwa sasa nchini).

Tumeshuhudia pia kuongezwa kwa mikoa na wilaya ambayo na hii yote imekuwa ni kutaka kuongeza wigo wa nafasi za kisiasa bila kujali hali za wananchi. Kwa sababu nchi hii maamuzi yote yanafanywa na wanasiasa kwa manufaa yao (kama kujiongezea posho wao na kuwanyima madaktari) utekelezaji wa jambo hili utakuwa mgumu sana kwa sababu unagusa maslahi ya watoa maamuzi (wanasiasa) na hawatakubaliana na hilo bila kujali itikadi zao za vyama.......wao watapendelea mfumo wa huu uliopo sasa au serikali tatu au kuuvuja muungano kwa sababu nafasi zao hazitaathirika sana .............

Hivyo kuendelea na hoja ya serikali moja kutaka kuuvunja muungano haraka sana.............na kama kwa miujiza ikiwezekana basi tutapiga hatua sana....matumizi ya uendeshaji yatapungua......wanasiasa wengi kama wahadhiri, waganga wa jadi, madaktari, wasanii, wahandisi nk watarudi kwenye kazi zao za ujuzi na taaluma kwani nadhani nazo zitaanza kulipa pia kwani keki ya taifa nayo itaanza kugawiwa kwa usawa
 
Bara wananchi wengi wangependa kueendelea na muungano na hawa jamaa zetu, binafsi nilipenda serikali moja lakini kwa mambo yanavyokwenda haswa toka nimsikie Mama Karume...Tume ikifika nilipo ni mwendo wa kukataa muungano..

Lakini pia tusaidiane katika hili,...inapotokea kwenye kura ya maoni kwakuwa na wingi wa watu bara wakataka serikali moja lakini huko visiwani wasitake hata huo muungano Let alone serikali moja...hapo itakuwaje? Je yatachukuliwa maoni kiujumla wake au ndo kama ilivyokuwa '92 kuhusu vyama vingi...
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Hapo kwenye RED - Kuwakataza wananchi kujadili maslahi ya taifa lao ni KULAZIMISHANA na pia kung'ang'ania serikali tatu ni KULAZIMISHANA. Kwa nini kulazimishana huku? Kwa faida ya nani?

Kuna waliotoa rai ya kura ya maoni, matokeo yake yatakuwa kwa kasima gani - Tanzania Bara 50+1 na Zanzibar 50+1 iwe ndio uamuzi wa wengi juu ya kile watakachoamua au Tanzania yote wakiamua 50+1 iwe ndio imepita?

Kwa mtazamo wangu ni kuwa MUUNGANO UMESHAKUA KIROBA CHA MISUMARI, hakibebeki tena. Uamuzi wowote utakaoamuliwa sasa - iwe serikali 1,2,3...au kanda 7 au serikali 30 (yaani kila mkoa na serikali yake)...bado kero za Muungano zitazidi na hivyo kuzidi kutobebeka.

Kwa maoni yangu, suluhisho pekee la kutatua kero za Muungano ni kuvunja Muungano.
 
Kila mmoja ana mawazo yake kheri muungano uvunjike kuliko serekali moja na hilo halitokuwa maisha hata watanganyika wote wapige kura yakutaka serekali moja mtu anakuja eti z'bar inabebwa kwa lipi au kuwekwa makao makuu yote tanganyika ndio kubebwa na kupewa 4.5% katika pesa za muungano au kutopewa kabisa ndio kubebwa kama mmechoka kubeba kateni ubeleko
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

Mwanakijiji,

..mimi nataka serikali moja, serikali ya Tanganyika.

..pia nitapendelea serikali hiyo iwe ndogo and more efficient than hii tuliyonayo.

..zaidi sitaki kusikia suala la serikali za majimbo huku Tanganyika. wanaotaka serikali za majimbo ndiyo hao hao wanaotaka muungano wa serikali 3. Ukizingatia kwamba wanataka tuwe na majimbo 10 then tunaelekea kuwa na jumla ya SERIKALI KUMI NA TATU.
 
Back
Top Bottom