Makamu wa Rais anaeweza kukaa nje ya nchi kwa mwezi mmoja kwa shughuli maalamu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,027
144,381
Naomba kufahamishwa inawezekana vipi mtu mwenye wadhifa wa Umakamu wa Rais kukaa nje ya nchi kwa mwezi mmoja eti kwa shughuli maalumu.?

Hata Katibu Mkuu tu wa wizara ni nadra kuweza kukaa mwezi mzima, sasa iweje kwa Makamu wa Rais?

Ni kazi gani hiyo?

Makamu wa Rais anaweza kuwa mtendaji wa kuwa na kazi ya kumuweka nje ya nchi kwa mwezi mzima?

Kwa nafasi yake, ni msaidizi wa Rais, mtu wa kusimamia sera, sasa nini kinaweza kumuweka nje ya nchi kwa muda wote huo?

Maswali ni mengi kuliko majibu.
 
Hapa kuna wanaotaka iwe makamu wa Rais alikuwa mgonjwa, na wengine wanasema hakuwa mgonjwa alikuwa nje kwa shughuli maalum.

Naamini hiyo yote inasababishwa na nafasi yake aliyonayo, watu wana haki ya kuhoji wapi alipo kiongozi wao, serikali inayosababisha ligi kwa kutuficha sababu ya kutoonekana kwake ndio inatukosea.

Makamu wa Rais ana bahati mbaya sijui kwanini haya makelele humkuta yeye, nakumbuka hata wakati ule wa Magufuli pia aliletwa kuongea na waandishi wa habari huku hali yake ikiwa haijakaa sawa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Naomba kufahamishwa inawezekana vipi mtu mwenye wadhifa wa umakamu Raisi kukaa nje ya nchi kwa mwezi mmoja eti kwa shughuli maalumu.

Hata Katibu Mkuu tu wa wizara ni nadra kuweza kukaa mwezi mzima sasa iweje kwa makamu wa Raisi?

Ni kazi gani hiyo?

Makamu wa Raisi anaweza kuwa mtendaji wa kuwa na kazi ya kumuweka nje ya nchi kwa mwezi mzima?

Kwa nafasi yake, ni msaidizi wa Raisi, mtu wa kusimamia sera, sasa nini kinaweza kumuweka nje ya nchi kwa muda wote huo?

Maswali ni mengi kuliko majibu.
.
Watanzania tumezoea kudanganywa na kuzuiwa kuhoji. Tuna viongozi wenye akili ya kawaida sana ila wakiwa madarakani wanajiona wana akili sana kuliko watu wote. Haiwezekani makamu akawa nje ya nchi kwa zaidi ya mwezi kwa kazi isiyojulikana. Je leo mbona mke wake hakuonekana kanisani? Wazazi wa wajukuu zake walikuwa wapi? Alipoona uzushi kwenye mitandao alichukua hatua gani......
 
Hapa kuna wanaotaka iwe makamu wa Rais alikuwa mgonjwa, na wengine wanasema hakuwa mgonjwa alikuwa nje kwa shughuli maalum.

Naamini hiyo yote inasababishwa na nafasi yake aliyonayo, watu wana haki ya kuhoji wapi alipo kiongozi wao, serikali inayosababisha ligi kwa kutuficha sababu ya kutoonekana kwake ndio inatukosea.

Makamu wa Rais ana bahati mbaya sijui kwanini haya makelele humkuta yeye, nakumbuka hata wakati ule wa Magufuli pia aliletwa kuongea na waandishi wa habari huku hali yake ikiwa haijakaa sawa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Chukua maua yako Mkuu.
 
Mwacheni mzee wa watu apumzike na uchovu wa safari.

Cha msingi tunakubaliana kwamba alikuwa nje ya nchi.

Sasa kama alikuwa kikazi au vinginevyo, siyo kazi yenu!

Kwani wewe ukienda mjini kufanya kazi si unaweza ukapitia sehemu ukafanya jambo tofauti na lililokupeleka?
 
Back
Top Bottom