Mtikila ampa siku 7 Ridhiwan aende mahakamani

Mchungaji Mtikila aliongea na waandishi wa habari juzi(28/5/2011) mjini Arusha akisisitiza kuwa Ridhiwani aendelee na hatua ya kufungua kesi mahakamani, ili yeye na Dr Slaa wapate nafasi nzuri na wanayoisubiri, ya kuweka hadharani aliyoita 'Madudu' ya mtoto huyo wa Rais.

Kwenye picha hii, kilichonifurahisha zaidi ni SIMU ZA MTIKILA!...Je ni bahili, au mkoloni, au SIMU MAANA YAKE MAWASILIANO, na si zaidi ya hapo?...
Simcheki Mtikila , Laa!, ila nilitegemea kwa wadhifa alio nao angekuwa na simu ambayo japo anaweza kusoma e-mail hata akiwa mbali na pc's.

Nawasilisha kwa maoni yenu!
mtikila.jpg
 
I really doubt kwa hapa kwetu 'mzee' kama mtikila anaweza kuwa kizazi cha emails! Watu wengi wa age yake simu ni kwa ajili ya kupiga/kupigiwa na si zaidi ya hapo...hata sms tu zinawapa taabu kweli! Ukichanganya na 'siasa za kichungaji' unaweza kuona ni kwa nini anatumia simu hizo!
 
teh teh simu maana yk mawasiliano , unapiga na kukea lol . Angalau ameongelea nje ya maelezo . Hapa ni cafe au ofisi za udp arusha
 
mbona hata yangu ni kama hiyo ya kwanza na hakuna kinachoharibika? acheni ulimbukeni, mlitaka awe na zigo la blackbery, la nini?
 
Si afadhali ya Mtikila, Mwalimu Nyerere alikataa kabisa!.

Ila kati ya hizo 2, moja inakubali net.

Tena ni afadhali ya Mtikila mara 100 ambaye yuko down to earth na ni mkweli, kuliko waheshimiwa bungeni, wanatumia masimu ya milioni hata mtandaoni hawapo. Watu kibao wana blackbery jina tuu, kwenye interprise hawagusi!.

Kwa hili la simu, namuunga mkono Mtikila, simple and plain ndio the pure truth!.
 
Kwa mtazamo wa kawaida sana huwezi kuchukua TShs. 900,000 kwenye mapato halali ukanunulie simu wakati kuna mambo muhimu kama ada za shule n.k.

Simu alizo nazo zinakidhi mahitaji yake ya mawasiliano, haitaji kuwa na simu ya ghali; BWT mliangalia salio kwenye hizo simu? Maana mtu anaweza kuwa na simu ya TShs. 900,000 lakini salio ni chini ya TShs 500 muda wote
 
Sioni sababu ya kushangaa. kwa kijana kama wewe unaeshinda facebook na jamii forum utamshangaa sana mchungaji. lakini simu ni kwa mawasiliana hiyo email mp3, kamera na mengineyo ni kwa vijana zaidi kama wewe, au wazee wasiokubali kuzeeka i mean mafataki.
 
Anaonyesha jinsi ya kubana matumizi kwa vitendo, Viongozi wetu wanabana matumizi kwa maneno. Nilishawahi kuambiwa kuwa kuliwepo na Mkuu wa Majeshi aliyekuwa anakataa vitu vya anasa, sijui ni kweli au watani zake wanamtania tu.
 
Kwa mtazamo wa kawaida sana huwezi kuchukua TShs. 900,000 kwenye mapato halali ukanunulie simu wakati kuna mambo muhimu kama ada za shule n.k.

Simu alizo nazo zinakidhi mahitaji yake ya mawasiliano, haitaji kuwa na simu ya ghali; BWT mliangalia salio kwenye hizo simu? Maana mtu anaweza kuwa na simu ya TShs. 900,000 lakini salio ni chini ya TShs 500 muda wote

Mkuu,
Hapo kwenye red kweli umetwanga Ikulu!
Kwa kweli nakiri hakuna aliyebahatika kujua salio la simu hizo...!
Lakini mkuu, kwani hata angeonekana anatuma msaidizi kuleta vocha ya alfu 1, ungempa mtazamo wa tofauti na sasa?
 
Mchungaji Mtikila aliongea na waandishi wa habari juzi(28/5/2011) mjini Arusha akisisitiza kuwa Ridhiwani aendelee na hatua ya kufungua kesi mahakamani, ili yeye na Dr Slaa wapate nafasi nzuri na wanayoisubiri, ya kuweka hadharani aliyoita 'Madudu' ya mtoto huyo wa Rais.

Kwenye picha hii, kilichonifurahisha zaidi ni SIMU ZA MTIKILA!...Je ni bahili, au mkoloni, au SIMU MAANA YAKE MAWASILIANO, na si zaidi ya hapo?...
Simcheki Mtikila , Laa!, ila nilitegemea kwa wadhifa alio nao angekuwa na simu ambayo japo anaweza kusoma e-mail hata akiwa mbali na pc's.

Nawasilisha kwa maoni yenu!
View attachment 31106

Your perception is wrong PJ, it is not always that people use phones to read e-mails. Mtikila has always his laptop connected to internet. Why should he bother having such an expensive phone. After all reading and typing mails through phones is not very convenient. I really admire this reverent for his unique lifestyle.
 
Sioni sababu ya kushangaa. kwa kijana kama wewe unaeshinda facebook na jamii forum utamshangaa sana mchungaji. lakini simu ni kwa mawasiliana hiyo email mp3, kamera na mengineyo ni kwa vijana zaidi kama wewe, au wazee wasiokubali kuzeeka i mean mafataki.
Mkuu,
Sielewi unajiamini vp na msisitizo wa kauli hiyo kweye red, maana nina uhakika hatujapata kuonana!...Dont you fear that you may be proved wrong?

BTW, sifahamu analogy kati ya umri wa Mch. Mtikila na Dr Slaa, lakini anyhow wanashabihiana!...Sipendi kueleza zaidi kuhusu DrSlaa na mtandao, maana unajua vyema...Umri si ishu broda kwa aliyedhamiria kwenda na wakati!...Information is always Power, age aint nothing!
 
Jamani pamoja na wadhifa wake yeye ni mlala hoi, hawezi mudu simu za gharama? msamaheni huyo mzee ila kwa kumsaidi mtu yoyote anaweza kujitolea kumnunulia simu ambayo anafikiri mpiganaji huyu itamfaa.
 
Back
Top Bottom