Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,904
WABONGO NI WATU WA KUKUOMBEA MABAYA. DUA ZAO MBAYA NDIO MAFANIKIO YAKO.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kama huombewi mabaya jua bado unasafari ndefu ya kufanikiwa. Yaani bado haujakutana na Bless za Mungu. Baraka za Mungu zinaendana na Lawama, chuki, hasidi, wivu mbaya kwa wanaokutazama.
Ukishaanza kupata uelekeo mzuri wa maisha au jambo lolote ndipo utakapoanza kuona rangi halisi ya watu.
Watu hawapendi uwe na maisha Mazuri.
Watu hawapendi ufanikiwe kiuchumi, sijui umejenga nyumba nzuri, gari kali, miradi. Hawataki.
Watu hawapendi kuona jina lako linakua kubwa (unakuwa maarufu na mashuhuri).
Watu hawapendi unapokuwa na familia yenye furaha.
Watu hawapendi watoto wako wawe na mafanikio.
Hawapendi kwa sababu roho ya shetani huwavaa na wanapambana na baraka za Mungu alizokushushia.
Watakuzushia maneno hata ya uongo ilimradi ili wajifurahishe, na chuki yao ipoe. Unachotakiwa kufanya ni kuwapuuza. Kutokuwajibu chochote ndio dawa ya mashetani yenye chuki na Wivu wa kijinga. Hiyo itazidisha maumivu makali.
Elewa Watu wanakuombea kila siku ufe au ushindwe maisha ili nafsi zao zisheherekee
Mfano wakisikia ndoa yako au mahusiano yako yanatatizika utawaona wakisherehekea na maneno kibao ya kujifurahisha.
Mfano, Wapo Mastar kibao ambao zikitokea changamoto katika ndoa zao, Watu huweza kuzusha uongo mara kachapiwa, ooh! Alikuwa anàringa sana. Oooh! Tulijua. Watu hao wote nafsi zao ni za kishetani na wanafanana katika nafsi zao za giza.
Kama utagundua, kwenye siasa za nchi hii. Litokee tatizo dogo utasikia mtumbue huyo. Mtumbue huyo! Anajiona sana. Anaharibu sana. Ukitumbuliwa Watu wengi wenye roho za chuki watafurahia sana. Utadhani uliwahi kuwafanyia jambo baya lakini wala sivyo. Ni Ushetani na uchawi waliorithi kutoka kwa Wazazi wao.
Kwa upande wa ndugu, ukiwa unafanikiwa wengi wao huchukia. Hawapendi. Wapo watakaonyesha chuki zao waziwazi na wapo watakaozionyesha nyuma ya mgongo wako.
Uwasaidie shida. Usiwasaidie shida. Hawana jema. Wao ili wakufurahie wasikie habari mbaya kwako.
Wengine wanakuombea Dua mbaya.
Ukisikia mtu anakuambia Dunia inazunguka, au kabla hujafa haujaumbika, au aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi. Hizo ni kauli za Wachawi, mashetani, wenye husda.
Au ukisikia mtu akikuambia, Ipo siku yako. Ujue anaiombea siku mbaya ya mkosi ikupate ili naye afurahie anguko lako.
Taikon Master ninakushauri, kamwe usipende kupendwa na watu. Yaani ati unafanya mambo ili ati Watu wakupende. Huo ni utumwa. Kwa nini Watu wakufanye mtumwa. Fanya mambo upendwe na huyo anayekupa pumzi ambazo ndizo unatafutia riziki zako. Tenda HAKI, Fanya kwa Upendo, Kuwa na Maarifa, penda UKWELI.
Watibeli hatufanyi vitu kuwafurahisha Watu. Tunafanya mambo tunayoyaona ni sahihi, haki, kweli, upendo na akili.
Mtu akichukia achukie, kwetu haina maana yoyote. Mtu akitupenda atupende pia haina maana yoyote kwetu.
Ila sisi siku zote tunatoa Haki, upendo, kweli na maarifa kwa Watu wote hasa wale waliotayari na wenye uhitaji.
Ndugu yangu, ishi maisha yako kwa Haki. Na haki haipo kwaajili ya kumpendeza mtu bali kumpendeza yule anayekupa pumzi
Kwa sababu mtu unaweza mpenda au ukampa haki zake lakini bado akaona umemfanyia jambo baya.
Chuki zao ni sumu kwao wenyewe. Wewe hazina maana yoyote. Labda uamue kuzipa umuhimu.
Dua zao mbaya maneno yao mabaya, ni dua la kuku tuu kwa mwewe. Hakuna wa kuyatekeleza. Ni Watu waliofeli, walioshindwa. Ni mashetani ambao siku zote ni wachini tuu anayeangalia waliojiunga yake akitaka wadondoke.
Acha Nipumzike sasa.
Sabato Njema
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam