mtoto wa nje anaweza kuzuia ndoa isifungwe

Joyceline

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
1,010
166
Kaka yangu anaoa tarehe 24 April, bado wiki 1 ndoa ianze kutangazwa, wiki 1 moja iliyopita kapigiwa simu na binti 1 akajitambulisha kwake wanajuana waliwahi kuwa na uhusiano mwaka 2004 wakaachana alimfumania msichana, kumbe wakati wanaachana msichana alikuwa na mimba hajijui wakapoteana msichana amezaa sasa hv mtoto ana miaka 6, kamtafuta kaka yangu kwa marafiki hadi kampata. wakaenda kupima DNA kweli mtot ni wa kaka na amemkubali kulipa gharama na matunzo yote na pia atampeleka shule boarding atakuwa anamuhudumia. Ila msichana hatakia anasema yeye anataka kuolewa waleee mtoto wao, mwanaume hataki kumuoa anamwambia sikupendi, masichana ametishia kwenda kupinga ndoa kanisan, la sivyoa aolewe yeye. na msichana anayeolewa alivyosiskia amekasirika amemwambia mwanume nakuacha mlee mtoto wenu, kaka yangu amechanganyikiwa ni mwanume lakini kwa mara ya kwanza nimemuona akilia kama mtoto,kwanza ameachwa ndoa inakaribia, pili hamtaki huyo aliyezaa naye. kama huyo mchumba wake atamrudia huyo mama mtoto akienda kupinga ndoa itavunjika ua kuna taratibu zitafuatwa, maana kamuambia mama mtoto kwamba nikikuoa nitakutesa sana mimi sikupendi kuzaa siyo kigezo, mimi nimekosa cha kumshauri maana ni mwanamke na wote nawaonea huruma.
 
Akapinge ndoa kwa sababu gani tena ? kwani aliahidiwa ndoa au anacheti cha ndoa na huyo kakaako mmh
Huyo aliyezaa naye amweleze tu ukweli kwamba hana mpango wa kumuoa ila atamtunza mtoto .huyu mwingine na yeye inabidi awe mpole yeye ndo amependwa na ameahidiwa ndoa hana haja ya kupanic
Haya ni maisha tu
 
Ni kanisa gani hilo litamsikiza huyo hayawani? Yaani kuzaa ndo iwe nongwa!
Huyo kaka'ko aendelee na mipango yake ya ndoa na huyo ampendae, wala haina kwere..asimsikize kabisa huyo kizabizabina wala asimpe fursa zaidi ya kumlea mtoto.
 
Hana sababu yoyote ya kupinga ndoa, na hata huko kanisani hataeleweka maana kama nimeelewa vizuri kaka yako hajawahi kuishi nae wala kumuoa in any way, they just had an affair ambayo ndani yake alipatikana mtoto, ambaye amemficha hadi six years ndo anaibuka. kimsingi hamna kesi, yeye kaka yako apige moyo konde ambembeleze mwali wake aweke hayo mambo wazi kwa wazazi wote na hata kanisani solution ipatikane aoe.
 
kama ni mkatoliki only cheti cha ndoa ndo kinapingamizi otherwise ni ishara tosha kwa bibi harusi wetu mtarajiwa kwamba kaka yetu anatema cheche
 
2004 mpka leo ndo anaibuka na kudai mtoto ni wa kakaako.....wat if its not even true (DNA itahusu)

hakuna ushahidi wowote wa hata waliahidiana kuoana basi walau jamaa adaiwe fidia...
hapana hamna pingamizi la ndoa, kaako aendelee na mpango, kazi kwake kuhakikishia mchumba wake vinginevyo ili waendelee na mpango wa kufunga ndoa....
 
