Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Serikali mbili ni mzigo sana kwa serikali ya Muungano kwa kuangalia yafuatayo:
-Kila Jimbo Zanzibar, pamoja na udogo wa majimbo haya, lina WABUNGE wawili. Mmoja ni wa Bunge la JMT na mwingine ni wa BLW;
-BLW lina wawakilishi watano ndani ya Bunge la JMT, Bunge la JMT halina uwakilishi kama huo kwenye BLW;
-Mabalozi wote wa Tanzania na gharama za balozi zote zinagharamiwa na serikali ya JMT;
-Vyombo vyote vya DOLA vinagharamiwa na serikali ya JMT;
-Mbunge kutoka Zanzibar anateuliwa kuongoza wizara yoyote ile ndani ya serikali ya JMT;
-Raia wa "NCHI" ya Zanzibar anaweza kuwa Rais wa JMT na sio kinyume chake;
Kwa kweli muundo serikali mbili umepitwa na wakati. Ni serikali moja au tuisaidie Zanzibar irudi ilikokuwa kabla ya MUUNGANO huu. Ndivyo wanavyotaka.
 
Kwa makusudi au kwa kutokujua, watanganyika tunajichanganya sana katika kudai serikali moja, nchi moja taifa moja.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(TanZan-ia) ni muungano wa baadhi ya mambo, mambo haya yanaitwa mambo ya muungano.
Muungano wa Tanzania si muungano kwa baadhi ya mambo, mambo haya yanaitwa mambo ya Tanganyika(Tz-bara) na mambo ya Zanzibar.
Mambo ya Tanganyika yamekasimiwa kwa Serikali ya Muungano ambayo pia inasimamia mambo ya muungano.
Mambo ya Zanzibar yanasimamiwa na kuendeshwa na serikali ya Zanzibar.

Mwalimu alitoa sababu ya kuwepo kwa serikali ya Zanzibar kama njia ya kuondoa hofu kwa wazanzibari na mataifa mengine kuwa Tanganyika haina nia ya kuimeza Zanzibar na kuanzisha ukoloni mpya.

Mwalimu anasema hivi:Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmoja wapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababuya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu(300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000).

Muungano wa Serikali Moja Ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tudhaniwe hata kwa makosa, kwamba tunaanzisha ubeberu mpya. uk 10-11
Link uongoziwetuna

Je umefika wakati wa kuimeza Zanzibar?
Je tumeshaamua kuanzisha ubeberu mpya(ukoloni)?

Mimi nafikiri Tanganyika ichukue madaraka yake kutoka serikali ya Muungano,iache kukasimu madaraka hayo. Baada ya hatua hiyo Tanganyika na Zanzibar ziende kwenye shirikisho la Afrika mashariki bila ya kuwa na uchafu wa kero za muungano.

Au tuige hii onecountrytwosystems huenda itasaidia Muungano kuendelea kuwa na uhai.
 
Wakuu,
Tanganyika haihitaji serikali 3. Serikali 3 ni wazo la ZNZ ili ile ya tatu isadie mambo yao.
Nimewahi kuuliza mara nyingi na sijibiwi, nauliza tena
1. Tanganyika inahitaji serikali 3 ili ifaidike na nini? Hiyo ya tatu itaisaidiaje Tanganyika.
2. ZNZ wanasema wanaonewa, je hiyo serikali ya tatu itaondoa nini katika uonevu
3. Je, serikali ya tatu itashughulikia mambo gani (yatajwe japo ili tuyachambue)

Kama hakuna jibu, basi jibu ni kupasua mashua tugawane mabao, I meana Tanganyika ichukue mbazo zake.
 
Serikali 3 ni mzigo kwa Tanganyika, Serikali 2 ni mzigo zaidi kwa Tanganyika, Serikali 1 ni mzigo na maradhi sugu kwa Tanganyika. LET ZANZIBAR GO!
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Katika hili mkuu wangu sikuungi mkono kabisa kwa sababu wewe huwajui Wazanzibar. Ndoa hii haiwezekani kufanywa kwa fikra za (samahani) Kikristu kwamba mume na mke wanapooana huwa wamoja. Hapa hakuna kitu hicho, ndoa yetu, mtu akiitaka talaka mpe muachane kwa kheri kabisa.. LETS ZNZ GO ndio solution ya kwanza, na ya pili ni Serikali tatu hakuna mzigo wowote kwa bara maana tayari tunao mgongoni tumeubeba miaka yote - hakuna litakalo ongezeka.

