Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM


"You have to learn the rules of the game. And then you have to play better than anyone else." Albert Einsten
 
Bakwata na Mufti inabidi watambue kuwa asilimia 85 ya wapiga kura hawajui "Mahakama ya Kadhi" ni nini na kazi yake nini na kwa maana hiyo, assuming kwamba kauli ya Mufti itakubalika na kutekelezwa come 2010 CCM itashinda kwa asilimia 85.

Naomba nisisitize, kuna tofauti kati ya wapiga kura na watakaojindikisha kupiga kura!
 
Subirini mwezi mtukufu wa Ramadhani unakuja utawaona hao Bakwata wanavyopigana vikumbo kwenye ftari za Ikulu.

Mufti anajitutumua tu aonekane nae yupo kwani nani asie jua Bakwata na serikali dugu moja
 
Imetosha kuwa ujumbe umewasilishwa au umefika sasa kama wataenda ikulu au uwanja waTaifa hayo ni maslahi binafsi ,kama ni kuruka nae mufti ameruka kwa kuwakabidhi waislamu uhuru wao wa kuchagua badala ya kuing'ang'ania CCM iliyojaa uwongo kwa kuthibitika kuwepo kwa ahadi hewa lukuki.
 
Ivi jamani ilani ilisemaje? swala litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi sasa ufumbuzi ndo huo hamuutaki inakuwaje hapo? Siasa bwana shida kwelikweli!!
 
Eee sawa mkuu mliangalia uwezekano sasa mme wezekana!

Uroho wenu wa kura mnarukia vitu ambavyo vinaivunja katiba! eti iingizwe kwenye katiba, lakini waislamu tu ndo watoe maoni? na waislamu tu ndo wawe mahakimu? Kwahiyo itabidi serikali isomeshe mahakimu wa kiislamu kwa ajili ya kuhudumia mahakama hizo? yaani yaaani...

Mkuu hujanielewa kwenye post yangu, rudia kuisoma tena.
 
..Kikwete alishachomoa kuhusu ahadi ya Mahakama ya Kadhi.

..alidai waliotumbukiza suala hilo kwenye ilani ni Philip Mangula[mkristo] na Ngombale Mwiru[hana dini].

sina tatizo na mahakama ya kadhi. ila waislam watafute pesa zao wenyewe za kuendesha hizo mahakama sio kodi za akina john. kama mahakama ya kadhi ni ibada, basi msitumie kodi za akina john kuiendesha hiyo ibada.
 
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu. Mzee Mwanakijiji kuhusu alleged grand corruption cases ni still allegation hakuna substance wala proof katika hilo bali ni accusations tu.

Sasa Mufti ni msomi hawezi kukurupuka tu na kudai fulani ni fisadi pasina kuwa na vielelezo (kumbuka uislamu unataka mtu atuhumiwe kwa vielelezo na sio watu fulani wanamhisi kuwa yeye ni fisadi wengine ni chuki zao binafsi au hasidi zimewatala)

Tukija katika swala la Kadhi hii sio mahakama tu bali mfumo mzima wa maisha ya waislamu. Ni ajabu kama si kichekesho eti sharia za kiislamu ziweke katika mahakama ya circular. Utahukumu vipi kuhusu ndoa wewe hakimu ambaye hujui hata herufi zake zimeandikwaje huoni ni ajabu. Pili unahukumu eti katika tafsiri ya mtu. Kumbuka tafsiri ni mtu aonavyo yeye na sio watu wote waonavyo hivyo basi kuna hatari mahakama zikatawaliwa na mlongo mmoja. Na sio ndoa tu, utawala, ujirani na mengineo mengi je haya tufate kanisa linavyosema au uislamu unavyosema?

Kiufupi CCM naona imejitafutia kaa la moto la hili wamelipata. Waislamu wanakuwa kimya lakini linapotokea jambo kama hili huwa kitu kimoja. Dhambi ya ubaguzi wa dini ni mbaya na Tanzania itachafuka tukielekea huko ule kawaimbo wa amani utatoweka.



Nionavyo mimi tatizo si kuanzishwa mahakama ya Kadhi, bali namna itakavyokuwa attached kwenye system ya nchi. Inavyoonekana ni kwamba waislam wanataka mahakama hii iwe chini ya Serikali lakini wao ndio wawe na maamuzi yote ya kiutendaji. Sidhani kama inashindikana waislam wangeamua kuwa na mahakama hii katika set up zao bila kuihusisha serikali. Dini nyingine kama Catholic wanazo mahakama zao na zinafanya kazi bila tatizo, kwanini waislam wasifuate mfano huu badala yake wanataka tu kubebwa na serikali?
 
huyo muft, hao wa chini yake je?? wasioenda shule kabisa???

tatizo ni CCM kujadili hii ishu, haikutakiwa kabisa kujadiliwa!
 
Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Na Ummy Muya
Alisema serikali imedhihirisha kuwa inaendeshwa na Wakristo na si kweli kama serikali haina dini na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.


