Mtikila ampa siku 7 Ridhiwan aende mahakamani

Nchi inaelekea kuzuri,huyu anaibuka na tuhuma,anapewa siku saba atoe ushahidi...kabla ya siku saba anaibuka aliyetuhumiwa na kuongeza siku saba kwa aliyemtuhumu atangulie mahakamani...ngoja tuangalie picha
 
Kuwa mwanasheria hakumaanishi unajua kila kitu. Hakumaanishi unazijua sheria zote. Kwanza hakuna mtu anayezijua sheria zote. Pia hakumaanishi unaweza kushinda kesi yoyote ile iliyoko mbele yako.

Ushindi wa kesi unategemeana na mambo mengi sana na si cheti cha kuhitimu kozi ya sheria chuo kikuu na hatimaye kujiita au kuitwa mwanasheria.
In all honesty lawyers are really not what they are cracked up to be.


Mganga hajigangi mwenyewe
 
Nina wasi wasi km shahada yake km kaumiza kichwa as tunavyoona wenzie wa LLB wanaumia...perhaps Maprof zetu njaa waliamua kumkosha kijana ili awakumbuke kwa "baba" na matokeo yake ndo haya tunayoona sasa...
 
Acha upunga wewe! Kwanini unaleta udini? Madrasa inaingiliana vp na Ridhiwan? Ucpende kuingiza wizi wa m2 na dini,who told u kwamba uislamu unaenda na wizi?

Beira, jitahidi kusoma sentensi na kuelewa maudhui yake, elewa maana ya maneno ukisharidhika ndipo utoe tuhuma kwa mhusika kwamba ameongelea udini, vinginevyo tutakuona nawe hukuhitimu vizuri shuleni bali ulikuwa mhudhuriaji tu darasani bila kumwelewa mhadhiri na leo unajisikia msomi ukifanya mambo kinyume cha tunavyotazamani kwa taaluma yako.
 
Mbona Mh Lissu amesimamia kesi yake na kashinda.TUNATAKA RIDHIWAN NAYE ASIMAMIE MANENO YAKE HADI MWISHO TENA TUNAMTAFUTA SANA KONA YEYOTE TUKIMKUTA TUNAYE.MWIZI MKUBWA.

Kila kesi iko tofauti na kila kesi ina facts zake. Tundu Lissu kujitetea na kushinda si jambo la ajabu kwani wapo watu binafsi wasio na legal training yoyote ile waliosimama kizimbani peke yao bila msaada wa mwanasheria na wakashinda kesi.

Costa Mahalu ana kesi mahakamani sasa hivi. Huyu ni profesa wa sheria. Kafundisha chuo kikuu cha Dar es salaam na kwingineko. Lakini sasa hivi anawakilishwa na Mabere Marando. Mahalu anamzidi Marando kielimu. Mahalu ana sifa zote za kuwa mwalimu wa Marando. Sasa jiulize kwa nini Mahalu hajajitetea mwenyewe na kaenda kununua huduma za mwanasheria ambaye anamzidi kielimu.

Ridhiwani ana kila haki ya kuamua jinsi atakavyojiwakilisha katika hiyo kesi kama itafunguliwa mahakamani. Anaweza akaajiri wakili au akajiwakilisha mwenyewe.
 
tehe tehe tehe, kitabu cha mama rwakatare kimeshatoka? Mtikila huwa namuona kama ZE KOMEDI nisameheni kama nimesema vibaya. Anaropoka yanamtokea pagumu ila huwa anashinda majaribu yote na kuwa huru.

Glory be to GOD.
 
Nawahakikishia kuwa ngoma hii itaisha bila mshindi kujulikana!!!, si kesho tu mwezi june tutakuwa tumesahau na kuibuka na kitu kingine ..............
 
Allahaula!!! Hili li serikali ni balaa tupu. Badala ya kushughulika na mafisadi sasa tunasikia wameanza kuwakaba makoo maaskofu. TAKUKURU fuatilieni mafisadi hawa wanaotajwa kila kukicha. Mmejikausha. Yaone....
 
Huyu dogo anautani na hivi vichwa inaonesha kaigilia dirishani sasa kutoka kanashindwa kwani dirisha jamaa washa piga nondo kapo ndani hakajua cha kufanya weeeeeeeeeee!!!! Silaa + mti killer =silaamtikiller sasa embu nambie katapona kweli hako kamjamaaa kama sio kamesha banwa mbavu hapo majina yenyewe tu sheria tosha... Kaache kwanza kanataka kujaribu ngoma ya wakubwa hako katoto katavuja jasho sasasasa katabebwa kwenye machela.
 