Serikali moja haitabadilisha lolote ktk haya yaliyopo leo ikiwa maswala makubwa ya Zanzibar ni Mamlaka kamili ya Dola ili wao kuamua mustakabali wa nchi yao kutokana na kero ama karaha kuhusu maamuzi ktk Wawekezaji, mikopo na misaada ya kiuchumi ndani ya nchi na mipaka yao.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa makusudi au kwa kutokujua, watanganyika tunajichanganya sana katika kudai serikali moja, nchi moja taifa moja.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(TanZan-ia) ni muungano wa baadhi ya mambo, mambo haya yanaitwa mambo ya muungano.
Muungano wa Tanzania si muungano kwa baadhi ya mambo, mambo haya yanaitwa mambo ya Tanganyika(Tz-bara) na mambo ya Zanzibar.
Mambo ya Tanganyika yamekasimiwa kwa Serikali ya Muungano ambayo pia inasimamia mambo ya muungano.
Mambo ya Zanzibar yanasimamiwa na kuendeshwa na serikali ya Zanzibar.

Mwalimu alitoa sababu ya kuwepo kwa serikali ya Zanzibar kama njia ya kuondoa hofu kwa wazanzibari na mataifa mengine kuwa Tanganyika haina nia ya kuimeza Zanzibar na kuanzisha ukoloni mpya.

Mwalimu anasema hivi:Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmoja wapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababuya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu(300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000).

Muungano wa Serikali Moja Ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tudhaniwe hata kwa makosa, kwamba tunaanzisha ubeberu mpya. uk 10-11
Link uongoziwetuna

Je umefika wakati wa kuimeza Zanzibar?
Je tumeshaamua kuanzisha ubeberu mpya(ukoloni)?

Mimi nafikiri Tanganyika ichukue madaraka yake kutoka serikali ya Muungano,iache kukasimu madaraka hayo. Baada ya hatua hiyo Tanganyika na Zanzibar ziende kwenye shirikisho la Afrika mashariki bila ya kuwa na uchafu wa kero za muungano.

Au tuige hii onecountrytwosystems huenda itasaidia Muungano kuendelea kuwa na uhai.

Nonda,

..kuhusu Tanganyika "kuimeza" Zanzibar Mwalimu alikuwa anazungumzia "perceptions" au "hofu" zilizokuwepo. Mwalimu alisema "Muungano wa serikali moja ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza Zanzibar." Zingatia maneno "ionekane kama."

..mimi nadhani kuwepo kwa nchi moja, dola moja, serikali moja, ilikuwa ni njia muafaka ya kuunganisha nchi zetu. sote ndani ya jamhuri hiyo mpya tungekuwa na haki sawa chini ya utaifa mpya wa Tanzania. Utaifa wa Zanzibar ulipaswa kufa kama ambavyo utaifa wa Tanganyika umekufa. Kinyume cha hapo nadhani ni ujanja-ujanja tu, au unafiki.

..wa-Zanzibar pia wamekuwa wakitamba kwamba dola ya Zanzibar ilipata kuwa kubwa na ikitawala mpaka maeneo ya Congo. Sasa kwanini leo hii hawataki kui-reclaim dola hiyo? Kwanini hawataki kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, na baadaye tukaendelea na muungano mpaka Congo and beyond, ili kuirejesha dola ya Zanzibar??

..Nilichojaribu kuonyesha hapa ni "matundu" katika hoja za wa-Zanzibar.

..Msimamo wangu mimi ni kwamba muungano uvunjwe. Kama kuna masuala tutapenda kushirikiana basi tufanye hivyo kupitia Jumuiya ya Afrika mashariki.
 
Nonda,

..wa-Zanzibar pia wamekuwa wakitamba kwamba dola ya Zanzibar ilipata kuwa kubwa na ikitawala mpaka maeneo ya Congo. Sasa kwanini leo hii hawataki kui-reclaim dola hiyo? Kwanini hawataki kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, na baadaye tukaendelea na muungano mpaka Congo and beyond, ili kuirejesha dola ya Zanzibar??
.

Hapo kwenye red: hayo madai ni kweli yapo. Lakini pia wanasema 'Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilikuwa dola kamili na walikuwa na kiti chao UN. Sasa ningetaka kuona ramani ya nchi inayoitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Na hiyo nchi iliyotambuliwa UN ilikuwa na ukubwa gani na mipaka yake ilikuwaje? Na pia ningetaka kujua walipopata uhuru ulikuwa ni uhuru wa maeeneo gani?
 