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao
 
DNA wamepima hospital tatu tofauti na majibu yanafanana, mtot ni wake maana wamefanana sana, ila binti anataka kuolewa, na huyu mwingine ameshikilia msimamo hataki, wivu na hasira vinamsumbua
 
kama ni mkatoliki only cheti cha ndoa ndo kinapingamizi otherwise ni ishara tosha kwa bibi harusi wetu mtarajiwa kwamba kaka yetu anatema cheche

siyo katoliki ni makanisa ya kiroho, ila anadai siku ya ndoa ataibuka kanisania siku hiyohiyo na mtoto mbele ya watu wote apinge si atatuharibi shughulu
 
Hana ubavu wa kuweka pingamizi kanisani kwani walisha funga ndoa pamoja? Si alikuwa hawala tu kaka ako alikuwa anamega tu kama ana ushahidi tosha kuwa walikuwa mke na mme kwa vielelezo thabiti kama walisha funga ndoa sasa kaka ako anafunga ya pili hapo sawa lakini kama hakuwahi funga nae ndoa mwambie kaka ako aendelee na mipango ya harusi kama kawa. huyu hawezi fanya lolote na hana madhara.
 
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao

kwenye red nawapenda sana wa hivo.......angechuna brake za mbuzi hapa
kwenye blue miaka sita baadae ndo analiona hilo....alipokuwa apoozea imekuwaje

DNA wamepima hospital tatu tofauti na majibu yanafanana, mtot ni wake maana wamefanana sana, ila binti anataka kuolewa, na huyu mwingine ameshikilia msimamo hataki, wivu na hasira vinamsumbua

hata kama mtoto ni wenu bana, hakuna pingamizi hapo hebu endeleeni na mipango yenu na siku ya siku akileta show off wekeni mlinzi ampe kibano.....huyo dada anataka kumkomoa jamaa tu hamna la ziada lakini kw avile mmeshajua mpango wake mie sioni tatizo
 
msichana ametishia kwenda kupinga ndoa kanisan, la sivyo aolewe yeye. na msichana anayeolewa alivyosiskia amekasirika amemwambia mwanume nakuacha mlee mtoto wenu, kaka yangu amechanganyikiwa ni mwanume lakini kwa mara ya kwanza nimemuona akilia kama mtoto,kwanza ameachwa ndoa inakaribia...[/QUOTE]

Hapa imenichanganya kidogo. Kaka yako ameachwa au mwanamke amekasirika tu kwa sababu mzee amezaa na mwanamke mwingine? Unasema: " Ameachwa ndoa inakaribia..." kwa hiyo ina maana uchumba haupo tena, na sio suala la pingamizi, sio? Lakini kama ni suala la pingamizi sioni uwezekano wa kanisa lolote kukubaliana na huyo mzazi mwenzie wa kaka yako.
 
sasa hii ya kuwa na illegitimate child imekuwa common ehh? ppl are not responsible at all and those poor kids have to pay... My heart goes to the kid poor little thing...

that was off topic... anyway back to the topic... naona huyo mchumba mwenyewe hana msimamo... kwanini anaanza kuzira?
 
sawa mtoto anaumia, lakini mbona mama ndo alifumaniwa na uhusiano ukafa? na bahati mbaya kumbe ana mimba ambayo kakaa kimya hadi six years later. mama ndo ana makosa,angekuwa mwadilifu basi angeomba msamaha waendelee na uhusiano japo isingeguarantee ndoa.
 
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao

Wifi taratibu!
 
Huyo anatishia tu, hakuna kanisa linalotoa pingamizi la ndoa sababu ya kuzaa na mtu, ni proof ya kuoa tu ndo inakubalika.
huyo wifi mpya naye sasa mi nina mashaka naye, ni kweli anampenda huyo kakako na anataka kuwa naye au vipi? alichotakiwa kufanya kwa sasa ni kuwa karibu na huyo mtarajiwa ili amsaidie mawazo nini cha kufanya. kama mume amemhakikishia kuwa anampenda yeye sasa hasira za nini?
 
