Mtuhumiwa ma mauaji ya Mwangosi afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

Mkuu "nimegooguka" hakuna profile yake hata katika secondary schools,sijui ni darasa la saba.Haya ni mazingaombwe mengine kama ya Kova

yaani kote huko hakuna. Hili jina haliko fB, twitter, google, wikipedia wala vodacom. Wenye access na makampuni mengine hebu check halafu mwaga namba jamvini
 
Naona nchimbi bado anataka kukwepa kikombe hiki kimsingi hawezi ruka hiki kikombe ,chagonja,kamuhanda na igp huyu dogo hakuwasha defender peke yake tu bila kupewa amri tutaendelea kulijadili mpaka kieleweke najua limekwenda mahakamani ili kuzuia lisijadiliwe mjadala uko palepale!!!!!!!!!!!!
 
Group lote lililokuwa kwenye Picha lilitakiwa kufikishwa Mbele ya Sheria
Bila kukosa huyo RPC muuaji ..
Nchi hii na wiongozi wake wanasikitisha sana
 
walivyomwua-wangosi.JPG

wote hawa ni wauwaji, Mwema na Felesh wako achani kutuletea maigizo! enough is enough!
 
daima nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa maofisa wengi wa POLISI. Ni Tibaigana Peke yake aliekuwa na akili TIMAMU na Aliekuwa anajua kutenda kazi kwa mujibu wa sheria, wengi wao ni vilaza na wasioweza kutimiza wajibu wao.
 
Naona nchimbi bado anataka kukwepa kikombe hiki kimsingi hawezi ruka hiki kikombe ,chagonja,kamuhanda na igp huyu dogo hakuwasha defender peke yake tu bila kupewa amri tutaendelea kulijadili mpaka kieleweke najua limekwenda mahakamani ili kuzuia lisijadiliwe mjadala uko palepale!!!!!!!!!!!!

Sitaamini kuwa hatua stahiki zimechukuliwa dhidi ya muuaji ikiwa Rpc hajashitakia na mtoa order kwani huyo kijana kama siyo wa kuchongwa basi kaonewa maani alitii order aliyopewa na mkubwa wake aliyekuwepo eneo la tukio. Mi nawashangaa sana waandishi na watanzania wanaporipoti kuwa muuaji amefikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali, lengo ni nini? Unadhani ni kuwa atatoroka au ni kumfichia aibu mwenzao, wanamleta na kumrudisha na shangingi? Maana yake amefanya tendo la kishujaa. Tuwe makini na hatua hizi.
 
Jamani Picha halisi ya haka katoto kauaji ili tukijue, ukweli ni kwamba huyu mtoto hatafungwa atahamishwa kituo(mkoa) au akionekana anatoa siri watamuua.
Kamuhanda anatakiwa mshitakiwa nambari1
 
RPC Hawezi kuwa shahidi kwani huyo ndiye anatakiwa kuwa Mshitakiwa No.1, Nadhani Shahidi NO.1 anakiwa kuwa RCO
 
Just curious, katika hii kesi polisi wanapeleleza nini ambacho hakijakamilika?
Upelelezi wa picha tu hautoshi,there is lot of facts to be established,Kesi ya murder ni kesi kubwa kuliko zote katika sheria za Tanzania na ndiyo yenye adhabu kubwa kuzidi kesi nyingine yoyote except treason,hivyo inatakiwa ushahidi ambao ni fool proof,usiache any reasonable doubt,uwe water tight,If you know what I mean.
Kitu pekee ambacho sikifurahii ni kuachwa kwa wale wengine wanaoonekana katika picha,hata kama mtuhumiwa kakiri kuwa ndiyew aliyeuwa lakini bila amri ya RPC aliyekuwepo kwenye tukio isingetokea,bila wale accomplices wanaooonekana kwenye picha kusaidia kumuangusha chini marehemu na kumzingira muuaji labda asingeweza kufanikisha lengo,inawezekana pia wakati mtuhumiwa analipua bomu marehemu aliisha fariki kutokana na kipigo alichokuwa amepewa na wale waliomzingira.Kuna kitu kwenye criminology kinaitwa CAUSATION. Inabidi wakiangalie sana katika kutenda haki.
 
Hivi hawa jamaa wanadhani sisi sote ni vilaza kama wao? Baada ya kuona nchi haikaliki sasa wanakuja na upuuzi huu??? Hivi kuna mtanzania ata mmoja ataamini huu upuuzi. Kuna sababu nyingi za kumkataa huyu jamaa :
  • kwanini apelekwe mmoja na wakati wanaoonekana kwenye picha ni wengi?
  • kwanini aingie mahakamani kwa kufichwa sana kama si kuwa anapelekwa pale ili mahakama ifanye danganya toto ili badae aachiwe na kurudi mtaani?
  • kwanini police walishatoa kauli ya kutojulikana muuji?
kamuhanda anatakiwa rumande mara moja,
 
Usije kuta tumepigwa changa la macho aliyepandishwa kizimbani siye yule muuaji wa mwangosi
 
halafu wanadai karudishwa rumande kwa kutumia gari binafsi? Kwa nini afichwe sura? Na kwa nini askari wote waliomsindikiza wavae kiraia? Kuna jambo hapa

Hata mi hainiingii akilini kabisa,huu ni uzushi
 
Back
Top Bottom