Mtihani wa kidato cha sita ni february 2013

Jul 19, 2012
7
1
katika hali ya kuonesha wamegundua makosa yao,Baraza la mitihani ya taifa NECTA,wameondoa ratiba yao ya mwez mei na kurudisha ya mwez february katika mtandao wao
 
Nchi imeshindwa kuongoza secta ya elimu kila waziri anaengia nakuja na mikakati yake.
 
Sababu za kubadilisha mihula ni zipi, kwa nini mtihani ufanyike mei? Wanafunzi wanahitaji kuandaliwa kiakili, hayo mambo ya kubadilisha mihula bila kuwaandaa hatuoni kama tunawaathiri?

Nani anajali kama yeye watoto wake shule za bongo haziwahusu? Hivi ni mtoto wa nani kati ya watoa maamuzi ambaye ataathirika na mabadiliko haya hatari? Siku hizi hatuna viongozi (wa kutuonyesha njia) waliopo ni watawala. Mtawala si lazima ajihusishe ma matatizo (wenyewe wanaita kero) ya mtawaliwa. Tusione ajabu kuwa kwao elimu yetu imekuwa ghali sana (pengine hata kuwa mwiba mkali) na kwa dhati wamaemua kujaribu ujinga. Ujinga wetu ndiyo mtaji wa watawala hawa.

Kupanga ni kuchagua na ingawa wahenga hawakusema lakini naamini pia kuwa kuchagua ni kupanga. Wanadai kuwa tumewachagua na hivyo tumewapanga wajaribu ujinga kwani elimu yetu kwao ni gharama kubwa.

Huu ni mpango kamambe wa kuimalizia pumzi ya mwisho ya elimu ya Tanzania na kuididimiza kaburini. Maana hata katika jitihada za kawaida tumekuwa nyuma ajabu ukilinganisha na jirani zetu hasa Kenya na Uganda. Sasa wameona kwa nafasi hiyo ya mwisho ni ya juu sana kwa viwango vyao, wanalazimika kuizika kabisa elimu ya Tanzania. "Mungu hadhihakiwi, kwa maana chochote apandacho mtu (nchi, taasisi, nk) ndicho atakachovuna". Kwa maamuzi haya hatuna sababu ya kusubiri mavuno ili tujue tutakachovuna kwani dhahiri yanajulikana na yatakuwa ya kishindo.
 
Facebook-like-button.png
 
Back
Top Bottom