Muhtasari wa elimu ya Maombi, Dua na Sala kwa Mtu Binafsi, na Familia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
MAOMBI, DUA NA SALA KWA MTU BINAFSI, AU FAMILIA

Anaandika, Robert Heriel.

Andiko hili lafaa kwa mtu yeyote, lafaa kwa rika zote, hadhi, elimu na hali. Andiko hili ni sehemu tuu ya kumbukumbu kwa wajuao mambo haya, aidha andiko hili ni elimu ya manufaa kwa wageni wa mambo haya. Haya basi, nisiwapotezee muda.

Hatukuwepo, tulitoka katika kutokuwepo, nasi tutarudi katika kusikokuwepo, hatukuwepo kwa sababu tumetoka kwake asiyekuwepo katika uwepo wa waliowepo katika ulimwengu huu, kutokuwepo katika macho ya nyama, nasi sasa tupo kwa sababu ya uwepo wa aliyepo kabla yetu ambaye kamwe hatokuwepo kwa macho ya nyama.

Basi nisiandike mengi, kwa maana kusoma kwingi huchosha mwili,

Kila mwanadamu anaasili yake rohoni, kila mwanadamu ananjia yake katika mfumo usioonekana, kila mwanadamu ananyota yake naam ndizo nyota za angani, kila nyota ni ufalme, kila mwanadamu ni ufalme unaojitegemea, mwanadamu lazima apate connection ya ufalme wake ili aweze kufanikiwa kwa kila anachokihitaji katika mapito yake hapa duniani. Mwanadamu akishaipata connection yake hujikuta akiitawala njia yake hapa duniani, huweza kutawala mambo madogo madogo yanayokuja mbele yake. Lakini jambo la kusikitisha ni kuwa zipo tawala ambazo hupenda kutawala tawala zingine, kuziteka nyara, kuzifanya watumwa na kuwa vibaraka.

NAMNA MBILI ZA KUTAWALIWA NA FALME ZINGINE;
1. Kutoa Utawala wako kwa hiyari
2. Kunyang'anywa utawala kimabavu (Hii hutokea mara chache sana)

Maisha ya binadamu yapo mikononi mwake mwenyewe, wewe ndio unaamua kwa sehemu kubwa utawaliwe au utawale, nadra sana mfumo wa dunia na Anga kuruhusu Upinduliwe katika utawala wako. Tawala za kiroho mara zote hutumia kanuni ya DHAMIRI YA HIYARI, hutumia Demokrasia na kuzingatia uhuru wa kiumbe mwenyewe, na hapa nazungumzia viumbe wenye utashi kama binadamu.
Bado sijaeleweka.

Jinsi unavyojiona hapo ulipo jua kabisa wewe ni mfalme/malkia katika nyota fulani usiyoijua, sasa jiulize; unatawala vyema vizuri au umekabidhi ufalme/umalkia kwa viumbe wengine iwe ni binadamu au viumbe wengine wenye utashi?

Kila mwanadamu anaakili yake, anaimani yake, ananamna yake inayomtofautisha na watu wengine, huo utofauti ndio huutambulisha ufalme wako, ikiwa utapuuza na kudharau asili yako ya ndani kabisa, ni wazi kuwa umekabidhi utawala wako kwa ufalme mwingine, kitendo cha kutamani kuwa mtu au kiumbe mwingine ni kukabidhi utawala wako kwa kiumbe hiko. Hiyo ni kanuni ya kwanza, katika masuala ya dua, maombi na sala "I am, and I am not like anyone else, neither is there any who is like me, and there will be no one like me. " Hiyo ni law namba moja kwenye sala, dua na maombi. Usijifananishe na chochote, yeyote, hakuna kama wewe, na hatakuwepo kama wewe. Endapo utaanza kujilinganisha, na kujifananisha ndio siku hiyohiyo unakuwa umeusalimisha ufalme wako kwa huyo unayejifananisha naye. Sijui kama naeleweka!

