Mume anatapika na kula maembe mabichi! Mkewe ni mjamzito wa miezi mi 3, hii imekaaje?

lakini, Nyamayao Mwenyezi mungu alishagawa majukumu toka anawaumba Adam na Eva. Adam atatafuta mali/chakula kwa shida na Eva atabeba mimba na kujifungua kwa uchungu!sasa hapo wanawake mnataka nini zaidi, hamuoni kuwa yote hayo ni mipango ya mungu na aliibariki iwe hivyo?!!!!!!

c ndio mana naishilia kutamani tu Bacha......
 
Bigirita bwana....haaa! hapana inatokeaga sana jaamni.

Haya mambo niliyasikia kwenye simulizi wakati fulani kwamba huwa yako kule kwa kina Mizengo ambapo Wataalamu wa Jadi huwa wanahamisha mimba kutoka kwa mtu mmoja na kuzihifadhi kwa mtu mwingine hadi nyakati za kujifungua zinapokaribia, na pia jamaa wa Ze Komedi waliekti wakati fulani hivi.
 
nilipokua mdogo, nilikuwa nasikia sana story hizi kuwa wanaume nao wakati mwingine zile shuruba za mimba huamia kwao, sasa leo naanza kuthibitisha, lakini mbona sipati connection hapa? Msaada tafadhali
 
duu hii chemistry imenishangaza sana, kuna nyingine niliwahi kuona mdada ana ujauzito na mzunguko wake wa mwezi anaupata kama kawaida, kipindi ananyonyesha mzunguko wake ndo ukasimama
 
hiyo kwangu kiboko khaa! mie nimeona ile mdada anaingia period kama kawaida mpaka mimba ilipofikisha miezi 5 ikakata, na amejifungua bila tatizo lolote, wakati kwa wengine ukiona period tu kama una ujauzito mara nyingi inaambatana na mimba kuharibika au ndio bed rest zanaanzia hapo.
 
Huu ndo uzuri wa JF, mauzoefu ya kumwaga yanapatikana!Thanks Nyamayao
 
duu hii chemistry imenishangaza sana, kuna nyingine niliwahi kuona mdada ana ujauzito na mzunguko wake wa mwezi anaupata kama kawaida, kipindi ananyonyesha mzunguko wake ndo ukasimama

Hapo juu mtaalam Pasco kasema sio kemistri hiyo...Ni muunganiko wa fiziks na bayoloji a.k.a PSI!:preggers::thinking::A S-confused1:

Nyamayao taratibu sio wote wengine wanajua jinsi gani ubebaji mimba ulivyo mgumu ni kweli kwa namna moja au nyingine linapokuja suala la kubeba mimba tungekuwa tunagawana majukumu basi mambo mengine yangekuwa yanaenda vizuri tu na mtu angeelewa adha ya kubeba mimba ilivyo kwahiyo ni utu wa mtu na kuthamini yule mtu aliyebeba kile kiumbe tumboni na kiumbe chenyewe pia
Kugawana majukumu kivipi?.....wewe miezi minne na nusu na mimi namalizia au wewe ulalamike unataka chips mayai saa tatu usiku mm nikimbie kama trolly kwenda kutafuta chips? dadavua basi!
 
una visa wewe...lol
 
Nilitaka nitafute kabinti.....ila sasa nimeghairi rasmi.....
Hii kitu ya kulishana maudongo hapana!
 
Nilitaka nitafute kabinti.....ila sasa nimeghairi rasmi.....
Hii kitu ta kulishana maudongo hapana!

nitakupa binti yangu....lol, kwani umeambiwa ni lazima itokee hiyo hali?...wacha uoga hebu panda mbegu huko.
 
hiyo kwangu kiboko khaa! mie nimeona ile mdada anaingia period kama kawaida mpaka mimba ilipofikisha miezi 5 ikakata, na amejifungua bila tatizo lolote, wakati kwa wengine ukiona period tu kama una ujauzito mara nyingi inaambatana na mimba kuharibika au ndio bed rest zanaanzia hapo.

Nyamayao naona ujuzi wako wa kutosha ngoja bibie akiishakamata kile kitu nitakuja kwako kwa ajili ya counsel.
 
nakukaribisha kaka.

Najua nitakuwa nahangahishwa mara ohoo nataka samaki wa maji baridi sitaki wa chumvi nataka mchele wa mbeya si huo wa morogoro nataka kuku wa kuchoma sitaki wa kukaanga ninahamu na mapera ukitoka kazini niletee mapera unaanza kupiga mahesabu mapera utayatoa wapi nataka juice sijui ya nini dah yaani kumbe mimba habebi mmoja mnabeba wawili maana hata huko kutumwa niletee hiki mara kile na wewe hapo umebeba pia on her behalf
 
nitakupa binti yangu....lol, kwani umeambiwa ni lazima itokee hiyo hali?...wacha uoga hebu panda mbegu huko.

Utanipa binti ambae tayari yupo au mimi na wewe tutatafuta binti?:smile-big:.....
ila bado hii bayo-fiziks haijaniingia kichwan...
 
Hii nzuri sana.Inaleta usawa.Na munug naye huwa anajua kufundisha watu kwa namna za ajabu sana.
Na inaonyesha huyu mwanaume ana upendo wa dhati kwa mwenzie.
 
Najua nitakuwa nahangahishwa mara ohoo nataka samaki wa maji baridi sitaki wa chumvi nataka mchele wa mbeya si huo wa morogoro nataka kuku wa kuchoma sitaki wa kukaanga ninahamu na mapera ukitoka kazini niletee mapera unaanza kupiga mahesabu mapera utayatoa wapi nataka juice sijui ya nini dah yaani kumbe mimba habebi mmoja mnabeba wawili maana hata huko kutumwa niletee hiki mara kile na wewe hapo umebeba pia on her behalf

haaa nimecheka cna mbavu, na tulio wengi ndio tunatumiaga huo wakati kudeka, mie nilikuwa nautumia ki kweli kweli, sana sana ya kwanza....utayapata tu hato mapera kwa juhudi zako...lol
 
Back
Top Bottom