Source: Mwananchi


CCM watajuta kuweka swala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao uchaguzi ya 2005.

Kwani serikali ilikuwa ikiendeshwa na waislamu kabla?
 
Waziri ametuthibitishia kama Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura kwa kigezo kuwa suala hilo litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na sio kuchanganywa kama ilivyokuwa mwaka 1970 katika Sheria ya Ndoa na kuwanyima haki Waislamu,alisema.

Ebo.! kumbe kulikuwa na ahadi? zilikuwa zikitolewa wapi? maana hatukuwahi kuzisikia hadharani!
Kama zilikuwa zikitolewa ndani ya nyumba za ibada then sisi maf........ kwisha. ni chama cha kidini na wla si kweli kwamba serikali ya sisi maf... haina dini
 
Imetosha kuwa ujumbe umewasilishwa au umefika sasa kama wataenda ikulu au uwanja waTaifa hayo ni maslahi binafsi ,kama ni kuruka nae mufti ameruka kwa kuwakabidhi waislamu uhuru wao wa kuchagua badala ya kuing'ang'ania CCM iliyojaa uwongo kwa kuthibitika kuwepo kwa ahadi hewa lukuki.

Kumbuka kuwa hao unaofikiri ni mbadala wa ccm walikuwa ccm, umewauliza kama wameacha uwongo? Usije ukafikiri atakayeweza kuleta mahakama ya Kadhi ndio huyo anayeweza kujenga barabara, madaraja, madarasa, n.k. Usileweshwe na jinamizi la huyu Kadhi ukasahau mengine!
 
serikali itambue kuwa Bakwata iko hai hao Wakristo walikuwa wapi wakati sisi tukipigania uhuru,alihoji.



Ama.! kwani uhuru walipigania waislamu pekee na kwa hiyo hilo tu liwape kuvunja umoja na mshkamano wetu leo?
 
"Haki ya waislamu" Haki gani hiyo ambayo sheria za Tanzania inawanyima? Na kama zipo serikali imeahidi kuziweka haki hizo kwenye sheria mama tatizo ni nini tena? Tuelimisheni.Tunacheza pamoja,tunasoma pamoja,tunalima pamoja,maji tunachota pamoja,mifugo tunachunga pamoja, maofisini kazi pamoja sasa kwa nini mjitenge?Huko bara watu wamechanganyikana.Msiannalie pwani tu.Tuacheni tushirikiane kusoma sayansi na teknologia ili tuondokane na aibu ya umaskini.Kwanza mbeleni hao wanawake wengi hawatakwepo.utawalisha na kuwasomesha niniwatoto titiri?mabinti wenyewe wakimaliza shule hizo za sekondari za kata hawatakubali uwake-wenza.Watu wapiganie mambo mengine siyo namna ya kugawa mirathi kwa wanawake.
 
Wakati huohuo, Sheikh Salum Rwambo alisema anawashangaa wabunge Waislamu ambao baadhi ni mahajat na malhaj wanakaa kimya na kushindwa kutetea hoja za msingi na kudai kuwa huo sasa ndio mwisho wao wa kuwaita masheikh na kutaka waombewe dua ili wasipate wepesi katika kampeni zao. Sheikh Rwambo pia alimsifia mbunge wa Nzega Lucas Selelii kwamba ni miongoni mwa wabunge katika Bunge hilo wanaozungumza ukweli na kwa kujiamini tofauti na wengine ambao wanaenda kukaa bila kufanya kazi zilizowapeleka.

Mmmhhh,! mwisho wao bungeni wabunge wa kiislamu?
Mbona walishatangaziwa mwisho siku nyingi. Sasa kwa hiyo ndiyo mtafanya nini masheik?
kuinyima sisi maf... kura hiyo imeshatangazwa hata kabla yenu. Msitake kuiteka nyara hoja. Wananchi walishasema hawataipa kura sisi maf.. si kwa kigezo hicho cha dini, bali kwa kigezo cha kurudisha nyuma maendeleo.
Nyie kumbe kwenu maendeleo ni mahakama ya kadhi? mbona hoja mlizo nazo kuhusu uanzishwaji wake ni dhaifu kuliko?
 
Kwa taharifa ya waislamu, Rais wa Tz 2010 ameshapangwa na wenye nchi, wapige wasipige kura kwa Kikwete, haitasaidia kitu. Nawashauri wapiganie kujenga mashule na mahospitari kuliko haya masuala ya mahakama ya kadhi.
 
Hapa hawa masijui MUFTIS etc wanalilia maslahi. Wanajua serikali ikianzisha watapata ulaji kwa kuajiriwa na kuwa na office in all regions and districts. Kama si hivyo kwa nini wasiseme kuwe na sheria maalumu for that. Mi naona hawa jamaa ni choka mbaya tu hawana lolote..kelele tu

Ushauri: Chapa kazi acheni longo longo... anzisheni miradi iwape fedha acheni longo longo hii serikali yenu kwanza ni mfu haiwezi tatua matatizo yenu mengi sana.
 
Back
Top Bottom