Kuwa wewe! Sasa ni lazima ujijue wewe ni nani, lazima ujiulize wewe ni nani, nafsi ya nje iiulize nafsi ya ndani wewe ni nani? Mara nyingi wewe OG umejificha ndani kabisa "Psycho-analysis" ndani ya "ung'amuzi bwete"

Mtu anayejielewe kamwe huwezi mkuta akijifananisha ni mtu mwengine, mara nyingi watu wanaojitambua huonekana wabaguzi, wajivuni, wanaojiona bora, wenye dharau. Watu wanaojitambua huwa na sheria zinazowatamabulisha wao kama watu bora na watawala wa jamii zingine.
Ngoja nilisema nisiandike mambo mengi;

Dua, sala, na maombi ni mawasiliano kati ya nafsi yako ya nje, na nafsi yako ya ndani kabisa. Watu wengi wanafikiri wakiomba dua, au sala au maombi hudhani wanamuomba Mungu jamabo ambalo sio kweli, Mungu haombwi na hajawahi kuombwa, isipokuwa ni mtu anajiomba mwenyewe, nafsi ya nje inaiomba nafsi ya ndani impe mahitaji yake ya msingi. Bado sijaeleweka.

Mungu sio kiumbe, hana masikio, hana macho, hana sifa zozote za kiumbe, ingawaje wapo viumbe wenye sifa za kiungu, ambao wengi huitwa miungu na inaabudiwa mpaka hivi leo. Hata wewe unaweza kuja baadaye kuwa mungu mdogo unayeabudiwa endapo utafanya baadhi ya mambo hapa duniani. Mungu aliweka tangu zamani na zamani, milele na milele haya tuyaonayo na tusiyoyaona kama yalivyo yakiwa yamekamilika, huna haja ya kumuomba kwa maana hawezi kukusikia wala hakuoni tena, uliyoyakosa mwilini basi yapo rohoni, ni kufanya connection tuu ili uweze kuyatoa katika nafsi ya ndani na kuyaleta nje.

Watu waelewe kuwa, kuna matamanio na mambo ambayo nafsi huyapenda, jambo lolote ukilitaka alafu ukalipata lisikufurahishe ujue jambo hilo ulilitamani tuu, furaha iliyotimilika hutoka ndani kabisa ya nafsi ya ndani.

Dua na maombi ni muhimu sana na ni jambo nyeti, la siri sana ikiwa litagusa mambo yako ya baadaye, hakuna Dua au maombi ya utawala yanayofanyika hadharani, hakuna kitu kama hicho.
Maombi na Dua ni kikao chako cha siri baina ya nafsi yako ya nje, na nafsi ya ndani, sio ajabu inashauriwa maombi yafanywe sirini tena ufumbe macho ili connection ya nafsi ya nje na ndani ziwe active.

Nilisema sitasema mengi!

Hakuna duniani ambaye anaweza kukuombea au kukupigia dua ukapona, au ukapata mahitaji yako, isipokuwa Imani yako(Nafsi yako ya ndani) ndani ndio inakusaidia.

Katika Dua na Maombi kuna mambo yafuatayo;
1. Nia
2. Nyakati
3. Mikao
4. Mazingira
5. Hali ya mwili.
6. Malighafi

1. NIA

Unania ya kupata kitu au jambo fulani, ni lazima uwe na nia kabla ya kufanya maombi ya kutaka kitu fulani. Labda unahitaji Kuolewa au kuoa, basi lazima uwe na Nia thabiti katika jambo hilo. Nia lazima iwe na sababu, na hizo sababu lazima ziwe hazihusishi kujitukuza kwa wengine au kuwaonea wengine bali zihusu kulinda heshima na utu wako, na ufalme wako.

2. NYAKATI
Baada ya kuwa na Nia, jambo la pili ni sharti ujue yafuatayo;
i/ Nyakati za Nia hiyo kutimia,
Ni upi wakati sahihi wa wewe kuolewa au kuoa. Kila jambo linawakati wake, ila lazima utofautishe wake wako na nyakati za watu wengine, kama vile kuna wengine wanawahi kubalehe, kupevuka na wengine huchelewa lazima uzingatie hilo. Au wengine huwahi kuzeeka na wengine huchelewa licha ya kuwa na umri sawa basi lazima ujue nyakati zako sahihi katika Nia fulani.

ii/ Nyakati za Dua na maombi katika Kila Nia
Maombi na Dua huzingatia zaidi nyakati, masaa, mchana, jioni, asubuhi, usiku wa manane, wakati wa mwandamo wa mwezi, wakati wa giza aambapo usiku hauna mwezi, wakati wa kiangazi, baridi, masika au vuli n.k.
Yapo maombi na Dua hupaswa kuombwa usiku wa manane, mengine hupaswa kuombwa kwenye msimu wa mwezi kuandama tuu, mengine alfajiri na mapema, n.k

Huwezi kuchuma Matunda kwenye mti msimu ambao miti haina matunda, labda uchume majani.

