mtoto wa nje anaweza kuzuia ndoa isifungwe

haijarishi ni kanisa la aina gani au bomani au kwa shehe,
mtoto wa nje hazuii ndoa kufungwa
huyo mama anapaswa kuwa mpole kwa yote maana nafasi ya kuolewa allipoteza enzi hizo
kwa misingi hiyo hakuna sheria yoyote au ushahidi wowote wa kuweka pingamizi ati ndoa isifungwe. ukiweza printi hii michango ya wana JF umsomee au umpe asome mwenyewe na atajua ukweli halisi. hata kama unamuogopa bro, jivike ujasiri wa kumtia moyo.
Cha muhimu jitahidi kumtafuta huyo wifi mtarajiwa umtie moyo na umfariji.
hivi ni vijimambo tu vya wadandiao ndoa za watu.
 
unaeokota nae kuni si lazima muokote majivu pamoja!

huyo dada vip? akapinge?
mwambie kaka aendelee na mipango ya harus lakini pia mwambie huyo bi harusi wetu atulie, mbona hivi vitu vipo.
 
Hapo unapimwa msimamo.....aweke msimamo wake wazi, kwa maneno na matendo kwamba:
  1. hatamuoa huyu mzazi mwenzie hata kama hatamuoa huyu mchumba wake wa sasa
  2. yupo tayari kupigania uchumba na ndoa yake, kwa gharama yoyoye.
Huyu ex-gf anapata nguvu za kuongea sababu anaona kuna nafasi ya kurudiana na jamaa! The guy needs to put things into black&white! Hakuna kubembeleza.
 
siyo katoliki ni makanisa ya kiroho, ila anadai siku ya ndoa ataibuka kanisania siku hiyohiyo na mtoto mbele ya watu wote apinge si atatuharibi shughulu
sawa,ataitia doa shughuli, lakini hatazuia ndoa isifungwe. Mpe moyo kaka yako aache kulialia ,aendelee na maanadalizi ya arusi.mchungaji aarifiwe mapema kuhusu swala hilo.mtafute wifi yako mpe moyo ukiweza mpelekee na zawadi.
 
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao

mhh hii situation ni more technical and my advice kwa mwanaume ni kuwa very careful na namna anavyoihandle.

My first instict ni kuhakikisha kuwa anaahirisha ndoa kuavoid the inevitable disruption. Huyo mwanamke hawezi kuishia hapo ataendelea kuwa msumbufu.

This situation is a bit similar na situation aliyokutana nayo rafiki wa mume wangu one year back. What they did then wao walienda kwa lawyer wakaandika affidavit kukana pingamizi. Hii ilikuwa delivered kwa padri one hour before marriage na ikazuia attempt yote ya kuweka pingamizi maana inakubidi utafute order ya mahakama kupinga affidavit na what my clever husband and his fellow lawers did walisubiri jumamosi na wakajua hakuna mahakama iliyo wazi mpaka jumamosi.

but this is only possible kama mke mtarajiwa ni strong na anakubaliana na possibility ya kwenda church akiwa hana uhakika kama ndoa itafungwa au la.

Another solution which has also worked is to ensure mwanamke hapati nafasi ya kuingia kanisani (kama nia ni kuzuia ndoa kanisani). Unaweka bouncers mlangoni. This worked well in Tegeta if you remember two years ago.

Nyingine ni mwanaume kukubali kisirisiri kukutana na mwanamke at least three hours before marriage with a trick kuwa watakuwa pamoja na haendi kanisani. Mkiwa pamoja unafanya naye tendo la ndoa. Akipata ile kitu sawasawa mara nyingi wakina dada wanalala. Unamfungia mlango halafu huyoo unaenda zako kufunga ndoa.

Nyingine ni kubadilisha at the last minute time ya kufunga ndoa. Unatangaza ndoa unafunga saa 11 halafu in reality unafunga saa 3 asubuhi. Halafu pale kanisani jioni mnakuja na kuzuga. Akileta pingamizi tu anaumbuka. Ndoa ishafungwa saa nyingi.

These are some of the basic tricks which some people have succesfully used in the recent past in tanzania.
 
haijarishi ni kanisa la aina gani au bomani au kwa shehe,
mtoto wa nje hazuii ndoa kufungwa
huyo mama anapaswa kuwa mpole kwa yote maana nafasi ya kuolewa allipoteza enzi hizo
kwa misingi hiyo hakuna sheria yoyote au ushahidi wowote wa kuweka pingamizi ati ndoa isifungwe. ukiweza printi hii michango ya wana JF umsomee au umpe asome mwenyewe na atajua ukweli halisi. hata kama unamuogopa bro, jivike ujasiri wa kumtia moyo.
Cha muhimu jitahidi kumtafuta huyo wifi mtarajiwa umtie moyo na umfariji.
hivi ni vijimambo tu vya wadandiao ndoa za watu.

Sheria za kupinga akipata mwanasheria mzuri zipo. its very possible kuzuia ndoa kufungwa (at least kwa siku hiyo) na hii huwa tayari niloss kwa kuwa maandalizi yote huwa yameshafanyika na hela imetoka. From a legal perspective i can think of three possible legal issues zinazoweza kuvuruga ndoa hiii.
 
sasa hii ya kuwa na illegitimate child imekuwa common ehh? ppl are not responsible at all and those poor kids have to pay... My heart goes to the kid poor little thing...

that was off topic... anyway back to the topic... naona huyo mchumba mwenyewe hana msimamo... kwanini anaanza kuzira?

Kwa mazingira yetu ya kiafrika kuwa na mtoto wa nje sio kitu cha kushangaza. Wanaume zetu wa kiafrika ndivyo walivyo. the only thing i tell my husband is to make sure he tells me now or to keep on hiding it for the rest of his life. But najua kuwa hali hii ipo na ndio maana sheria mpya ya watoto iliyopitishwa mwaka huu imesema kuwa hakuna tena mtoto kuitwa mtoto wa nje.
 