Katika hili mkuu wangu sikuungi mkono kabisa kwa sababu wewe huwajui Wazanzibar. Ndoa hii haiwezekani kufanywa kwa fikra za (samahani) Kikristu kwamba mume na mke wanapooana huwa wamoja. Hapa hakuna kitu hicho, ndoa yetu, mtu akiitaka talaka mpe muachane kwa kheri kabisa.. LETS ZNZ GO ndio solution ya kwanza, na ya pili ni Serikali tatu hakuna mzigo wowote kwa bara maana tayari tunao mgongoni tumeubeba miaka yote - hakuna litakalo ongezeka.

Serikali moja haitabadilisha lolote ktk haya yaliyopo leo ikiwa maswala makubwa ya Zanzibar ni Mamlaka kamili ya Dola ili wao kuamua mustakabali wa nchi yao kutokana na kero ama karaha kuhusu maamuzi ktk Wawekezaji, mikopo na misaada ya kiuchumi ndani ya nchi na mipaka yao.
Mkuu Mkandara, nakubaliana kabisa na wewe kuwa LET ZNZ GO ndiyo suluhu!

Nadhani hoja ya Mwanakijiji hapa ni kuwa kwa vile WZNZ wamegoma kuleta au wanaogopa kuleta hoja ya LET ZNZ GO! njia nyepesi ya kuwasaidia ni kuwa na serikali moja. Hii maana yake ni kuwa WZNZ hawatakubali na ikifika hapo LET ZNZ GO! itakuwa imetimia.

Ninapotofautiana na wewe ni uwepo wa serikali 3. Hakika Tanganyika hawahitaji serikali tatu kwasababu hakuna kitakachobadilika zaidi ya malalamiko.

Wznz ni wazuri sana wa kujenga hoja nyepesi na ni weupe wa kutetea hoja zao. Tukikubali kuwa tumebeba mzigo huu miaka dahari na hivyo tuendelee, watakuja na madai mengine yasiyo na mashiko. Sasa hivi kwa chini chini wanasema kuwepo na zamu ya madaraka wakimaanisha kuwa kiongozi atoke upande mmoja kwa wakati fulani hata kama ni kiazi au zezeta.

Juzi ndani ya BLW wamesema mafuta yaondolewe katika muungano, hawajasema pesa za bure za elimu ya juu ziondolewe. Wanasema meli zilizosajiliwa Iran ni haki ya ili wapate mapato wasichokisema ni kuwa ada ya meli hizo kule International Maritime Organization inalipwa na Sumatra.madai yao hayaishi na tukiyaendekeza wataomba tuwapelekea maji chooni!

Napinga serikali 3 kwasababu moja ya madai ya WZNZ ni kuwa na kiti UN, EAC, SADC n.k. Wanataka wawe na waziri wao wa mambo ya nje. Hadi sasa wana kila kitu, swali ni kuwa hiyo serikali ya muungano itashughulikia nini?
Kwa maneno machache serikali ya muungano ni ya kuwasaidia pale walipokwama. Hawana bajeti ya jeshi, na wasipotaka kulipa bili zao JMT italipa n.k.

Ukitaka kujua kuwa hawana hoja na serikali 3, waulize
1. Mambo gani yawe ya muungano
2. Serikali ya muungano iendeshweje
3. Nini mamlaka ya Rais wa JMT

Nakuhakikishia mkuu wangu, si Jussa, Maalimu Seif, Amour, Ally Salehe, Ahmed Rajab, Nonda,Abdulsahaf, Takashi, Baru baru ua Hamad Rashid mwenye jibu kwa uchache tu wa kuwataja. Kule Mzalendo.net wanajadili athari zitakazowakuta muungano ukivunjika, ukisoma hoja zao ni za kudanganyana tu maana hakuna hata mmoja mwenye proposal inayoeeleweka. Wote wanaimba nyimbo ya taifa la ZNZ, Serikali 3 au Mkataba, hawasemi vunja! wanatofautiana kwa hilo

BLW linamaliza kikao, Wabunge wa ZNZ Dodoma wanamaliza kikao, hakuna hata mmoja mwenye uthubutu wa kusema vunja muungano au kluleta hoija ya kuvunja muungano. Wote wanaongelea katika vijiwe vya kahawa vichochoroni.
Hii maana yake ni kuwa they are losers! and Tanganyika has nothing to loose, nothing! probably more to gain

LET THEM GO!
 