Mwenye kupinga ndoa ni mwanamke katika mazingira haya:

1. Mwanamke uliyeishi naye mfululizo kwa kipindi cha miezi sita (awali ilikuwa miaka miwili) na kuendelea na ambao mnafanya tendo la ndoa kama mume na mke, kusheria anatambulika kama mke hata kama hamjafunga ndoa, hivyo ni lazima muachane kisheria. Kwa huyu binti na taarifa ya mleta mada inaelekea kuwa hawakuwahi kuishi pamoja na huyu ndugu yako zaidi ya kupeana mimba,

2. Mwanamke uliyezaa naye bila ndoa hata kama hamjaishi pamoja lakini hutunzi yule mtoto. Huyo mwanamke ana haki ya kuzuia ndoa kwa muda ili aweze kupata hatima ya matunzo na malezi ya mtoto yule. Kwa binti huyu si tatizo kwani nduguyo amekubali kumtunza na kumelea mtoto. Pingamizi la ndoa hapa hakuna.

3. Mwanamke uliyefunga naye ndoa, hata kama mmeishi kwa sekunde na mkaachana, hili ni pingamizi tosha hadi pale talaka itakapotolewa mahakamani/au vyombo vingine vyenye mamlaka ya kutengua ndoa. Huyu binti hana ndoa hivyo pingamizi hakuna.

Kwa yote hapo juu huyu binti hawezi kuwa pingamizi kwa ndoa hii na hii ni lazima iwekwe wazi kwa wachungaji/mapadre kabla ya siku ya ndoa il asije akavamia ile ibada maana inawezwa kusitishwa ili kusikiliza malalamiko hivyo itakuwa imeharibu gharama zenu.
 
msichana ametishia kwenda kupinga ndoa kanisan, la sivyo aolewe yeye. na msichana anayeolewa alivyosiskia amekasirika amemwambia mwanume nakuacha mlee mtoto wenu, kaka yangu amechanganyikiwa ni mwanume lakini kwa mara ya kwanza nimemuona akilia kama mtoto,kwanza ameachwa ndoa inakaribia...[/QUOTE]

Hapa imenichanganya kidogo. Kaka yako ameachwa au mwanamke amekasirika tu kwa sababu mzee amezaa na mwanamke mwingine? Unasema: " Ameachwa ndoa inakaribia..." kwa hiyo ina maana uchumba haupo tena, na sio suala la pingamizi, sio? Lakini kama ni suala la pingamizi sioni uwezekano wa kanisa lolote kukubaliana na huyo mzazi mwenzie wa kaka yako.

uchumba mtarajiwa kauvunja hataki kuolewa tena anasema hawezi competition
 
Hana ubavu wa kuweka pingamizi kanisani kwani walisha funga ndoa pamoja? Si alikuwa hawala tu kaka ako alikuwa anamega tu kama ana ushahidi tosha kuwa walikuwa mke na mme kwa vielelezo thabiti kama walisha funga ndoa sasa kaka ako anafunga ya pili hapo sawa lakini kama hakuwahi funga nae ndoa mwambie kaka ako aendelee na mipango ya harusi kama kawa. huyu hawezi fanya lolote na hana madhara.

hawajawahi kufunga ndoa.
Unajua mtarajiwa ni mgeni hapa dar amezaliwa na kukulia Arusha, ndo mara yake ya kwanza kuja dar, kaja kujiandaa na ndoa yake, kufika tu kakutana na mgogo yeye anaongea moja mwenzake mia, kwanza hakutegemea, pili imemshtua alivyopata hizo taarifa alizimia masaa 2 ndo akashtuka, mama mtoto anamwambia hii ni dar unafikiri upo Arusha hapa 2one hiyo ndoa kama utafunga.
 
sawa mtoto anaumia, lakini mbona mama ndo alifumaniwa na uhusiano ukafa? na bahati mbaya kumbe ana mimba ambayo kakaa kimya hadi six years later. mama ndo ana makosa,angekuwa mwadilifu basi angeomba msamaha waendelee na uhusiano japo isingeguarantee ndoa.

both are wrong...having unprotected sex is being irresponsible...whatever goes around comes back...thats Karma... lakini huyu mamii ndo anamakosa zaidi halafu she dont stand a chance... so mchumba wa huyu baba should be smart and go ahead with marriage...
 
Back
Top Bottom