Mtihani mzito sana kwa JK mwezi huu

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Kwa kuwa imekuwa kawaida yake, Rais wetu Jakaya Kikwete, kulihutubia Taifa, kwa njia ya Televisheni na Redio, kila mwisho wa mwezi, kwa lengo la kutolea ufafanuzi masuala mazito yaliyolikumba Taifa katika kipindi cha mwezi mzima.

Natabiri kuwa hotuba ya mwisho wa mwezi huu, inaweza kuwa na wasikilizaji na watazamaji wengi, kuliko hotuba yoyote aliyowahi kuitoa Rais, tokea aina hiyo ya kuwasiliana na wananchi, alipoianza mwaka 2006! Nasema hotuba hiyo inasubiriwa kwa hamu na mamilioni ya wananchi kutokana na matukio makubwa yaliyojitokeza mwezi huu.

Ingawa yapo mambo mengi yaliyotokea, mimi nitayataja mawili ambayo nayaona yametawala vyombo vya habari mwezi huu. Suala la kwanza, ni kuuawa na polisi, kwa mwanahabari wa channel ten, mkoani Iringa. Ingawa suala hilo limetikisa vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, na pamoja na Rais wetu huwa anakuwa mwepesi sana wa kutuma salaam za rambirambi, kwa misiba mbalimbali, lakini kilichowashangaza wananchi, ni namna alivyokaa kimya kabisa, bila kusema chochote, kwa jambo hilo zito, lillotokea.

Siamini kuwa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, ataamua kutoliongelea, hasa tukitilia maanani kuwa, kwa mazngira ya kifo cha Mwangosi kilivyotokea, kuna shinikizo kubwa kwa kutakiwa kuwajibishwa baadhi ya vigogo wa Polisi.

Suala la pili linahusu ripoti ambayo ilitolewa mwezi wa 6 mwaka huu na Benki kuu ya Uswisi kuwa wapo vigogo kadhaa, ambao wameficha kwenye nchi hiyo, pesa zinazofikia shilingi bilioni 315, kwa kuwa tokea itolewe taarifa hiyo, tulisikia kauli ya mkurugenzi wa Takukuru, akiahidi kulifuatilia suala hilo, na ikithibitika ni kweli wawafichue watu hao na kuwafikisha kwenye, vyombo vya sheria.

Tokea kipindi hicho, hatujasikia lolote, hadi majuzi, majina ya wale wanaosadikika kuficha mabilioni hayo, kuwekwa mtandaoni, na kwa kuwa miongoni ya hayo majina 30 yaliyotajwa, limo la JK na mwanae Ridhiwani, naamini Rais, ataona umuhimu wa kutoa ufafanuzi wa suala kubwa kama hilo.

Vile vile, kwa kuwa inafahamika hotuba za Rais, huwa zinaandaliwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, ambaye naamini, anapita sana humu jamvini JF.

Naamini katika uandishi wa hotuba ya Rais, ya mwisho wa mwezi, hawezi kuacha kutolea ufafanuzi, masuala hayo mazito sana, yaliyolikumba Taifa letu, katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Wananchi tunaisubiri kwa hamu sana, hotuba ya mwisho wa mwezi
 
Unasahau kuwa huyu ni mheshimiwa dhaifu?unategemea uthabiti kutoka kwa mtu dhaifu?sina sababu ya kusubiri jibu ambalo tayari ninalo.
 
hana jipya huyo...aendelee kucheza kidali poo na mkewe huko...hatuna rais hapo...
 
Muheshimiwa umesahau kuingiza suala la kufungwa kwa ubalozi wa America sijui kama atatoa tangazo lasrmi la kuufunga au tutegemee kauli ya "SERIKALI SIKIVU IMELISIKIA NA INALIFANYIA KAZI"
 
Mkuu inaonekana wewe umeingia hapa JF mwaka huu. Ukiangalia issue hizi utagundua kuwa zipo tangu miaka na miaka hakuna litakalofanyika, zaidi ni kuwa watu watazugwa hakuna la maana litakalofanyika.

Kwakuwa ni wewe umeanzisha thread hii, subiri usikie kitakachosemwa (kama kikisemwa) halafu uone kama kuna lolote litafanyika.
 
huyo huwa hana mtihani mzito wala mwepesi!!
Tegemea yale yale majibu rahisi ktk swali gumu.
 
Mkuu usipoteze muda wako juu ya huyu mkwe.re, tumeshalamba ghalasa...
 
Mkuu hivi unafikiri huyu bwana anaweza kuwa na mtihani mzito? Kwake hakuna kitu kigumu, ni kawaida ukiona mwanafunzi kila anapotoka kwenye chumba cha mtihani anasema "huu mtihani haukuwa mgumu hata kidogo" ujue amefeli sana. Huyu bwana kila kitu ni rahisi tu kwasababu yeye mwenyewe ni DHAIFU!!!!
 
