Mtikila ampa siku 7 Ridhiwan aende mahakamani

Tena kwa kuwa yeye RIZ1 ni Mwanasheria asiajili wanasheria wengine ajisimamie au ashirikiane na Masha,wanaweza kushinda.

Kuwa mwanasheria hakumaanishi unajua kila kitu. Hakumaanishi unazijua sheria zote. Kwanza hakuna mtu anayezijua sheria zote. Pia hakumaanishi unaweza kushinda kesi yoyote ile iliyoko mbele yako.

Ushindi wa kesi unategemeana na mambo mengi sana na si cheti cha kuhitimu kozi ya sheria chuo kikuu na hatimaye kujiita au kuitwa mwanasheria.

In all honesty lawyers are really not what they are cracked up to be.
 
Mimi naamini hakuna kitu hapo,Bongo bana siasa za taarab tu.

Siku saba zitakuja zitapita,wanasiasa wote ni kitu kimoja wanakula meza moja na wadangayikwa wataendelea kudanganywa tu.
 
MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amemtaka mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, kwenda mahakamani ndani ya siku saba alizosema vinginevyo atakwenda yeye kushtaki kutokana na utajiri alionao kwani ni kosa la jinai.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mchungaji Mtikila alisema kwa taratibu za kisheria Ridhiwan anapaswa kuwapa kwanza ‘Demand Note Letter’( barua ya kuwataka wamwombe radhi au kufuta kauli zao) yeye na Dk. Willibrod Slaa.

“Ikiwa Ridhiwan hatafanya hivyo nitajipanga kwenda mahakamani kuwaeleza Watanzania namna mtoto huyo alivyo ni bilionea kupindukia kwa kumiliki mali nyingi zikiwemo fedha za Watanzania ambazo ni mabilioni katika akaunti zake, kampuni ya malori 150 na ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha,” alisema Mtikila.

Kwa mujibu wa Mtikila, hawezi kuthibitisha kwa vielelezo aliyoyasema wakati alipokutana na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusu utajiri wa mtoto huyo wa Rais kama hatapelekewa barua hiyo.

“Yawezekana Ridhiwan anazungumza maneno asiyoyafahamu kisheria na yeye tunasikia ni mwanasheria, kama unamtaka mtu akuombe radhi na kama akishindwa utampeleka mahakamani…maneno hayo kisheria huenda na demand note letter, sasa yeye hajatufikishia je tujipeleke? Alihoji Mchungaji Mtikila.

Alieleza kuwa kama kweli Ridhiwan ni mwanasheria na anazifahamu sheria, siku ile aliyozungumza na waandishi wa habari angekuwa na barua hizo mkononi tayari kwa kuwapelekea na kusubiri matokeo yake.

“Sasa naamini kwamba ni kweli Ridhiwan hajui sheria na kama angezifahamu, ningeshapata barua yangu mapema kwa kuwa anayafahamu makao makuu ya DP pale Ilala Msikitini na kama hazifahamu ofisi hizo angeniletea nyumbani kwangu Mikocheni B tuko jirani.”

Juzi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, naye alimtaka Ridhiwan kwenda mahakamani haraka kwa kuwa yaliyozungumzwa na kinywa chake yana ukweli.

Baada ya tamko hilo la Dk. Slaa siku chache baadaye Ridhiwan alizungumza na waandishi wa habari na kutoa siku saba kwa Dk. Slaa na Mtikila akiwataka kukanusha tuhuma walizomtupia au kuthibitisha kwa vielelezo, vinginevyo angewaburuza mahakamani kwa kumchafua yeye na familia yake.

Mwanzoni mwa wiki hii Ridhiwan aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona akiendesha magari ya bei ghali na wazipuuze kauli zinazotolewa na wanasiasa hao wa upinzani kwamba ni za uongo.

Ridhiwan alikaririwa na vyombo vya habri akisema, “Hapa mjini jamani tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake.”
Alisema yeye si bilionea kama wanavyodai wanasiasa hao, na kutaja mali zake kuwa ni shamba la ekari 1.5 lililoko Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti katika benki za Stanbic na NBC na CRDB.

Tanzania Daima
 
Huyu mzee alimention kikosi cha firsu eleven pale mwembe uji,kumbe kuna ambao wako bench tena watoto wao,kumbe tz tuna wachezaji wakar zaid ya mesi.hii mech main character liz1 obviouz atambwela kotini.
 
Huyu kijana wasimwache atazoe vibaya. Wakubwa zake wanatuibia na yeye anaiba af anakuja kujikosha wampeleke kabsa, astuletee zile za Misri familia inamiliki nchi.
 
Kahitimu na tena ana daraja la uwakili, :bange:
 
Kuwa mwanasheria hakumaanishi unajua kila kitu. Hakumaanishi unazijua sheria zote. Kwanza hakuna mtu anayezijua sheria zote. Pia hakumaanishi unaweza kushinda kesi yoyote ile iliyoko mbele yako.

