Mtikila kufungwa jela leo?

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumatatu, Agosti 27, 2012 06:33 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, anatarajia kuhukumiwa leo mahakamani. Mtikila atahukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam, kutokana na kesi inayomkabili ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba anataka kuuangamiza Ukristo.

Hukumu hiyo itatolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi, Illivin Mugeta anayeisikiliza.

Mchungaji Mtikila alifunga ushahidi baada ya kutetewa na mashahidi wawili badala ya kumi alioahidi kuwafikisha mahakamani hapo.

“Mheshimiwa, nafunga ushahidi, ilikuwa nilete mashahidi 10, lakini wawili wanatosha kwa sababu wengine walikuwa maaskofu kutoka Mwanza ambao naamini wangekuja kueleza kile kile nilichoeleza.

“Nahofia kupoteza fedha za Serikali kwa kuwaleta mashahidi hao, kwani nao hawana kitu tofauti na mashahidi wengine,” alidai Mtikila.

Hakimu Mugeta alisema uamuzi wa Mtikila ni mzuri, asipoteze fedha za umma kama anaamini hivyo atasoma hukumu leo.

Mtikila ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi, alidai kuwa, kesi hiyo ilifunguliwa kutokana na chuki zilizokuwapo kati yake na mchungaji mwenzake, lakini kwa upande wa Rais Kikwete hakumshitaki pamoja na kwamba alimpa nakala ya waraka huo unaodaiwa wa uchochezi.

Shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Mpoki Bukuku kutoka Gazeti la Mwananchi, alidai mahakamani hapo kwamba, walichapisha habari yenye kichwa cha habari ‘Mtikila apiga kampeni kanisani kumpinga Kikwete’.

Pia alidai kwamba, gazeti hilo liliandika Mtikila achunguzwa na Polisi kwa kumwaga sumu, Rais Kikwete asichaguliwe mwaka 2010 na kuongeza kuwa habari hiyo iliripoti kilichotokea Mwanza na ilikuwa ya kweli kwa sababu kati ya polisi na Mtikila, hakuna aliyekanusha.

Alidai habari hiyo, ilikuwa ikielezea mafundisho waliyokuwa wakitoa viongozi wa dini katika kongamano.

Mtikila, anadaiwa Aprili, 2010 mjini Dar es Salaam, alisambaza waraka anaodai wa kuunusuru Ukristo wenye lengo la kuangamizwa na Jihad ya Rais Jakaya Kikwete na kwamba Wakristo wajitoe muhanga kukomesha ugaidi.

Alidai waraka uliosambazwa, alisaini akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuunusuru Ukristo na walichapa nakala 100,000, lakini aligoma kutaja mahali walipochapishia nakala hizo.

Maelezo yote hayo yalitolewa mahakamani kama kielelezo na SSP, Ibeleze Mrema aliyemuhoji Mtikila Aprili 14, 2010 na alipotakiwa kueleza chochote kuhusu kielelezo hicho, mshitakiwa alisema hana swali na akakubali kipokelewe na mahakama.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imehairisha kutoa hukumu ya kesi ya mtikila hadi septemba 6 mwaka huu. Hakimu alikuwa na shughuli nyingine muhimu.
 
Mtikila ajiweke tayari kufungwa. Lakini alishafungwa hivyo anarudi home
 
[h=2][/h]JUMATATU, AGOSTI 27, 2012 06:33 NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, anatarajia kuhukumiwa leo mahakamani. Mtikila atahukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam, kutokana na kesi inayomkabili ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba anataka kuuangamiza Ukristo.

Hukumu hiyo itatolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi, Illivin Mugeta anayeisikiliza.

Mchungaji Mtikila alifunga ushahidi baada ya kutetewa na mashahidi wawili badala ya kumi alioahidi kuwafikisha mahakamani hapo.

“Mheshimiwa, nafunga ushahidi, ilikuwa nilete mashahidi 10, lakini wawili wanatosha kwa sababu wengine walikuwa maaskofu kutoka Mwanza ambao naamini wangekuja kueleza kile kile nilichoeleza.

“Nahofia kupoteza fedha za Serikali kwa kuwaleta mashahidi hao, kwani nao hawana kitu tofauti na mashahidi wengine,” alidai Mtikila.

Hakimu Mugeta alisema uamuzi wa Mtikila ni mzuri, asipoteze fedha za umma kama anaamini hivyo atasoma hukumu leo.

Mtikila ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi, alidai kuwa, kesi hiyo ilifunguliwa kutokana na chuki zilizokuwapo kati yake na mchungaji mwenzake, lakini kwa upande wa Rais Kikwete hakumshitaki pamoja na kwamba alimpa nakala ya waraka huo unaodaiwa wa uchochezi.

Shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Mpoki Bukuku kutoka Gazeti la Mwananchi, alidai mahakamani hapo kwamba, walichapisha habari yenye kichwa cha habari ‘Mtikila apiga kampeni kanisani kumpinga Kikwete’.