Nguruvi3,
Serikali tatu sio tena hoja ya Zanzibar wameshagundua utata wake kwao ndio maana wanataka muungano uvunjike na tuunde Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki kama EU. Kwetu sisi bara, serikali tatu itatusaidia sisi kuanza kujiandaa na utawala wa bara, nchi tulolipoteza zaidi ya miaka 40. Tutakuwa na katiba yetu wenyewe ambayo ndio sababu kubwa ya kulemaa kwa maendeleo bara. Katika katiba hii iliyopo tumeweka mambo mengi sana muhimu ktk katiba ya Muungano kwa kuchelea WaZanzibar watakavyo react kama tutayafanya kwa faida ya bara.

Hapatakuwa na mpango wa Uuwiano, sijui rais akitoka huku basi makamu lazima atoke huku, Uislaam mara Ukristu sijui uuwiano ktk Bunge na masharti mengineyo. Haya ni maswala madogo sana ktk utawala maana sijasikia wakerewe tukidai rais, waziri au naibu lazima awe Mkerewe. Marekani wana marais wangapi? kuna states hazijawahi kumtoa rais wala makamu wake na wanaendelea zaidi ya sehemu zilizotoa marais na makamu.

Serikali tatu itatuwezesha sisi kuanzisha madaraka mikoani kwa wepesi zaidi ili kila mkoa kutazama investments, kodi na matumizi yake, mchango wake ktk mfumo wa maendeleo ya Tanzania hautakuwa msingi wa maendeleo ya jimbo isipokuwa kuunganishwa na majimbo mengineyo kujenga Taifa moja. Na viongozi watawajibika zaidi kwa wananchi na majimbo yao maana hatutakuwa tena na serikali kuu na rais kuteuwa wakuu wa mikoa na wilaya bali wananchi wenyewe ktk majimbo yao. Hii itarahisisha zaidi ombi la Chadema badala ya kuigawa majimbo maana malengo ni yale yale. Elewa sababu kubwa ya kuwepo serikali kuu, madaraka makubwa kwa rais yote haya ni ktk habari hii ya kulinda Muungano wa nchi mbili zenye serikali mbili. Na pia Zanzibar wataona jinsi serikali za majimbo zinavyotakiwa kujitegemea na sii kulalamikia serikali kuu.

.Hatuwezi kupata katiba nzuri ikiwa bado tutaendelea kuwa na serikali mbili maana madai yote yatazidi kujitokeza hata kama tutabadilisha katiba mara 10 - Serikali mbili ndio Tatizo ndiyo inawafanya baadhi ya watu tu kuwa wenye mamlaka na haki ya kuongoza na lazima washike nyadhifa kubwa kubwa kuhakikisha Muungano hauvunjiki.

Matatizo ya Zanzibar leo yanahusiana zaidi na Baraza la Mapinduzi, watu wana uchu wa demokrasia ili viongozi watoke nje ya baraza hilo lakini kila wanapouliza wanaambiwa haya ni maswala ya Muungano wakati mengine sio, isipokuwa kulinda Mapinduzi kama Zimbabwe na ZANU au Sisi bara na CCM. Muungano huu unawalinda CCM na ASP na kama utavunjika basi vyama vyote hivi havitakuwa na nguvu.

Tukiunda Tanzania moja kuna hatari kubwa ya CCM na ASP kuwa madikteta wakubwa zaidi maana hakuna chama ambacho kinaweza kupata umaarufu bara na visiwani isipokuwa CCM, upinzani utakuwa kwa makundi miaka yote..Let's Zanzibar go ni option ya kwanza, na serikali tatu ni wazo la Watanganyika na Wazanzibara kwa faida yao mzigo huu lazima tuutue..
 
Hapo kwenye red: hayo madai ni kweli yapo. Lakini pia wanasema 'Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilikuwa dola kamili na walikuwa na kiti chao UN. Sasa ningetaka kuona ramani ya nchi inayoitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Na hiyo nchi iliyotambuliwa UN ilikuwa na ukubwa gani na mipaka yake ilikuwaje? Na pia ningetaka kujua walipopata uhuru ulikuwa ni uhuru wa maeeneo gani?

FJM,

..hata mimi nazitafuta documents zinazobainisha mipaka ya Tanganyika vs Zanzibar lakini sijafanikiwa kuzitia machoni.

