Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Bakwata hawana ubavu huo wanabwaka tu, wao wenyewe credibility yao ni questionable wasafishe nyumba yao kwanza.

Hawana jipya zaidi ya kutafuta njia ya kutokea na kuficha madudu yao. Ni ukweli usio na shaka uislam haupo kitaasisi kama ukristo na madhehebu yake catholics, Lutheran, Anglican nk. Bakwata ni kikundi cha wajanja wachache wasio na mandate yeyote kwa waislam ndio maana no body is taking them serious.

Masatu.. nakuunga mkono 100% kuhusu credibility ya BAKWATA kwenye safu za waislamu.

Ila ni ukweli usiopingika kuwa at least kwa hili they have said some thing.... yaani kwa maneno mengine ile kauli ya enough is enough wameithibitisha. Nadhani tuwapongeze.

Unajuwa sikutegemea kusikia kauli hii kutoka BAKWATA. Maana hawakuwa na kuumauma maneno..they went very straight to the pint na kuita nyeupe ni white.

Takbiir.
 
Wajameni.... Sintojiingiza kwenye uchambuzi wa kidini, siwezi na sina upeo

Swali ni moja tu, JE WASIPOWAPA CCM WATAWAPA NANI WENGINE? CUF? CHADEMA? TADEA?

...i think its just a move to score some points kwa waumini wake now that anajongelea upinzani wa kiti chake
 
Kwa ufupi CCM inaendelea kushikwa pabaya maana kila wanapojaribu kuziba kunatoboka na kuvuja kwengine.
Inaelekea wanapoteza wapiga kura kwenye mambo yahusuyo Muungano,Ufisadi na sasa waiislamu wenye siasa kali bado wakiristu wenye siasa kali naona wao bado wanajikurubisha kwa kila hali ,wakiristu amkeni wacheni kuikumbatia CCM ,vyama mbadala vimejaa tele ahadi za CCM zitawatoa vibega.
 
Na wasiislaam wasiokuwemo Bakwata, kama Answari Sunaah, (Mtaniwia radhi kama nimekosea spelling) nao itabidi waanzishe mahakama ya kadhi yao na ilipiwe na serikali hihi hihi bila kuleta vumbi?
 
Bakwata hawana ubavu huo wanabwaka tu, wao wenyewe credibility yao ni questionable wasafishe nyumba yao kwanza.

Hawana jipya zaidi ya kutafuta njia ya kutokea na kuficha madudu yao. Ni ukweli usio na shaka uislam haupo kitaasisi kama ukristo na madhehebu yake catholics, Lutheran, Anglican nk. Bakwata ni kikundi cha wajanja wachache wasio na mandate yeyote kwa waislam ndio maana no body is taking them serious.

Masatu,

Nakubaliana na uliyoyaeleza isipokuwa niliyo bold. Tatizo la Waislam Tz ni dogo. Serikali haijawaruhusu wajipange waweke viongozi wenye muono kwenye hiyo Bakwata. Na hilo waislam wanaweza kulifanya kama hawataingiliwa katika mambo yao na Serikali. Hakuna uchaguzi mkuu wa Bakwata utafanyika bila kuingiliwa na serikali. Hata TEC au CCT zikiweka na bogus leaders hakuna cha maana wanachoweza kufanya.

Bahati mbaya ni kuwa serikali inafurahi kuwa na dudu bovu kama Bakwata kisha inalipa nguvu nyingi. Na hapo ndipo watu wanapata fursa ya kuwatukana Waislam.

Waislam wanaweza. Mfano mdogo ambao wewe unaufahamu, tazama tofauti ya shule za Bakwata na zilizoanzishwa na vitaasisi vidogo tu vya Kiislam tena karibuni. Waislam wasipoingiliwa katika masuala yao wanaweza kufanya zaidi ya hapo.
 
Mambo yote mengine ambayo sisi tunayapigia kelele hayawafanyi wao kuichukia CCM; yaani yote yaliyofanyika dhidi ya nchi yetu na utajiri wetu wao hayawagusi wala kuwataka waumini wao kuyafanya ya kisiasa na kuiadhibu CCM; yaani yote hayo hayajafikia kiwango cha kuwakera.. isipokuwa hili moja tu?

Nachelea kusema huu ni ubinafsi, kwani hii nchi imeraluliwa na hawa manyang'au wa CCM. Sasa kusema wanakataa CCM kwa sababu tu ya kukatiliwa kwa mahakama ya kadhi ambayo ni sehemu yao ya ibada haingii akili na naweza kusema ni uamuzi wa kukurupuka.

Naikataa CCM kwa sababu kuu, imeifilisi nchi hii na hakuna matumaini kwa waTZ.
 
Mi nafikiri tuaiche Tz kama secular nation. Tusiingize halafu ya kidini ili kuwe na fair play kwa dini na imani zote. Wahubiriane misikitini na makanisani na watu wawe converted kwa kutafuta pepo na si maslahi ya kiuchumi, vyeo serkalini n.k
 
There are two things in our job. Criticism i accept with respect. Disrespect i dont accept and dont respect" - Arsene Wenger.

