BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
wandugu, nilipata mtoto na binti mmoja miaka kadhaa iliyopita, hatukuoana wala kuwahi kuishi pamoja, nilimchukua mtoto akiwa na miaka miwili (pls dont ask why)na nilimlea mwenyewe hadi nilipooa, hii ikiwa ni miaka miwili na nusu baadae, mke wangu alimkubali na kumlea mtoto kwa mapenzi yote kiasi kwamba ni wachache mno ambao wanafahamu kuwa yeye sie mama yake mzazi, hata mtoto na wadogo zake hawalifahamu hilo na baadhi ya ndugu zangu pia. mama mzazi wa mtoto alishaolewa na ana maisha yake kwa mumewe na watoto wao na tuna mawasiliano ya msimu kuhusu mtoto, hajawahi kumuona mwanae kwa zaidi ya miaka nane sasa! tatizo linakuja ni kwamba mtoto amekua na ana shughuli mbeleni ambayo sidhani kama itakuwa jambo la busara mama yake kutohudhuria au kutopata taarifa, je mtoto, wadogo zake, na mama yake(mke wangu) watalipokeaje?!nachelea kufanya lolote litakaloikosesha familia yangu amani, i love my family na siko tayari kuona hili litokee,je nimpotezee tu mama yake bila kumfahamisha? but in otherside ana haki kwani ni mwanae! ni wakati gani muafaka wa kumuweka wazi mtoto kuhusu hili au nalo nilipotezee hadi atakapokuja gundua mwenyewe mbele ya safari??seriosly hili linanitatiza na noamba ushauri wako..tafadhali usinihikumu kwa makosa ya nyuma, nakaribisha ushauri wako..
Ni kweli kabisa huyo mama ana haki kama mama wa mtoto, lakini alikuwa wapi miaka zaidi ya minane bila hata kutamani kumtia machoni mwanae kuona kama anaendelea vizuri au la na pia kujenga uhusiano na mwanae ili wafahamiane kwa karibu!? Muulize Mkeo ili usikilize naye ana maoni gani kuhusu swala hili, lakini kwa maoni yangu hasa ukitilia maanani kwamba miaka yote hii amempa malezi bora binti yenu na yeye na wadogo zake mliojaliwa na mkeo bila wao kugundua kama dada yao ana mama tofauti, basi mpotezee tu huyo mama ila kama mkeo ana mawazo tofauti basi msikilize.