Dar: Mlinzi wa Kanisa anayetuhumiwa kumlawiti Mtoto Muimba kwaya kwenye vyoo vya Parokia apandishwa kizimbani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mtuhumiwa Baraka Benedicto ambaye kabla ya kutiwa mbaroni alikuwa mlinzi katika Kanisa Katoliki la Sinza, Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi-Sinza, amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka moja la kumuingilia mtoto kinyume na maumbile.

Shtaka hilo limesomwa na Wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemarila ikielezwa kuwa mtuhumiwa anadaiwa kutenda tukio hilo Februari 3, 2024, mtuhumiwa amekana shtaka hilo.

Kufuatia hatua hiyo Mahakama imepanga kusikiliza tena shauri hilo Namba CC.5866, Jumatatu Machi 18, 2024 Saa tatu asubuhi ambapo mtuhumiwa amepelekwa rumande Segerea.

Baraka Benedicto anadaiwa kumuingilia mtoto wa kiume anayesoma Darasa la Tano katika moja ya Shule iliyopo Sinza, Dar, kinyume na maumbile "ulawiti" katika vyoo vya Parokia Bikira Maria Mama mwokozi - Sinza, ambapo awali ilidaiwa kuwa alikuwa nje kwa dhamana.

Hatua ya kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa umefanyika siku moja baada JamiiForums kuripoti madai hayo ambayo yaliibuliwa na mdau kwenye jukwaa huru la maoni na mijadala.

TUMEMUONDOA KAZINI MLINZI ANAYETUHUMIWA KUMLAWITI MWANAFUNZI.jpg
Soma:
-Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie

- Tukio la Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kudaiwa kumlawiti Mwanafunzi, Padri asimulia kilichotokea
 
Kuna mashaka makubwa kwenye shauri hili mbona hatuoni ripoti ya DNA kuonesha kwamba hizo sphincter muscles za huyo mwanafunzi zimetanuliwa na mlinzi baraka?! What if huyo mwanafunzi anayedaiwa kutokuwa na uwezo wa kujieleza vizuri huwa analiwa siku zote tukizingatia kuwa tabia hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwenye nyumba hizi za ibada hasahasa kwenye makanisa ya mlengo wa hili kanisa?

Baraka aweke wakili kwenye kesi hii vinginevyo watamtoa kafara!
 
Uovu ni uovu bila kujali Nani anafanya, awe mtu wa kawaida, au mwenye dhamana fulani eneo fulani iwe Kanisa, masikiti au serikalini, mtu ahukumiwe kwa makosa yake bila kuhusishwa na Imani au wadhifa anaoutumikia, na kama alitenda kosa kwa kutumia hiyo Kofia bado kosa ni la kwake.
 
Ile kesi ya yule teacher bishoo ilifikia wapi ? Naye alikuwa na tuhuma za kulawiti
 
Back
Top Bottom