..unajua wa-Zanzibari wanatabia ya kudanganyana sana. nilibishana kwa siku kama 4 hivi hapa JF na m-ZNZ aliyejazwa ujingwa kwamba Tanganyika haikuwahi kuwa na kiti chake UN. I am telling it was not an easy task to educate him.

..kwa kifupi ni kwamba Sultani hakuwa mtawala wa huku Tanganyika and beyond. He had what u would call spheres of influence ktk maeneo mbalimbali ya bara. Pia alikuwa na trade posts maeneo ya pwani ya Afrika mashariki.

..kama Sultani wa Zanzibar angekuwa na dola na mabavu yanayotambulika ulimwenguni basi bila shaka angealikwa kwenye mkutano wa Berlin na yeye akajikatia mapande ya ardhi ktk bara la Afrika.

..kuna kisa nimepata kusoma kwamba Usultani wa Zanzibar ulivyotenganishwa na ule wa Oman baada ya Waingereza kuingilia na kumpachika mtu wao Zanzibar. Walifanya hivyo kwa kumzuia mrithi halali aliyekuwa akitokea Oman asifike Zanzibar.

NB:

..wakati tunaungana ZNZ ilikuwa na watu 300,000. leo hii inasemekana D'Salaam peke yake ina wa-ZNZ 350,000. halafu kuna watu wanadai wa-ZNZ hawafaidiki chochote kile ktk muungano huu.
 
Acha hiyo unajua huyu Jamheed ndiye alitakiwa kuwa mrithi halali wa Usultan Oman kulingana na historia ya kule. Lakini Mjomba wake ndiye alochukua nchi baada ya vita kali ya kiukoo, mambabu zake wakakimbilia Mombasa na hadi kuhamia Zanzibar kwa safety yao. Sasa nashangaa sana anataka sana kurudi Zanzibar wakati Usultan na halali yake uko Oman ambako mababu zake ndio walikuwa watawala.. Kule kuna mafuta wala sii ya kupima na exploration, anaitakia nini Zanzibar ambayo haina kitu zaidi ya karafuu?..
 
Mkuu Mkandara
Well said Bro! Thanks

Nimecheka sana uliposema Wakerewe hawadai Rais au Makamu wake! Sisi kule Bonde tunakunywa madafu tu wala hatuhitaji katibu mkuu! Tukishakula ngogwe raha mustarehe! ha ha ha ha.

Tena ukiangalia kama Marekani, jimbo kama Montana utadhani halipo, lakini watu wanaishi vema tu.
Nadhani tuyachambue yale maoni ya baraza la katiba la Waislam maana ulichoongea kinajibu hoja. Na ni kule ndiko kuna vituko vya kupokezana uongozi.
 
kweli wewe umetoka kijijini yaani mfuko wa serikali tatu unasema ni kubeba zanzibar what about hiyo serikali moja umeangalia nayo inafanya nini? kama hujui ni kuimeza zanzibar kitu kitu ambacho hakitotokea kwani wenye inchi yao wameanza kuidai so kuuwa fitna kila mtu ale corner tu hii kujuana sana nayo inaleta umasikini
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

Mzee Mwanakijiji huyo wa kusema ametukataza tusidai uhuru wa tanganyika amepewa mamlaka na katiba ipi wakati siye ndiye tumempa ugali...................
 
Last edited by a moderator:
I beg to differ.

While one state one govt is the (seemingly) ideal solution (conceived in economic and proximity motives), but essentially both historically and objectively, Muungano cannot have any better structural shape legally and/or lawfully viability than first and fore mostly have Z'bar and Tanganyika reinstated as full and functioning sovereign states respectively.

Why one state one govt isn't an outright solution?

1) It will authenticate the theory of a "forced" rather than a "free" union outcry. Z'baris in particular has echoed such allegations and if they were to be told to forfeit their statehood that would be like handing a rope to a homicide.

2) Obviously we know that every union or partnership has its goods and bads. We need to critically identify, openly elaborate and analyze critically the collective benefits of a union. So far I feel it were mainly political and security(?) factors which has so blanket and drive this muungano.

3) There's a need also to consider, agree and declare stages and limitations of any such union. I'm unaware of existence of any lasting union which didn't categorically and clearly define those areas.

4) Towards a free union for a common cause, how much is expensive? I'm an avid skeptic when just the factuation of economic item could so decidedly swung the structure of the entire union. If we want the best then we should pay the best price and that's is too common a norm. Let's be honest at mere individual levels of how much and what distance did we trouble to pay to have our wives/husbands. Costs are lightweight if the quality and benefits guarantee the attainability of common goals. However, prudence wisdom should be fully applied in context.