3. MIKAO
Baada ya kujua nyakati za dua na maombi kinachofuata ni kujua utatumia mikao gani. Kwenye Dua kuna mikao ifuatayo
A. Kupiga magoti
i/ Ukiwa umekunja mikono miwili ngumu ikiwa kifuani
ii/ Ukiwa umeachia viganja vya mikono yako kwa kuvikutanisha kama unapiga makofi, ikiwa kifuani.

B. Kupiga magoti na kuweka paji la uso Ardhini "Kusujudu"
c. Kusimama
i. Ukiwa umekunja mikono ngumi na kuiweka kifuani
ii/ Ukiwa umeachia viganja vya mikono yako kwa kuvikutanisha kama unapiga makofi, ikiwa kifuani
iii/ Ukiwa umeiinua mikono juu kama unajisalimisha
iv/ Ukiwa umeupeleka mkono wa kuume mbele kama unabariki au kuweka kitu wakfu

D. Kulala Kifudifudi (Kulalia tumbo)

E. Ukiwa umelalia ubavu (inaweza kuwa wa mkono wa kulia au wakushoto)
F. Kuikunja miguu ipishane kisha uikalie,

G. Kukaa kawaida (iwe chini au kwenye kiti au kitu chochote)
H. Kuchanganya mikao katika dua au sala moja, mfano, kusujudu, kusimama, kukaa, na kulala kwa wakati mmoja kwa kufuata utaratibu maalumu

Kila Dua huweza kuwa na Mkao wake kutokana na Nia inayoombwa na mhusika. Jambo moja la kuzingatia ni kuwa kadiri mkao utakavyomchosha mtu kwa haraka utachukuliwa ndio mkao bora zaidi ya ule uliomwepesi na usiochosha kwa haraka, mfano, mkao wa kupiga magoti na kuweka mikono juu, huu huchosha magoti na makwapa kuuma, huu utachukuliwa kuwa bora kuliko mingine, au kuweka paji la uso kwenye ardhi au sakafu. Pia Mkao unaoonyesha Unyenyekevu zaidi kuliko mkao mwingine utahesabika mkao bora kuliko ule ambao ni wakawaida.

Ikiwa jambo linaloombwa ni kubwa basi mkao pia unapaswa uwe mgumu kuliko kuchagua mkao rahisi. Jambo moja la uhakika ni kuwa ipo connection muhimu kati ya nafsi ya nje inavyotaabika na nafsi ya ndani, ndio maana mkao migumu itakayoumiza mwili ni muhimu kuunganisha na nafsi ya ndani kabisa, sio ajabu watu hutakiwa kufunga kula na kunywa na kuzitesa nafsi zao, hii ni moja ya sababu.

4. MAZINGIRA
Mazingira lazima yazingatiwe, chumba cha dua au maombi lazima kiwe kimetayarishwa kikamilifu kwa ajili ya maombi, haitarajiwi uchafu na mazingira yasiyo rafiki katika kufanya connection ya mwili wako na nafsi ya ndani. Pasiwepo na mwanga mkali, kama utashindwa, kuukadiiria basi utawasha mishumaa kadiri ya utakavyoona kuukadiria mwanga usiwe mkali sana, mazingira yawe na harufu inayoamsha hisia za ndani kabisa, sakafu iwe safi, kwenye kuta uweke vifaa au zana zinazoendana na asili yako, kama ni muafrika basi uweke vitu vya asili ya kiafrika kama upembe wa ng'ombe kama umetoka jamii za kifugaji, kama umetoka jamii za wakulima, basi utaweka miti na mazao, au jani linalotambulisha mahali utakapo, kama umetoka jamii za wavuvi, basi utaweka mabaki ya moja ya viumbe wa majini wanaopatikana kwenu, vitu kama mabaki ya kasa, jamii za konokono n.k. Kama umetokea jamii za migodi, utaweka sehemu ya madini yanayopatikana kwenu kama ni kipande cha dhahabu, au almasi au kitu chochote, weka kitu ambacho kinaitambulisha jamii yenu kwa ubora kabisa, mfano kama jamii yenu inasifika kwa kupiga ngoma au kucheza ngoma, basi weka ngoma ukutani

