Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,150
Muswada wa Sheria ya DNA wapitishwa
Thursday, April 23, 2009 11:53 AM
BUNGE la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imepitisha muswada wa sheria ya kusimamia matumizi ya Teknolojia ya DNA ya binadamu nchini
Muswada huo ulipitishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Makyusa Bungeni jana.
Mwakyusa alisema, sheria hiyo itatumika kutambua magonjwa ya urithi kabla na baada ya mtoto kuzaliwa, kuchukua tahadhari na kutengeneza tiba ya magonjwa hayo.
Alisema muswada huo ambao utatungwa kwa sheria itakayotumika katika tafiti na tiba, kinga na vilevile kuwalinda wananchi watakaoweza kuathirika na matokeo ya uchunguzi ya teknolojia hiyo.
Vilevile alisema sheria hiyo italinda katika kugundua makosa mbalimbali ya jinai na migogoro ya kijamii ambayo kwa sasa yanakwenda kinyume na sheria hizo.
Amesema matokeo ya uchunguzi wa DNA ya binadamu yatathibitisha uhalali wa mtoto kwa mzazi pia na Mahakamani, wapelelezi, wanasheria itawasaidia kutoa hukumu na hata kuwaachia huru watu aliohukumiwa kimakosa na kwa wale waliobambikiziwa kesi ambazo haziwahusu.
Muswada huo ulipitishwa baada ya kuungwa mkono na wabunge mbalimbali wakiwemo na wabunge watano wa upinzani.