Mtoto anayeungua nguo bila kujiona atua Dar

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
CHRISTINA Mjema (12) kutoka mji mdogo wa Kabuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, ambaye nguo zake zimekuwa zikiungua kwa moto bila ya yeye kuungua amefikishwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika Kanisa la House of Prayer, lililopo eneo la Boko Magengeni alipo Christina, ambapo alionekana akiwa mwenye furaha pamoja na mama yake, Calister Massawe.
Akizungumza, Mwanjilisti wa kanisa hilo, Vera Nzowa alisema baada ya kusoma gazeti la Mwananchi Jumamosi toleo la Februari 16 kuhusu mateso aliyokuwa akiyapata binti huyo, uongozi wa kanisa hilo uliamua kuwatuma watumishi wake kwenda kumchukua mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kabuku mjini Handeni.
“Jumatano iliyopita niliongoza wenzangu kwenda katika eneo la Kabuku ili kumtafuta mtoto huyo, ambaye alikuwa katika mateso makubwa,” alisema.
Nzowa alisema kuwa alipofika katika nyumba hiyo alikutana na mama wa mtoto huyo na kumweleza nia ya kanisa hilo, ambapo kutokana na shida alizokuwa akizipata alikubali.
“Tulikwenda polisi kwa ajili ya kutoa taarifa za kuondoka na mama na mtoto huyo nao walikubali kutokana na matatizo, ambayo wamekuwa wakishuhudia yakimpata mtoto huyo,” alisema.
Alisema baada ya kukabidhiwa na polisi na viongozi wa kijiji hicho kwa ajili ya kuondoka naye, walifanya maombi na kumpaka mafuta ya baraka ili kuzuia moto huo usitokee wakati wakisafiri.
Alisema kuwa walisafiri salama hadi katika kanisa hilo na kufanya maombi, ikiwamo mkesha maalumu, ambao ulifanyika usiku wa Alhamisi iliyopita.
“Tangu amefika kanisani hapa tatizo la nguo za mtoto huyo kuwaka moto halijatokea tena, tuna imani hali ile haitajitokeza tena,” alisema Mwinjilisti Nzowa.
Alisema wamebaini kwamba mtoto huyo amekuwa akiteswa kwa nguvu za giza na ushirikina.
“Hapa wamefika mahali pake, tatizo hili haliwezi kujirudia,” alisema.
Ingawa hakusema lini ataruhusiwa kurudi nyumbani Kabuku, lakini alisema kuna mikesha kadhaa imeandaliwa kwa ajili ya kuendelea kumwombea mtoto huyo.

by: www.mwananchi.co.tz
 
Mungu nnaemjua Mimi angesolve hilo Tatizo huko huko Kabuku.Sasa mmumpake mafuta ya baraka (temporary ili aweze safiri bila kuungua) Ili aje Dar kwa Maombi?...Ee Mungu utujalie macho ya Kiroho tuweze tambua mbwa mwitu waliovaa Ngozi ya Kondoo.
 
Huna haja ya kuhangaika na imani ya mtu...mwache anayeamini kwa dini yake aendelee kuamini akitakacho
 
kama ni hadithi ya kweli ,inayomuhusisha binti huyo na mateso anayopata na hao waumini wa kanisa hilo wanaouwezo wa kumuondolea kadhia hiyo kwa kumshirikisha MUNGU basi nami naungana nao ktk maombi shetani ashindwe.
 
Ya nn kuita waandishi habari si wangemwombea tu kimyakimya huko handen
 
Yaani huo moto unapeleka shida juu ya shida. Ungeliwaandama mafisadi wa nchi hii ingelikuwa pouwa sana.

Moto kwa Jina la Mungu anayeishi milele uzimike milele ktk maisha ya huyo binti; na nuru ya Mungu akammwangaziye huyo binti; maisha yako yakawe ya kheri uwasaidiye wazazi; ndg; wanakijiji na watz; Amen
 
Mungu nnaemjua Mimi angesolve hilo Tatizo huko huko Kabuku.Sasa mmumpake mafuta ya baraka (temporary ili aweze safiri bila kuungua) Ili aje Dar kwa Maombi?...Ee Mungu utujalie macho ya Kiroho tuweze tambua mbwa mwitu waliovaa Ngozi ya Kondoo.
Kwani Mungu wako ni Mungu wako wao?
 
Back
Top Bottom