But if the union is born out of contentiously schemes of force and cunning, unilateralism, inferiority complexes etc then whatever costs paid will be equated to extravagancy.

5) We simply cannot run away from our feelings even if we opt to ignore the existence and the force of the same. Any better union must win the souls and the minds of the collective citizenry. For it do symbolize the very souls of two countries wrapped in mutual interests.

Just for a start.
 
Wazanzibar hawatakubali kamwe serikali mmoja - hawataki kumezwa, wameshasema. Hivyo, suluhisho ni serikali 3.
Pili, hoja ya gharama ni suluhisho lake ni sera ya Chadema ya Majimbo. Kwamba serikali ya Muungani iwe na wirara zisizozidi 5 tu. Hivyo,ishu nyingine ziwe managed ktk local level. Gharama zitakuwa zimeshukua sana ukizingatia hata hizo serikali za mitaa tunaondoa nafasi ya DC na kubaki na kiongozi wa Kuchaguliwa tu, iwe kwa mujibu wa sera ya Chadema ya majimbo makubwa au la.
 
MMJ:
Mimi naona kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ni very unpractical tokana na matokeo mabaya ya kiuchumi UNDER CCM government. Ikiwa tutaungana, Tanganyika ambayo ni kubwa sana lkn ni maskini sana sana hivyo mwali Zanzibar watakua na kinyongo cha kumezwa ama kuolewa na maskini - ambapo wakideka Tanganyika hawafurahii. Practically hakuna NCHI ama MTU atakaye kuolewa na maskini, mzembe ama mhuni ama mtu ambaye hayupo serious kama CCM.
Tanganyika kubwa ingekua na uchumi mkubwa ni dhahiri Zanzibar dogo dogo wasingeona noma kupoteza Uzanzibar wao. Tukiungana itakua kama Tanganyika baya, kubwa na maskini inavizia mali za mrembo dogo dogo Zanzibar na hawatakubali kwa hilo. Naamini CCM kama kawaida yao watalazimisha Muungano, lkn uwezo wa kuuimarisha hawana.

Kama CCM wangekua vidume wa kweli wangeinua chati za uchumi kwanza ili kila mtu aone faida ya kuungana, kuungana ni pamoja na mnyonge kupata ufueni sio na kujiongezea mzigo.

Halafu just imagine serikali moja kubwa ya MUUNGANO under serikali fisadi ya CCM - juzi tu wamewafukuza drs wakati hatuna drs wa kutosha, hivyo usitegemee itaweza mudu kuongoza serikali ya Muungano yenye challenge nyingi na ngumu.
 
Kinachoonekana hapa ni kwamba mwanakijiji anacampaign na kuadvocate for compete colonization of zanzibar by tanganyika. Tanganyika can not forcefully impose muungano wanaoutaka wao kwa zanzibar. Huo ni ukoloni na wala Zanzibar haikumpindua Mkoloni na Sultani wa Kiarabu ili itawaliwe na Mkoloni Mweusi Mtanganyika. Kwa hilo sahauni, sio leo tena.
Jumaane,
Mimi naona kwa sasa hivi Zanzibar ndiyo inayo colonize Tanganyika kwa sababu yenyewe inajitawala na bado inashare kwenye Muungano. Unasema Tanganyika can't force Muungano wanaoutaka wao na Zanzibar, Je huoni kwa kusema hivyo unataka Zanzibar ndiyo i force Muungano wanaoutaka wao na Tanganyika? Marekani ni muunganiko wa nchi zaidi 40 ambazo zilikuwa na mchanganyiko wa nchi ndogo na kubwa. Maskini na Tajiri lakini wameunda serikali moja. Kwa nini Serikali moja iwe nongwa kwa Tanganyika na Zanzibar? Je nini mantiki ya Muungano kama bado kila muungana ana serikali yake?

Hoja ya Serikali tatu ni hoja ya wanasiasa kujitengenezea nafasi za ulaji.

Nakala: Mzee Mwanakijiji.

TUMBIRI (PhD, University of HULL, United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Na hii Tanganyika nayo ni kubwa sana ,hakuna serikali ambayo itaweza kutenda haki kwa Mikoa yote ,ili kupunguza mzigo kwa serikali ni bora ikagawanywa mapande manne.
 
Back
Top Bottom