Mtoto wa Wassira ajiunga Chadema

Hawa Chadema ni kuokoteza watoto wa vigogo tu sasa

Halafu wanajifanya wanawachukia baba zao eti mafisadi,kwani mtoto wa panya hakosi mkia,huko USA kafika kwa pesa gani?

Halafu kuna yule alikuwa mwenyekiti wa vijana arusha wa ccm walimchukua kwa mbwembwe kaishia wapi?
 
IMG_1642.JPG


Ni mtoto wa Tyson Wasira huyu?
wanaomfahmu zaidi tujuzeni maana lisije kuwa pandikizi tu
 
Nawasubiri rafiki zangu Ridhiwani Kikwete, Januari Makamba, Wilium Malecela nk. Salama yao ni kuokoka mapema, ukombozi u mbele yao tu.
 
duh naona sisas ya tanzania sasa inachukua upepo mpya ipo siku utasikia yule first born wa baba mwanahasha naye kavua gamba.........
 
Wana-CDM kidogo tuwe na subira na wanachama wapya wanaojiunga kwenye mapambano kwani kila mmoja nje ya zile koo za kitawala kule CCM, tumezulumika kwa njia moja au nyingine.
 
Hapo kwenye bluu chini;

hao vijana wenzetu wawili tayari ni wana-CDM hata ukitazama wanavyotembea, wanavyoongea, sema tu woga wao eti ni kule kuogopa kuogopa kwao kule tishio la kupewa radhi na wazee wao kukipa mgongo chama kilichowajazia wazazi wao MI-TONGE KIBAO KINYWANI.

Lakini huyo mwingine ni mtaalam wa flip flop tupu.


Nawasubiri rafiki zangu Ridhiwani Kikwete, Januari Makamba, Wiliam Malecela nk. Salama yao ni kuokoka mapema, ukombozi u mbele yao tu.
 
Stephen Wassira hafai kwa lolote. Hata akisafishwa, hasafishiki. Siku akiingia CDM, na akakubaliwa, ndipo nitakapojiridhisha kuwa CDM tumekuwa vilaza wa kufikiri. HIVI WASIRA AKIJA CHADEMA, TUTAMPA KAZI GANI?
Historia inatuambia kuwa Wassira aliwahi kujinga na chama cha upinzani (NCCR MAGEUZI).Pengine siku za mwisho za CCM zikikaribia anaweza kuwa mwanachama wa CHADEMA.
 
Stephen Wassira hafai kwa lolote. Hata akisafishwa, hasafishiki. Siku akiingia CDM, na akakubaliwa, ndipo nitakapojiridhisha kuwa CDM tumekuwa vilaza wa kufikiri. HIVI WASIRA AKIJA CHADEMA, TUTAMPA KAZI GANI?

Kazi pekee anayoiweza Wassira ni kutukana, hivyo tutampa kazi ya kuwatukana MAGAMBA
 
Kwa jinsi Wasira anavyochukia upinzani sidhani kama hakuna mchezo mchafu unaotaka kuchezwa hapo. Kumbuka hata baba yake aliwahi kutumika kama mamluki ili akavuruge upinzani

Unamkumbuka Makongoro Nyerere ambaye alipoenda kuwa mwanachama na mbunge kupitia chama cha upinzani wakati Nyerere babake akiwa hai. Madaraka Nyerere alikuwa mbunge huko Arusha kama sijachanganya kupitia NCCR Mageuzi wakati mzee wa Kiraracha (nji hii) aka Lyatonga Mrema alipoiteka Tanzania na kuitetemesha CCM kutokana na kosa la Mwinyi kumwengu kwa sababu ya kutowajibika pamoja kwa malengo ya kulindana.
 
Wassira ni mmoja wa waanzilishi wa CHADEMA. Hilo watu wengi hawalifahamu. Atarudi tu.
 
Unamkumbuka Madaraka Nyerere ambaye ni kifungua mimba alipoenda kuwa mwanachama na mbunge kupitia chama cha upinzani wakati Nyerere babake akiwa hai. Madaraka Nyerere alikuwa mbunge huko Arusha kama sijachanganya kupitia NCCR Mageuzi wakati mzee wa Kiraracha (nji hii) aka Lyatonga Mrema alipoiteka Tanzania na kuitetemesha CCM kutokana na kosa la Mwinyi kumwengu kwa sababu ya kutowajibika pamoja kwa malengo ya kulindana.

mkuu .... correction .... alikuwa ni Makongoro Nyerere .... ambaye sasa ni ubunge wa East Africa legislative assembly
 
May be huyo ndo katumwaa kuja kukakamilisha kale ka mradi ka kuisambaratisha CDM before mwaka kuisha.

Zaidi ya kuwa mtoto wa Wasira sidhani kama ana nguvu kwenye chama kilichomtuma kwani kama baba yake anaaminika na ana nguvu kwenye chama chake sidhani kama mtoto ana nguvu kivile (kwa kesi hii MTOTO WA NYOKA SI NYOKA)
 
Historia inatuambia kuwa Wassira aliwahi kujinga na chama cha upinzani (NCCR MAGEUZI).Pengine siku za mwisho za CCM zikikaribia anaweza kuwa mwanachama wa CHADEMA.
Si sahihi kumhukumu kijana huyu na hata wengine watakaojitokeza kujiunga na CHADEMA kwa makosa ya wazazi au wanafamilia zao. Steven Wassira anafahamika kwa political opportunist behavior yake na kinachomuweka CCM sasa hivi ni mkate anaopata kutokana na cheo alichohongwa na kina Makamba ili abaki huko. Hana msimamo na ni Political harlot ambaye bei yake huamuliwa na njaa yake. Wanaojidanganya ana mapenzi ya kweli na CCM wajaribu wamuengue kwenye shibe waone rangi yake halisi.

 
Vigogo sasa wanatanguliza watoto wao cdm katika harakati za kutafuta mahali pa kuficha sura Tz inapobadilika na kuipa kisogo ccm.
 
Zaidi ya kuwa mtoto wa Wasira sidhani kama ana nguvu kwenye chama kilichomtuma kwani kama baba yake anaaminika na ana nguvu kwenye chama chake sidhani kama mtoto ana nguvu kivile (kwa kesi hii MTOTO WA NYOKA SI NYOKA)

Huyo sio mtoto wa Steven Wasira. Kalaga baho.
 
Back
Top Bottom