Let us discuss the issue with clear mind. As far as I am concerned there is nothing wrong with having " mahakama ya Kadhi". The sticking point is to make it a constitutional affair. Its establishment does not need a government hand, it should be internally handled by the Muslim community itself. We all know the legality and acceptability of BAKWATA, an institution established with a government hand, among the Muslim community is not at 100% with alot of discenting voices. Some going as far as calling it a govern;ent tool used to deter development of the concerned community. The isue was a non starter in the parliament. Here again we see how politician can exploit and distabilise a country by giving false or hard to implement promises, just to have your vote.

Muslims, if they will heed to the call, they will be doing all of us a favor to vote CCM out,but will they still have the Kadhi demand?
 
Nakubaliana na mheshimiwa Omulangi. Ingefa taasisi za dini kuwekeza kwenye kulea wafuasi wao na kukusanya wengine wengi mitaani tuliopotea na kuwaelekeza kwa Mwenyezi Mungu Subhana wa taalah! Hizi mahakama zitatuvuruga tuu, that is a time bomb!! Poor us!!!!!
 
Let us discuss the issue with clear mind. As far as I am concerned there is nothing wrong with having " mahakama ya Kadhi". The sticking point is to make it a constitutional affair. Its establishment does not need a government hand, it should be internally handled by the Muslim community itself. We all know the legality and acceptability of BAKWATA, an institution established with a government hand, among the Muslim community is not at 100% with alot of discenting voices. Some going as far as calling it a govern;ent tool used to deter development of the concerned community. The isue was a non starter in the parliament. Here again we see how politician can exploit and distabilise a country by giving false or hard to implement promises, just to have your vote.

Muslims, if they will heed to the call, they will be doing all of us a favor to vote CCM out,but will they still have the Kadhi demand?

Nimesoma maoni ya mufti mmoja gazeti la mwananchi, anaweka wazi kabisa kwamba hiyo mahakama na maamuzi yake ni sehemu ya ibada, na kasema lazima hakimu awe muislamu, haiwezekani John akahusika kuendesha ibada hiyo.

Sasa nikabaki nashangaa, kumbe wanacho lalamika ni nini? mbona kumbe wanaelewa? Iweje serikali iunde mahakama ambayo ajira zake zitalenga kundi moja la jamii yaani waislamu tu? Je hawaoni kwamba hiyo itakuwa inaleta ubaguzi na kuvunja katiba?

Siwaelewi kwakweli wanapo lalamika kuonewa wakati ukweli wanaujua. Wao wajipange waianzishe kama taasisi yao lakini si chini ya serikali.

Kwa hapa CCM ilikurupuka kuirukia hoja kwa uroho wa kura, so let them pay for it!
 
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu. Mzee Mwanakijiji kuhusu alleged grand corruption cases ni still allegation hakuna substance wala proof katika hilo bali ni accusations tu. Sasa Mufti ni msomi hawezi kukurupuka tu na kudai fulani ni fisadi pasina kuwa na vielelezo (kumbuka uislamu unataka mtu atuhumiwe kwa vielelezo na sio watu fulani wanamhisi kuwa yeye ni fisadi wengine ni chuki zao binafsi au hasidi zimewatala)

Hakuna mtu aliyesema Mufti akurupuke and start naming names, it is very clear that there is something very wrong going on with this government. hakuna asiyejua kwamba corruption inayoendelea katika hili taifa letu haijawahi kutokea. Yeye kama kiongozi wa dini alikuwa anatakiwa kukemea haya kwa viongozi wa serikali na taifa kwa ujumla.

Uadilifu wa viongozi kwa ujumla ni kitu muhimu na ungeweza kusaidia sana kutuepusha na malumbano haya kama wangekuwa wa kweli na kutoa ahadi ambazo wanajua zinatekelezeka sio kutoa ahadi ili wapewe kura.

Na kama mufti angekuwa mjanja akagusia kidogo tu jinsi CCM walivyowalaghai na sio wao tu bali taifa zima nadhai watu wote wangelichukulia hili jambo tofauti kabisa.
 
Katika taarifa yake, Bakwata ilifikia hatua ya kusema Waislamu wasimchague Rais Jakaya Kikwete iwapo atasimamishwa na CCM kugombea urais,...

... na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.
Naona mapungufu mengi tu. Kama umeshaamua JK asichaguliwe na Waislamu 2010, inakuwaje tena uje kusema kuwa huyo huyo asiyetakiwa kuchaguliwa anachafuliwa na kauli ya Waziri wake? Ni contradictions au ni kuuma na kupulizia?
 
Nimesoma maoni ya mufti mmoja gazeti la mwananchi, anaweka wazi kabisa kwamba hiyo mahakama na maamuzi yake ni sehemu ya ibada, na kasema lazima hakimu awe muislamu, haiwezekani John akahusika kuendesha ibada hiyo.