Pia alidai kwamba, gazeti hilo liliandika Mtikila achunguzwa na Polisi kwa kumwaga sumu, Rais Kikwete asichaguliwe mwaka 2010 na kuongeza kuwa habari hiyo iliripoti kilichotokea Mwanza na ilikuwa ya kweli kwa sababu kati ya polisi na Mtikila, hakuna aliyekanusha.

Alidai habari hiyo, ilikuwa ikielezea mafundisho waliyokuwa wakitoa viongozi wa dini katika kongamano.

Mtikila, anadaiwa Aprili, 2010 mjini Dar es Salaam, alisambaza waraka anaodai wa kuunusuru Ukristo wenye lengo la kuangamizwa na Jihad ya Rais Jakaya Kikwete na kwamba Wakristo wajitoe muhanga kukomesha ugaidi.

Alidai waraka uliosambazwa, alisaini akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuunusuru Ukristo na walichapa nakala 100,000, lakini aligoma kutaja mahali walipochapishia nakala hizo.

Maelezo yote hayo yalitolewa mahakamani kama kielelezo na SSP, Ibeleze Mrema aliyemuhoji Mtikila Aprili 14, 2010 na alipotakiwa kueleza chochote kuhusu kielelezo hicho, mshitakiwa alisema hana swali na akakubali kipokelewe na mahakama.

Huyu Mchungaji anajua kona zote za jela... Nikiwa Mtoto yeye anatembelea Jela sasa Mimi Mzee bado

Yeye anatembelea Jela... Sijui kama ana Meno yote Mdomoni???
 
Mtikila kweli kiboko si juzi tu ametishia kufungua kesi ya kushikwa makalio na askofu Mokiwa? Kweli hiki kichwa kina mamabo!
 
itasomwa september 6 baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo ndg IIvin Mugeta kuwa na shughuli nyingine muhimu na kushindwa kufika mahakamani leo
 
Huyu mtikila atakuwa hamnazo..

we muone chizi mwenzio maisha yanakwenda

ameishtaki Serikali mara 43

mara 41 ameshinda

mara 1 ameshindwa

na hii 1 inaendelea

cjiwi nani mgonjwa kati

ya Mtikila na Serikaki yetu
 
[h=2][/h] Jumanne, Agosti 28, 2012 05:49 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

mtikila.jpg
Mchungaji Christopher Mtikila

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeahirisha kusoma hukumu dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila hadi Septemba 6, mwaka huu.
Hukumu hiyo iliahirishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi, Frank Mosha, baada ya Hakimu Mkuu Mkazi, Illivin Mugeta, anayeisikiliza, kutokuwapo mahakamani.

“Kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya hukumu, hakimu anayesikiliza kesi hii amepata udhuru, hivyo itasomwa Septemba 6 mwaka huu,” alisema Hakimu Mosha wakati akiahirisha shauri hilo.

Mtikila anakabiliwa na mashitaka ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba anataka kuuangamiza Ukristo.

Mshitakiwa alifunga ushahidi kwa kuwa na mashahidi wawili wa utetezi, akihofia kupoteza fedha za Serikali kwa kuwaleta mashahidi wengi ambao hawana kitu tofauti na mashahidi wengine waliokuwa wamewasilisha ushahidi wao mahakamani hapo.

Mtikila, anadaiwa kwamba, Aprili, 2010 jijini Dar es Salaam, alisambaza waraka aliokuwa akidai ni wa kuunusuru Ukristo wenye lengo la kuangamizwa na Jihad ya Rais Jakaya Kikwete na kwamba Wakristo wajitoe muhanga kukomesha ugaidi.

“Kikwete anaangamiza Ukristo, amekuwa jasiri wa kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai Mtikila katika waraka wake huo.

Alidai waraka uliosambazwa alisaini akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuunusuru Ukristo na walichapisha nakala 100,000, lakini aligoma kutaja mahali walipochapishia nakala hizo.

Maelezo yote hayo yalitolewa mahakamani kama kielelezo na SSP, Ibeleze Mrema aliyemuhoji Mtikila Aprili 14, 2010 na alipotakiwa kueleza chochote kuhusu kielelezo hicho, mshitakiwa alisema hana swali na akakubali kipokelewe na mahakama.

Hata hivyo, akizungumza nje ya mahakama hiyo, Mtikila alisema yuko katika mikakati ya kuandaa waraka mzito kuliko aliouandaa mwanzo na kuwa chanzo cha yeye kufikishwa mahakamani hapo.

Alisema waraka huo utagusia rais anayestahili kuiongoza nchi kwa masilahi ya Watanzania.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
udini utalipeleka Taifa letu kubaya, watu wanapenda dini zao na kuona za wengine siyo dini! Wa Tanzania tusiwe hivyo, tufanye kazi mbona wazungu wanaishi kwa amani kuliko wengine? Ni kwa sababu wanapedana na kutokuwa na waumini wa dini wengi wa dini zinazochochea chuki!
 
Back
Top Bottom