Kama kuna mzee shujaa aliyewahi kutokea katika ukoo wenu au jamii yenu, weka picha yake katika ukuta.
Epuka chumba cha maombi au dua kuwa na mambao yasiyo na asili yako wewe, kuanzia jina lako mwenyewe, tafuta jina la kikwenu hata kama unatumia jina ulilopewa na wazazi wako, ukifika kwenye maombi tumia jina lenye asili ya kwenu, mfano mimi naitwa Robert Heriel, nitapaswa kutumia jina la kikwetu na kama sina basi nitajiita "Mimi Heriel, nipo mbele yako Mungu wangu, nipo hapa kuutukuza utukufu wako uliompa mtumishi wako, yeye na uzao wake"
Kamwe usiweke picha za wazungu, au wayahudi au waarabu au watu wa jamii ambayo sio yako.

Kama utaweza, omba kwa lugha yako ya asili, kama Kinyakyusa kwa waliowanyakyusa, au Kisukuma kwa waliowasukuma, kama hujui basi utatumia lugha unayoimudu, hapa ndipo ile dhana kuwa ni lazima mtoto umfundishe lugha ya kwenu, kwa maana kuna ishu zinakuwaga complicated ambazo zitahitadi asili itawale.

5. HALI YA MWILI
Je mwili umechoka, unanjaa, unausingizi, au unahamu ya tendo la ndoa, je umeboeka. Hayo ni mambo ya kuzingatia.
Je mwili wako ni mchafu, unanuka makwapa, unanuka mdomo kwa sababu haujasafisha kinywa?
Je Upo kwenye siku zako, au mkeo yupo kwenye siku zake? Au mtoto wako yupo kwenye siku zake?
Lazima uyazingatie hayo, yapo maombi na dua yanabagua hali za mwili wa mtu.

Mwanamke hapaswi kushirikishwa kwenye Dua na maombi ya mambo makubwa akiwa kwenye siku zake,
Je mwanamke anamimba, ikiwa ndio lazima Dua au maombi akiomba lazima aombe kwa nafsi mbili, kama anaenda kulala asiombe; nilinde nikienda kulala" au yeye mume asiombe; Mimi na mke wangu tunaenda kulala" bali aombe; Utulinde mimi(taja jina lako) na kiumbe kilichopo tumboni. Utukinde na mabaya na hila zote zenye kuleta maumivu na hasara"

6. MALIGHAFI
Kuna baadhi ya Maombi na Dua huhitaji malighafi fulani za kusindikiza na maombi, kama vile udi na uvumba, maji, moto, mafuta, mchanga, chumvi, au aina fulani ya mavazi ambayo mtu hupaswa kuvaa.

Malighafi muhimu ni Maji aidha ya mvua, baharini, au mtoni, ardhi hasa maeneo uliyozaliwa na mahali unapokaa au unapofanyia biashara, au shambani kama wewe ni mkulima, moto ni muhimu kwa wale wasioweza kuituliza akili sehemu moja, hao watawasha moto iwe kwenye mshumaa au popote kisha watakuwa wakiomba dua wakiutazama huo moto, hii husaidia kwa watu ambao wakiwa wanaomba akili hujikuta ikifikiri jambo au mambo mengine.

Mambo haya mtu yeyote huweza kuyafanya akiwa pekeake kwa kadiri atakavyoona, wala hauna haja ya kwenda kwa mganga, au nambii au kuhani, ila unaweza ukafanya mwenyewe na kile unachotaka kuwa kikawa.

Naomba niishie hapa,

Ni yule Mtibeli,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kuna mambo makubwa unayazungumzia hapa napenda ile intellectual freedom yako, ila kuna maswali yataibuka kwa sababu ya contradictions zilizopo, ni nyingi tu ila chache sana hizi:

Kwa haya uliyoandika unakiri kwamba hakuna Mungu mmoja, kila mtu ni mungu.

Unaonesha hapa au katika andiko jingine kwamba yupo Mungu mkuu na miungu chini yake. Huyo Mungu mkuu hana hisia zozote wala hafanyi communications zozote na viumbe ila kuna miungu chini yake nayo hutii maagizo yake.

Malighafi wakati wa kuomba za nini? Hili hufanya mfumo wako wa imani na maombi kuwa wa level ya chini kama voodoo, santeria, animism, tunguri, nk.

We don’t come from nothing and return to nothing, but from life and return to life. Machache kwa sasa.
 
Back
Top Bottom