Ushindi wa kesi unategemeana na mambo mengi sana na si cheti cha kuhitimu kozi ya sheria chuo kikuu na hatimaye kujiita au kuitwa mwanasheria.

In all honesty lawyers are really not what they are cracked up to be.

Mbona Mh Lissu amesimamia kesi yake na kashinda.TUNATAKA RIDHIWAN NAYE ASIMAMIE MANENO YAKE HADI MWISHO TENA TUNAMTAFUTA SANA KONA YEYOTE TUKIMKUTA TUNAYE.MWIZI MKUBWA.
 
Kiherehere chake cha kupenda kuuza sura kwenye vyombo vya habari kama dingi. Atamkoma mtikila hapa ni lazima mtikila alambe kitu alimtega akaingia alidhani atafika kingi kumba hakujua kuwa mtikila anaishi kimjini zaidi yake. He will be forced to compromise with him. Hapa mtikila lazima ale sahani moja naye labda kama ana kesi nyingine ambayo ameshatega na inamlipa.
 
Acha upunga wewe! Kwanini unaleta udini? Madrasa inaingiliana vp na Ridhiwan? Ucpende kuingiza wizi wa m2 na dini,who told u kwamba uislamu unaenda na wizi?

Wewe acha kukurupuka na kutuhumu wenzio udini bila kusoma kwa makini kilichoandikwa.
Amesema "madarasa" siyo "madrasa". Soma vizuri.
 
MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amemtaka mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, kwenda mahakamani ndani ya siku saba alizosema vinginevyo atakwenda yeye kushtaki kutokana na utajiri alionao kwani ni kosa la jinai.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mchungaji Mtikila alisema kwa taratibu za kisheria Ridhiwan anapaswa kuwapa kwanza ‘Demand Note Letter'( barua ya kuwataka wamwombe radhi au kufuta kauli zao) yeye na Dk. Willibrod Slaa.

"Ikiwa Ridhiwan hatafanya hivyo nitajipanga kwenda mahakamani kuwaeleza Watanzania namna mtoto huyo alivyo ni bilionea kupindukia kwa kumiliki mali nyingi zikiwemo fedha za Watanzania ambazo ni mabilioni katika akaunti zake, kampuni ya malori 150 na ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha," alisema Mtikila.

Kwa mujibu wa Mtikila, hawezi kuthibitisha kwa vielelezo aliyoyasema wakati alipokutana na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusu utajiri wa mtoto huyo wa Rais kama hatapelekewa barua hiyo.

"Yawezekana Ridhiwan anazungumza maneno asiyoyafahamu kisheria na yeye tunasikia ni mwanasheria, kama unamtaka mtu akuombe radhi na kama akishindwa utampeleka mahakamani…maneno hayo kisheria huenda na demand note letter, sasa yeye hajatufikishia je tujipeleke? Alihoji Mchungaji Mtikila.

Alieleza kuwa kama kweli Ridhiwan ni mwanasheria na anazifahamu sheria, siku ile aliyozungumza na waandishi wa habari angekuwa na barua hizo mkononi tayari kwa kuwapelekea na kusubiri matokeo yake.

"Sasa naamini kwamba ni kweli Ridhiwan hajui sheria na kama angezifahamu, ningeshapata barua yangu mapema kwa kuwa anayafahamu makao makuu ya DP pale Ilala Msikitini na kama hazifahamu ofisi hizo angeniletea nyumbani kwangu Mikocheni B tuko jirani."

Juzi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, naye alimtaka Ridhiwan kwenda mahakamani haraka kwa kuwa yaliyozungumzwa na kinywa chake yana ukweli.

Baada ya tamko hilo la Dk. Slaa siku chache baadaye Ridhiwan alizungumza na waandishi wa habari na kutoa siku saba kwa Dk. Slaa na Mtikila akiwataka kukanusha tuhuma walizomtupia au kuthibitisha kwa vielelezo, vinginevyo angewaburuza mahakamani kwa kumchafua yeye na familia yake.

Mwanzoni mwa wiki hii Ridhiwan aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona akiendesha magari ya bei ghali na wazipuuze kauli zinazotolewa na wanasiasa hao wa upinzani kwamba ni za uongo.

Ridhiwan alikaririwa na vyombo vya habri akisema, "Hapa mjini jamani tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake."
Alisema yeye si bilionea kama wanavyodai wanasiasa hao, na kutaja mali zake kuwa ni shamba la ekari 1.5 lililoko Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti katika benki za Stanbic na NBC na CRDB.

Tanzania Daima

Sasa ndio tutajua kati ya R1 na Mtikila nani anaishi kimjini kimjini zaidi.
 
Acha upunga wewe! Kwanini unaleta udini? Madrasa inaingiliana vp na Ridhiwan? Ucpende kuingiza wizi wa m2 na dini,who told u kwamba uislamu unaenda na wizi?

pole umepata hasira pasi na sababu!yeye amesema madarasa na sio madrasa!mtu kuhudhuria madarasa bila kuhitimu hiyo ipo so hapo hakuna udini wowote
 
Back
Top Bottom