Mimi nikokinyume na wadau wengi ambao wanashadadia serikali mbili kwa tatu. Mimi ninasema kama nchi ni moja basi hata serikali iwe moja tu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Rais awe mmoja na pasiwe na cheo cha makamu wa rais badala yake waziri mkuu atoke upande wa pili wa muungano ambao haukutoa rais. Rais atawale miaka 8 kwa mhula wa 4 by 2, kisha upande wa pili wa muungano ndio uwe na haki ya kutoa rais. Baraza la mawaziri liwe 2/3 kwa 1/3 Tanganyika wawe 2/3 na Zenji wawe 1/3 ya mawaziri wote. Bunge liwe moja tu la muungano. Mikoa iwe majimbo na Zenji iwe na majimbo pia. Jeshi liwe moja na pasiwe na mambo ya muungano na yasiyo ya muungano yote yawe ya muungano maana nchi ni moja yenye serikali moja. Ni mtazamo wangu japo unaweza kubezwa na watu kadhaa.
Umenisoma bila ya hivo, ukivunjika muungano Zanzibar tunajipanga miaka mitano then tunai Dar es salam, mtwara, tanga, bagamoyo, mombasa kuwa ni maeneo halali ya Zanzibar kabla ya kuja mjerumani Tanganyika, uaije ukashanga wa zenji watakapo kuja na full document
Mimi naafiki serikali moja na tena Raisi awe Kutoka ZANZIBAR MAwaziri wote watoke Zanzibar Mkuu waMajeshi atoke Zanzibar MaBalozi wote watoke Zanzibar Mkuu wa Usalama Atoke Zanzibar Mkuu Wa Polisi atoke Zanzibar Na Nyazifa zote KUbwa Kubwa zishikwe na Watu Kutoka Zanzibar hapo ndipo tutakapo endeleza Umoja wetu na Amani tupinge serikali TAtu ni kuvunja Umoja wetu na kuongeza Gharama za bure wananchi tusikubali kamwe kama kuna pesa za ziada Basi Zipelekwe ZAnzibar zikandeleze muundo mbinu.