Sasa nikabaki nashangaa, kumbe wanacho lalamika ni nini? mbona kumbe wanaelewa? Iweje serikali iunde mahakama ambayo ajira zake zitalenga kundi moja la jamii yaani waislamu tu? Je hawaoni kwamba hiyo itakuwa inaleta ubaguzi na kuvunja katiba?

Siwaelewi kwakweli wanapo lalamika kuonewa wakati ukweli wanaujua. Wao wajipange waianzishe kama taasisi yao lakini si chini ya serikali.

Kwa hapa CCM ilikurupuka kuirukia hoja kwa uroho wa kura, so let them pay for it!

Ni hapo tunasema kwa Mufti hakuna kichwa cha mchanganuo,Ibada iwe yako wewe muislam halafu kodi yetu sote ndo ilipie ibada yako. Akili mukichwa kwanini asiombe msaada huo wa Ibada yake Saudia , au waumini wake kama watamkubalia
 
Ni kweli, Mufti inabidi aiangalie kauli yake kwa upya. si vizuri kuambatisha vitu vinavyohusu dini fulani na serikali na pia alipaswa kuelewa kwamba serikali haina dini
 
zanzibar si kuna mahakama ya kadhi? mbona hatujasikia hata siku moja mtu kakatwa mkono?
mbona pia hatujasikia watu zaidi ya asilimia 60 kujitoa kwenye uislam kwa kuwa kuna mahakama ya kadhi?

mwanakijiji mufti ndio amekerwa na sio hili tu, lakini kama kazi yake kama mufti hili lazima limkere zaidi, kwa kuwa kachaguliwa umufti kuwawakilisha waislam kwa mujibu wa dini, na wananchi walipotaka kuwakilishwa kwenye kupigania mambo yasiyokuwa ya kiroho ndio waliwachagua kina zitto kable, dr slaa, john cheyo, Chenge, Lowasa...n.k

mufti anaongea kwa mujibu wa jukumu lake kama kiongozi wa kiroho.
 
Tatizo si kuwa na mahakama tatizo ni kudhalilishwa na kuonewa waislamu.
Mkuu Mdondoaji, lazima nikubali kuwa sina ufahamu wa kutosha kuhusiana na madai ya jumuiya ya Waislamu kwa serikali katika kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi.

Nawaomba wote wenye ujuzi wanisaidie kuelewa zaidi mambo yafuatayo;
1. Kama Mahakama hiyo ni sehemu ya ibada ya waislam, inawezekana ikaanzishwa na waislam wenyewe? Kama haiwezekani, ni kwanini?
2. Naelewa wajibu wa serikali kufanya hivyo kwa kubadilisha katiba kama wabunge wataridhia. Hii ikifanyika, ina maana madhehebu yote nchini yatakuwa na haki ya kuanzisha mahakama zake kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo. Je, baada ya kufanya hivyo, wajibu wa serikali utakuwa umekwisha na mahakama hizo zitahudumiwa na madhehebu husika au zitajihudumia zenyewe?

3. Nimesikia baadhi ya wabunge wakianza kuicharukia serikali kuhusu mijadala ya kufikia muafaka wa kuanzisha au kutoanzisha mahakama ya Kadhi. Wengine wakidai kuwa, dini nyingine hazina haki ya kujadili suala hilo kwakuwa linawahusu waislam pekee. Nadhani ni kweli.
Kama wote tunadhani hivyo, je ni kwa vipi suala la Katiba ya nchi lisihusu watu wote? Je, Katiba hii itabadilishwa vipi (Bungeni) bila kujadiliwa kwa kina na wabunge wote (walau 2/3) kuipitisha ili kuwa sheria? Je, waislam wako tayari kuweka mapendekezo yao yote kwa wabunge (mchanganyiko) ili kujadili mipaka na malengo ya mahakama hiyo?

Naomba wanaojua zaidi watufahamishe. Maana tunaweza kujadili bila kujua tunachokijadili halafu tukapotoshana katika mambo muhimu ya kiimani.
 
Nao wakristo waungane kuanzisha "mahakama zao kiroho ndani ya katiba"?Nchi hii itakuwaje?anyway siwalaumu ndugu zangu Waislam maana CCM na serikali yake iliwahaidi jambo hili na hata ikawekwa kwenye ilani yao ya uchaguzi,maskini haweakujua kama wanatapeliwa ili watoe kura kama ambavyo ahadi nyingi hewa zilizotolewa!
Bytheway lkn Waislam hawajachambua wazi wanakosa kitu gani kwenye sheria mama zilizopo tz hivi sasa hadi wanapigania mahakama ya kadhi?watapata ni ni ikianzishwa mahakama ya kadhi ambacho sasa hawapati?

Hiyo ahadi haikuwa absolute, ila ccm ilikuwa inaangalia uwezekano wa kuanzisha mahakama ya kadhi!
 
Back
Top Bottom