Kwa nini asiongee, atajisemea tu ilikuwa bahati mbaya maana kazi ya polisi si kuua bali ni kulinda raia
 
Hakuna lolote la maana atakalosema, sana sana anaweza kuahirisha kuhutubia na kama akihutubia utasikia maelezo ya kisaniisanii kama haya:

1/Daraja la kigamboni.

2/Mradi wa mabasi ya kwendakasi Dar.

3/Kitisho cha mvua za El-nino

4/Hali ya uchumi na chakula nchini.

5/Mradi wa vitambulisho vya taifa(Updates)

6/Mchakato wa katiba mpya(Updates)

7/Feedback ya kufanyika kwa mtihani wa darasa la saba

8/Msisitizo wa kupigia kura vivutio vya utalii(Mt. Kilimanjaro, Ngorongoro)

9/Suala la mauaji ya mwangosi lakini kwa lugha ya kisanii sana(eg. Rambirambi!!, Liko mahakamani, Tusubiri report ya kamati)

10/Mgogoro wa ziwa Nyasa(Updates)
 
Kama ni mtihani keshafeli huyo. Huwa hataki jambo la kufikirisha ubongo!

Any way do we really need him or his words on any of recent itching issues? I doubt.
 
Vipi hautabiri kuwa ataongelea kifo cha muuza magazeti Ally wa Morogoro?
 
Hawezi kuongelea masuala kama hayo,anaweza akaongelea masuala haya,kwanza daraja la kigamboni,mabasi yaendayo kasi,chuo kikuu cha jeshi pamoja na kuwashangaa"wahuni" waliomzomea pidapinda pale mwanza badae mtaona ving'ora vinaelekea uwanja wa jk nyerere akapumzike canada baada ya kazi ngumu.
 
Kwa kuwa imekuwa kawaida yake, Rais wetu Jakaya Kikwete, kulihutubia Taifa, kwa njia ya Televisheni na Redio, kila mwisho wa mwezi, kwa lengo la kutolea ufafanuzi masuala mazito yaliyolikumba Taifa katika kipindi cha mwezi mzima.

Natabiri kuwa hotuba ya mwisho wa mwezi huu, inaweza kuwa na wasikilizaji na watazamaji wengi, kuliko hotuba yoyote aliyowahi kuitoa Rais, tokea aina hiyo ya kuwasiliana na wananchi, alipoianza mwaka 2006! Nasema hotuba hiyo inasubiriwa kwa hamu na mamilioni ya wananchi kutokana na matukio makubwa yaliyojitokeza mwezi huu.

Ingawa yapo mambo mengi yaliyotokea, mimi nitayataja mawili ambayo nayaona yametawala vyombo vya habari mwezi huu. Suala la kwanza, ni kuuawa na polisi, kwa mwanahabari wa channel ten, mkoani Iringa. Ingawa suala hilo limetikisa vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, na pamoja na Rais wetu huwa anakuwa mwepesi sana wa kutuma salaam za rambirambi, kwa misiba mbalimbali, lakini kilichowashangaza wananchi, ni namna alivyokaa kimya kabisa, bila kusema chochote, kwa jambo hilo zito, lillotokea.

Siamini kuwa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, ataamua kutoliongelea, hasa tukitilia maanani kuwa, kwa mazngira ya kifo cha Mwangosi kilivyotokea, kuna shinikizo kubwa kwa kutakiwa kuwajibishwa baadhi ya vigogo wa Polisi.

Suala la pili linahusu ripoti ambayo ilitolewa mwezi wa 6 mwaka huu na Benki kuu ya Uswisi kuwa wapo vigogo kadhaa, ambao wameficha kwenye nchi hiyo, pesa zinazofikia shilingi bilioni 315, kwa kuwa tokea itolewe taarifa hiyo, tulisikia kauli ya mkurugenzi wa Takukuru, akiahidi kulifuatilia suala hilo, na ikithibitika ni kweli wawafichue watu hao na kuwafikisha kwenye, vyombo vya sheria.

Tokea kipindi hicho, hatujasikia lolote, hadi majuzi, majina ya wale wanaosadikika kuficha mabilioni hayo, kuwekwa mtandaoni, na kwa kuwa miongoni ya hayo majina 30 yaliyotajwa, limo la JK na mwanae Ridhiwani, naamini Rais, ataona umuhimu wa kutoa ufafanuzi wa suala kubwa kama hilo.

Vile vile, kwa kuwa inafahamika hotuba za Rais, huwa zinaandaliwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, ambaye naamini, anapita sana humu jamvini JF.

Naamini katika uandishi wa hotuba ya Rais, ya mwisho wa mwezi, hawezi kuacha kutolea ufafanuzi, masuala hayo mazito sana, yaliyolikumba Taifa letu, katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Wananchi tunaisubiri kwa hamu sana, hotuba ya mwisho wa mwezi

Kwanza ndio atauliza kama ndege ina mafuta then aendelee kutalii bado hajamaliza vijiji vya china.
 
Back
Top Bottom