Sunday, 29 May 2011

mtikila.jpg

Mchungaji Christopher Mtikila

Peter Saramba, Arusha

LICHA ya mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani kuwaandikia barua ya kusudio la siku 10 kuwafikisha mahakamani Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameambiwa aende huko mahakamani.

Katika kusudio lake Ridhiwani amedai kuwa endapo watashindwa kumwomba radhi na kumlipa Sh2 bilioni atakwenda mahakamani.Katika kusudio hilo, Ridhiwani amewataka wanasiasa hao wamwombe radhi na kumlipa fidia hiyo ndani ya siku kumi kuanzia Mei 13, kwa madai waliyoyatoa hadharani kuwa yeye ni bilionea aliyetajirika kifisadi.


Katika kusudio hilo, Ridhiwani pia amehusisha gazeti la Tanzania Daima ambalo amedai limechangia kumchafua kwa kuripoti madai ya wanasiasa hao dhidi yake.


"Tumeelekezwa na mteja wetu kuwataka wote kwa pamoja kukanusha na kusahihisha tuhuma zote na kuchapisha habari hiyo ya kuomba radhi kwa uzito na herufi kubwa (bold print) katika kurasa za mbele wa gazeti hilo (Tanzania Daima) kwa siku tatu mfululizo hadi Mei 23, 2011," alieleza wakili Sam Mapande wa Law Associates, anayemwakilisha Ridhiwani.Wakili huyo aliendelea, "Pia, wote kwa pamoja mnatakiwa kulipa fidia ya Sh2 bilioni kwa madhara ya jumla aliyopata mteja wetu."


Barua hiyo ya kurasa sita ambayo Mwananchi ina nakala yake, imetaja baadhi ya maneno yaliyoandikwa kwenye matoleo mawili ya gazeti la Tanzania Daima yakimkariri Dk Slaa na Mchungaji Mtikila, wakimhusisha pia Rais Jakaya Kikwete na mwanaye (Ridhwani) na watu wengine walio karibu yake na matukio ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na ofisi ya umma. Kwa mujibu wa Ridhiwani, madai hayo yamemchafulia jina, kumdhalilisha, kumshushia hadhi na heshima yake katika jamii inayomzunguka.


Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda amekiri kupokea barua hiyo, lakini akasema hawezi kusema chochote kwa jambo ambalo ni la kisheria.

"Kwa kuwa bado hatujafikishwa mahakamani, siwezi kusema tumejiunga vipi. Tunasubiri tufikishwe mahakamani kwanza," alisema Kibanda.

Mchungaji Christopher Mtikila amemtaka mtoto huyo wa rais kwenda mahakamani haraka akidai kuwa hana shaka kwa kuwa ana ushahidi mzito kuthibitisha madai yake.Mtikila aliwaambia waandishi wa habari mjini Arusha jana kuwa, kesi hiyo itakuwa ni ukombozi kwa taifa kwa sababu itampa yeye na mwenzake, Dk Slaa muda wa kueleza kile


alichokiita madudu yanayofanywa na mtoto huyo wa rais.


Mtikila aliendelea kudai kuwa Ridhwani anatumia vibaya ofisi na madaraka ya baba yake (Rais Kikwete) kujilimbikizia mali kinyume cha sheria.

"Kitendo cha Ridhwani kutaka aombwe radhi na fidia ni njia na ngazi muhimu itakayosaidia mambo mengi yaliyojificha kuwekwa hadharani," alisema Mtikila na kuongeza:"Tutatumia sheria zilizopo kuwabana wote ambao majina yao yameandikishwa kwenye mali za vigogo nchini waeleze walivyopata mali hizo na hapo ndipo watakapowataja wahusika halisi," alisema Mtikila.


Kiongozi huyo wa DP aliendelea kudai kuwa viongozi wengi nchini wamejilimbikizia mali kupitia wizi na ufisadi, wakitumia nafasi zao za umma huku wakiandikisha majina ya watu wengine kwenye mali hizo kuficha umiliki wao.


Alidai kuwa kesi anayotaka kuifungua Ridhiwani itaibua mambo mengi kwani walioandikishwa majina kwenye mali hizo, watawataja wamiliki halisi badala ya kufungwa jela kwa kumiliki mali inayodhaniwa kuwa ya wizi au kupatikana isivyo halali.