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao

Hiyo ni kesi ndogo sana. Huyo ex-GF hana hoja wa chochote cha kudai katika suala la ndoa zaidi ya gharama za kulea mtoto. Mwache apige domo kwani haisaidii chochote. Msaidieni huyo kaka kwani tatizo litakuwa kwa huyo mke wake mtarajiwa. Kwani anaweza kumpiga chini kwa sababu hakuwahi kuambiwa kuwa jamaa ana mtoto na hivyo kujiandaa kuolewa na mtu aliyezaa nje. Kama mchumba wake akimwelewa hakuna tena tatizo.

DNA wamepima hospital tatu tofauti na majibu yanafanana, mtot ni wake maana wamefanana sana, ila binti anataka kuolewa, na huyu mwingine ameshikilia msimamo hataki, wivu na hasira vinamsumbua

Hapa TZ hakuna hospitali inayopima DNA. Ni kwa mkemia mkuu wa serikali tu ndio wanafanya testing na kwa utaratibu maalumu. Kama wamepima hospitali basi anza kuweka alama za kuuliza. Inawezekana huyo binti ni fisadi na ametengeneza mchezo wa kuigiza ili kuharibu ndoa ya wenzake!
 
Hapa TZ hakuna hospitali inayopima DNA.
Mkuu umeona kitu kikubwa sana katika maelezo ya jamaa.
Something is wrong with the presentation!
 
Mwenye kupinga ndoa ni mwanamke katika mazingira haya:

1. Mwanamke uliyeishi naye mfululizo kwa kipindi cha miezi sita (awali ilikuwa miaka miwili) na kuendelea na ambao mnafanya tendo la ndoa kama mume na mke, kusheria anatambulika kama mke hata kama hamjafunga ndoa, hivyo ni lazima muachane kisheria.


Mkuu..darasa limepita ila naomba tusahihishe kidogo.... unless unazungumzia sheria ya nchi nyingine... ya Tanzania haiko kama ilivyoelezewa hapo juu na hadi sasa kuna debates kali kujaribu kusukuma marekebisho ya LMA 1971- ila bado haijatokea.

Sheria ya Ndoa ya Tanzania ( Law of Marriage Act no.5 of 1971 - kuna ndoa za kufikirika - sijui kama ni kiswahili sanifu.. for Presumption of Marriage. Hii ni kama mwanamke na mwanaume wameishi kwa miaka miwili au zaidi.. katika mazingira ya kuifanya jamii iamini kuwa wao ni mke na mume basi there will be a rebuttable presumption that the couple are husband and wife.

Endapo basi kutatokea hali ya kuachana basi wana haki kudai kwa mfano walichochuma pamoja etc.Lengo la hii presumption hasa ni kuzuia watu wasi take advantage ya wengine kwa kuwafanya waamini kuwa wana mahusiano ya kindoa ilhali kuna utapeli.Ikitokea mmoja anataka kufunga ndoa mfano kanisani - maadam kanisa linakataza kuishi kinyumba bila ndoa basi mwenye kutaka kufunga ndoa hatakaliwa kufunga ndoa na mtu mwingine maana kuishi kinyumba siyo ndoa kufuatana na sheria za kanisa. Hali hii ilishawapata watu wengi hasa waliokuwa wanaishi kwenye mitala kienyeji au kimila..wakati wakristo hutambua ndoa ya mke mmoja tu.
Nimeona nichangie kwa kuweka sawa msimamo wa kisheria.
Asanteni.
 
Mkuu..darasa limepita ila naomba tusahihishe kidogo.... unless unazungumzia sheria ya nchi nyingine... ya Tanzania haiko kama ilivyoelezewa hapo juu na hadi sasa kuna debates kali kujaribu kusukuma marekebisho ya LMA 1971- ila bado haijatokea.

Sheria ya Ndoa ya Tanzania ( Law of Marriage Act no.5 of 1971 - kuna ndoa za kufikirika - sijui kama ni kiswahili sanifu.. for Presumption of Marriage. Hii ni kama mwanamke na mwanaume wameishi kwa miaka miwili au zaidi.. katika mazingira ya kuifanya jamii iamini kuwa wao ni mke na mume basi there will be a rebuttable presumption that the couple are husband and wife.

Endapo basi kutatokea hali ya kuachana basi wana haki kudai kwa mfano walichochuma pamoja etc.Lengo la hii presumption hasa ni kuzuia watu wasi take advantage ya wengine kwa kuwafanya waamini kuwa wana mahusiano ya kindoa ilhali kuna utapeli.Ikitokea mmoja anataka kufunga ndoa mfano kanisani - maadam kanisa linakataza kuishi kinyumba bila ndoa basi mwenye kutaka kufunga ndoa hatakaliwa kufunga ndoa na mtu mwingine maana kuishi kinyumba siyo ndoa kufuatana na sheria za kanisa. Hali hii ilishawapata watu wengi hasa waliokuwa wanaishi kwenye mitala kienyeji au kimila..wakati wakristo hutambua ndoa ya mtu mke tu.
Nimeona nichangie kwa kuweka sawa msimamo wa kisheria.
Asanteni.

na kwa case hii mi sioni presumption ya hiyo ndoa wala promise to marry
bado namuona muoaji ana haki ya kuendelea na mipango yake na afunge ndoa yake..
labda kama kuna point tutamis toka upande wa pili....(dada aliyezaa na kijana huyu)

Vinginevyo asante WOS kwa kutuweka sawa kwenye sheria No 5 ya 1971
 
Back
Top Bottom