Kwa upande wake, Dk Slaa jana hakupatikana kuzungumzia kusudio hilo la Ridhiwani kutokana na simu yake ya kiganjani kutopatikana kwa siku nzima.


Jana, Ridhiwani alipotakiwa kueleza nini kinafuata baada ya muda aliotoa kuisha alijibu kwa ufupi kuwa asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa ni jambo la kisheria na kwamba sheria ina kanuni zake.


"Ndugu yangu, sitaki kuzungumzia hili kwa kuwa sheria ina kanuni zake. Hili litazungumzwa mahakamani."


Dk Slaa na Mtikila walikaririwa mwanzo wa Mei wakisema kuwa mtoto huyo wa rais ana utajiri mkubwa licha ya kumaliza shule miaka ya karibuni huku wakimtuhumu kutumia cheo na madaraka ya baba yake kujitajirisha.


Mtikila: Ridhiwani nenda mahakamani
 
Hali hii ndiyo inafanya baadhi yetu tuamini kila kitu kibaya kinachosemekana kufanywa na JK na wafuasi wake wenye imani kuwa sasa ni zamu yao kula. Hata kina Lowasa, Rostam, Chenge nk walikuwa wepesi kudai wangeenda mahakamani mara tu kashfa za ufisadi wanazohusishwa nazo zilipotajwa na wanasiasa wa upinzani, mwisho wake inaonekana hawana watakalopata mahakamani zaidi ya aibu hivyo wameamua kukaa kimya huku wakiendeleza njama na mbinu zao chafu nje ya mahakama.
Naamini huyu mwana wa Mfalme naye ni yaleyale. Wanatamani kuonekana matajiri wakubwa kwa kuwapora wanyonge. Yana mwisho mambo haya na mwisho wake utakuwa mbaya kiasi kwamba hakuna mjukuu wa baba yake atakayetamani kuiba tena katika nchi hii.
Kwako Rizwan: Ibeni weee hadi mtakapochoka lakini angalieni sana njia zenu maana siku tutakayoamua kudai nchi yetu. Septemba 11 itawaangukia na familia zenu bila kujali mtakuwa wapi duniani.
 
Mh,hivi huyu jamaa ana hudumu katika kanisa gani?
natamani kweli nije kusikiza mahubiri yake one day
 
zilianza siku saba, leo kumi
kimahesabu anaruka siku 13 na kuongeza siku 3 kwa kila mkwara
kwa mwezi, ngoja nijaribu fasta nione kama zitafika 2015
naona kufikisha 2015 anaitaji mikwara kama 18 hizi
sio mingi sana nadhani hataweza.
weraaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mh,hivi huyu jamaa ana hudumu katika kanisa gani?
natamani kweli nije kusikiza mahubiri yake one day

mkuu wakristo tumesoma bana
hacha dini,
au nikutajie shule zetu
angalizo maleria sugu kafunguliwa ukianza dini tu hatakua hatoki kwenye hii thread
 
zilianza siku saba, leo kumi
kimahesabu anaruka siku 13 na kuongeza siku 3 kwa kila mkwara
kwa mwezi, ngoja nijaribu fasta nione kama zitafika 2015
naona kufikisha 2015 anaitaji mikwara kama 18 hizi
sio mingi sana nadhani hataweza.
weraaaaaaaaaaaaaaaa

Porojo za kisiasa au uelewa mdogo wa sheria? Mtu anapokupa siku kadhaa ufanye kitu fulani ama sivyo anakwenda mahakamani, ana maana siku hizo exactly zinapoisha au baada ya siku hizo kuisha anaanza mchakato wa kisheria? Mchakato wa kisheria Mkuu huchukua siku au wiki kadhaa, hukurupuki tu na kwenda mahakamani kufurahisha vilaza wa JF.
 
zilianza siku saba, leo kumi
kimahesabu anaruka siku 13 na kuongeza siku 3 kwa kila mkwara
kwa mwezi, ngoja nijaribu fasta nione kama zitafika 2015
naona kufikisha 2015 anaitaji mikwara kama 18 hizi
sio mingi sana nadhani hataweza.
weraaaaaaaaaaaaaaaa

Nlisoma kitabu kinachoitwa KUSADIKIKA " mchwa akitaka kufa hugeuka kumbikumbi kisha huruka mwisho wake hupotea na kufa" Mwacheni afe kama hawajui kina SLAA na MKITILA ktk nchi hii basi ILA atafungua mlango wa kutujuza zaidi UFISADI wake ulinyo MTU MZIMA HATISHIWI NYAUU UUUUU !!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom