Mtei kasema UKWELI ULIOSHINDWA KUTAMKIKA, tuache unafiki!

Tuache udini! Nani kati ya hao mnaowasema ni muislamu na hana sifa ya kuwa kiongozi ktk nafasi yake? Hiyo tume inaongozwa na viongozi waikristo sidhani kama akina Warioba na Jaji mstaafu watakubaliana na hoja yoyote ile yenye chembe chembe za udini. Pili hii tume imeundwa kutokana na majina yaliyoteuliwa na taasisi mbalimbali sasa kama Zanzibar hakuna taasisi au Asasi yyoyote iliyoteuwa majina ya waikristo ni nani wa kulaumiwa?

Tuiombee mungu tume ifanye kazi yake ila kama itapendelea upande wowote basi ndio tuanze kuionyoshea kidole.
 
Zitto ameitetea CHADEMA vizuri sana kuliko wengi wenu mnavyoweza kudhania,KAMA TUKITUMIA VIGEZO ALIVYOWEKA MZEE MTEI NADHANI WA KWANZA KWA UDINI NA UKANDA WANGEKUWA CHADEMA,ASILIMIA YA VIONGOZI WAKRISTO WALIOKO CHADEMA WANASHINDA ASILIMIA YA WAJUMBE WAISLAM WALIOKO KTK TUME!KWA HIO KAMA TUME YA DINI MOJA NA CHADEMA NI YA DINI MOJA VILEVILE,WA TZ TUWE NA MUONO WA MBALI KABLA YA KUSHABIKIA MAMBO.
 
Kwamfano umebakia kumwita mzee Mtei mdini na wakati hujasema kama ni kweli ama si kweli kuwa mawazo ya Ar-nuur yameonekana kufuatwa?


Mkuu JM1 nimemuita mdini rejea kwenye ule uzi wake .. nadhani post yangu ilikuwa ya 3 kupingana na kile alichokiandika na pia serikali ni kubwa sana, serikali sio JK peke yake, wala wabunge wake, mpaka JK ametua yale majina kutakuwa na vigezo alivyopitia na sidhani serikali huwa inaendeshwa kwa maoni ya waandishi wa magazeti ..! mwandishi wa ar-nuur hakutoa mawazo yoyote zaidi ya maoni yake yeye mwenyewe na kanzu yake aliyovaa hiyo siku akiandika yale maoni yake.

Na kama ingekuwa the other way around, yani wangekuwa wakristo wengi zaidi, si kungekuwa na malalamiko?

Of course kwa tanzania bara tume ina wakristo wengi kuliko waislam...?! je umesikia ndugu zetu waislam wabara wakilalamika..?! sababu wenyewe wanapigania kadhi upande wa bara .... nadhani sasa wame giveup . hapa usiichukulie tanzania kama nchi moja. chukulia tanzania ni muungano wa NCHI MBILI TOFAUTI.

Hata wenye kusema Tanganyika tume ina wakristo wengi, waki balance hilo na Zanzibar watabalance?

sijajua ni vigezo gani vimetumia kuchagua ila nadhani kigezo kimoja ni uzoefu katika nyanja ya siasa na sheria!... Je jiulize politicians wa kizanzibari kuna mkristo..?! kama wapo ni wangapi.. you can not just pick any one from michenzani streets just bcz his name is joseph and he is zanzbarian kumbuka majority ya wazanzibar ni tuseme 98% ni waislam Je mkuu inamaana ulitarajia hili jambo lichukuliwe kidini zaidi ya vigezo!. Na pia nina uhakika majina kutoka zanzbar yalipendekezwa na wazanzibar wenyewe.. maybe kupitia baraza lao la wawakilishi..!? udini wa JK unaingia wapi hapo..?!

kumbuka zanzibar ni nchi sidhani kama wangekubali JK mwenyewe awataulie yale majina bila serikali ya mapinduzi ya zanzbar kuwa consulted first! so majina yaliotoka zanzbar yamependekezwa na wazanzbar wenyewe ambao asilimia kubwa ni wa dini moja.

Chadema kama kweli tunahitaji kuiondoa CCM madarakani.... basi kuna vitu vinatakiwa kuwa adjusted .... aim glad viongozi wa CDM walitoa tamko wakasema yale ni maneno ya MTEI na wala si msimamo wa chama kwani it was totaly very low from him.

Mzee Mtei namkumbusha maneno ya Mahatma Gandhi and i quote "I suppose leadership at one time meant muscles; but today it means getting along with people"hapo kwenye RED panahusika sana
 
Mkuu usiendelee na upuuzi wa mbuni kuficha kichwa na kuacha mwili wote nje! CHADEMA ndiyo issue hapa! Pengi angesema haya watu wangejadili katika muktadha mwingine! Na hakuna mtu
angesema 'amefilisika'! Issue ni INAKUWAJE CHAMA CHA SIASA KITETEE MASLAHI YA DINI FULANI? AU KWA NINI CHADEMA IONE WAISLAMU WENGI NI TATIZO KWENYE TUME YA KATIBA?


Wewe unafikiri kwa nini CHADEMA isione kuwa na Waislamu wengi ni tatizo,unataka taifa hili lisilimishwe? Idadi ya Wajumbe Kiimani ilitakiwa iwe sawa,Kwa uwakilishi wa Bara na Visiwani,Bara waliihitaji uwakilishi Mpana zaidi kuliko visiwani!!
 
Mkuu nimependa hizo takwimu zako naona ni mzuri kwenye mambo ya takwimu naomba unasaidie na hizi takwimu.

Kwa nini wabunge wa Chadema viti maalum wengi ni Wakirsto?

Kuna wabunge 25, Wakirsto ni 19 na Waislam ni 6 tu.

Mlitumia vigezo gani kuwapata hawa wabunge?

Mkuu kwa huku bara ukitazama hilo unalolitazama yakubidi uwe fair hata kwa CCMatusi. Angalia wabunge wa CCMatusi wa kuchaguliwa, 90% ni WAKRISTO. Wa viti maalum nadhani 90+% ni wakristo. Sijajua kwa KAFU maana hata yule mama wa Tabora mwenye lafudhi ya Kichagga namwona ana doa jeusi kwenye paji la uso.
 
mkuu ni kawaida yetu kusahau na kuchangia bila kujali mada halisi ya mleta hoja.

Soma posti ya kwanza halafu majibu ama maswali yako yatokane na hoja zake.

Kwamfano umebakia kumwita mzee mtei mdini na wakati hujasema kama ni kweli ama si kweli kuwa mawazo ya ar-nuur yameonekana kufuatwa?

Na kama ingekuwa the other way around, yani wangekuwa wakristo wengi zaidi, si kungekuwa na malalamiko?

Hata wenye kusema tanganyika tume ina wakristo wengi, waki balance hilo na zanzibar watabalance?

Kuna maswali kama hayo ambayo yanauathiri uhusiano wa muungano wetu na usalama wake.

jmushi1 usiwe mpenzi wa mtu/dini vikakufanya kuwa blind!- maana ya busara ni kutenda, kunena mambo fulani kwa akili na kwa wakati wake, ukweli peke yake siyo justification kutamka mtu!. Mathalani jambazi wanavamia nyumba yenu na mzee anajificha chini ya uvungu, wanakuuliza mzee yuko wapi, kuwa honest, wewe utawaeleza mzee alipo eti kwa sababu unasema ukweli?- je katika familia mathalani unakuja kudokezwa siri kwamba mmoja wa ndugu zako siyo mtoto wa baba yako, siku mgeni akitembelea kwenu akakuomba utambulisho wa ndugu zako utasema ukweli "kwamba lakini huyu fulani si mtoto wa baba, mama alipitia nje?".

Kuna wakati mwalimu nyerere akiitolea ufafanuzi ishu za uteuzi wa viongozi kwenye serikali yake akasema kwamba kipindi wakati huo anateua alikuwa haangalii kabisa dini zao, bali alikuwa anaangalia utendaji wao- ni dhahiri basi wakati huo kwa watu wenye muono kama wa mzee mtei, walikuwa wanaona nyerere mdini.

Jmushi1 tumeshaona teuzi nyingi nchini, kuanzia wagombea ubunge, wakuu wa mikoa, mabalozi, tume zilizopita na nakuhakikishia mara nyingi sana wakiristo ni wengi kuliko waislamu, hebu niambie honestly baadhi ya waislamu walipokuwa wakilalamika wamekuwa wakijibiwaje?- kwamba wamesema ukweli na hivyo wako sawa, au kwamba teuzi haziangalii dini bali utendaji?

Usiwe blind jmushi1- udini ni pale unapoliangalia kila jambo kidinidini wakati kumbe huyo unayemdhania anatenda udini wala hafikirii kabisa jambo hilo.

Unazungumzia kubalance kati ya waislamu na wakiristo kwa pande zote mbili. Hebu piga mahesabu mwnyewe, tanzania bara kwa logic yako ilistahili waislamu wengi zaidi ya hao iliowapata maana inasemekana waislamu wa tanganyika ni almost sawa na wakiristo na kuna sehemu nyingine nimesoma wanasema waislamu ni wengi kidogo kuliko wakiristo.

Zanzibar ukiangalia percentagewise ni dhahiri hata ukijaribu kubalance yaani utakuta waislamu bado ni wengi kuliko wakiristo. Cheki mwenyewe kwa kuchukua 1% uzidishe na wajubmbe kutoka zenji uone watakuwa wangapi dhidi ya wale 99%.

At the end of the day tukifanya haya mambo kidinidini, kwa kuwa kila upande wa muungano unatoa wajumbe kwa usawa, always waislamu watakuwa wengi kuliko wakiristo kutokana na factor ya zanzibar. Lakini tukifuata vigezo vingine tofauti, sura ya teuzi inaweza kuchukua form ya aina yoyote ile.
 
Kuna udini kweli unainyemelea tanzania, vyama kama Chadema vinalalamikiwa kuwa na viongozi wengi wa kikristo, CUF ina lalamikiwa kuwa na viongozi wengi wa kiislamu NA ccm inalalamikiwa kutumia udini wakati wa uchaguz kupata kura. Pia ukisikiliza baadhi ya redio za kidini ni hatari hatari! Kazi si kuhubiri tena bali ni kushambulia upande mwingine wa dini. Mbaya zaidi tuna rais dhaifu!
 
Zitto ameitetea CHADEMA vizuri sana kuliko wengi wenu mnavyoweza kudhania,
Kauli ya Zitto ndio kauli ya Chama. Hakuna aliyempinga Zitto na sidhani kama kuna aliye timamu atakayempinga Zitto. Ukweli ni kuwa Kauli ya Mtei ni maoni yake binafsi sio maoni ya Chama. Lakini alichokisema Zitto ni nadharia ya kufunika kombe. Mtei ana hoja na huo ndio ukweli.

ngozimbili said:
KAMA TUKITUMIA VIGEZO ALIVYOWEKA MZEE MTEI NADHANI WA KWANZA KWA UDINI NA UKANDA WANGEKUWA CHADEMA,ASILIMIA YA VIONGOZI WAKRISTO WALIOKO CHADEMA WANASHINDA ASILIMIA YA WAJUMBE WAISLAM WALIOKO KTK TUME!KWA HIO KAMA TUME YA DINI MOJA NA CHADEMA NI YA DINI MOJA VILEVILE,WA TZ TUWE NA MUONO WA MBALI KABLA YA KUSHABIKIA MAMBO.
ungeshirikisha ubongo kabla hujapost huu upuuzi. Inamaana CUF ni chama cha Kikristo? Na CCM je ambacho 90+% ya viongozi ni wakristo utakiitaje?
 
Mkuu kwa huku bara ukitazama hilo unalolitazama yakubidi uwe fair hata kwa CCMatusi. Angalia wabunge wa CCMatusi wa kuchaguliwa, 90% ni WAKRISTO. Wa viti maalum nadhani 90+% ni wakristo. Sijajua kwa KAFU maana hata yule mama wa Tabora mwenye lafudhi ya Kichagga namwona ana doa jeusi kwenye paji la uso.

Mkuu umeshindwa kabisa kutupa vigezo mlivyotumia kuchagua wabunge wa viti maalum Wakirsto 19 na Waislam 6 tu.
 
...Kwa mchanganuo huo maslai ya waislamu yataingia kwenye katiba mpya. Kwani 75% ya wajumbe watakuwa waislamu na25% tu ndio wawe wakristo. Ila moja ya dai kuu la waislamu ni nafasi sawa za uongozi, mahakama ya kadhi na kupinga mfumo kristo. Hawana habari juu ya ufisadi mfumo mbovu wa elimu, huduma duni za afya, rushwa na mfumuko wa bei...

Hao 75% ya tume wanachangamoto ya ku-prove hii assertion (red) kuwa ni potofu. Watunge katiba kwa ajili ya Watanzania wote, na waepuke kishawishi cha kuona hii fursa kuwa ni wakati muafaka wa "ku-revenge"
 
kweli kazi ipo...waislam wakristo, waislam wakristo..ukitaka kuanza kuteua kwa kuangalia idadi sawa ya udini basi huo ndio mwanzo wa udini, haiwezekani mtu ashindwe kuteua watu flan hata kama wanauwezo eti kisa ni wa dini flan, raisi kateua tume kulingana na uwezo wa mtu husika suala la dini umeliona wewe na mtei baada ya kuanza kuhesabu wateuliwa kwenye hiyo tume na ulipoona wengi ni waislam basi ukakurupuka na hoja udini, vipi ungekuta wakristo ni wengi ungesema? au babaako mtei angesema? rais hawezi kushinikizwa wala kufuata matakwa ya taasisi ya dini wala mtu flan huo ni mtizamo wa kibinafsi..hoja yako ya udini katika tume wala siikubali...
 
Mzee Mtei has a full right to give out his opinions because he is a tanzanian like others and he should speak out what he saw is ok to say. It is true that the commision comprising a lot of muslim members even if you argue against this point but the truth remain the same. Let us now give them assistance while awe re taking care, once we see there is some sort of religiouslism tanzanians dont hestate to revoke out, dont be silence for things which may put our country into controvercial. GOD BLESS TANZANIA.
 
kweli kazi ipo...waislam wakristo, waislam wakristo..ukitaka kuanza kuteua kwa kuangalia idadi sawa ya udini basi huo ndio mwanzo wa udini, haiwezekani mtu ashindwe kuteua watu flan hata kama wanauwezo eti kisa ni wa dini flan, raisi kateua tume kulingana na uwezo wa mtu husika suala la dini umeliona wewe na mtei baada ya kuanza kuhesabu wateuliwa kwenye hiyo tume na ulipoona wengi ni waislam basi ukakurupuka na hoja udini, vipi ungekuta wakristo ni wengi ungesema? au babaako mtei angesema? rais hawezi kushinikizwa wala kufuata matakwa ya taasisi ya dini wala mtu flan huo ni mtizamo wa kibinafsi..hoja yako ya udini katika tume wala siikubali...
 
Point iliyotumika ni 1. wengi wa kura alizopata mgombea urais kwenye eneo husika 2. Mchango wa mchaguliwa mwenyewe kwa chama kwa kipindi cha nyuma 3. sifa za mchaguliwa mwenyewe binafsi zamchaguliwa (kulingana na vigezo vya utawala bora) 4. Uwezo wa kujenga hoja 5. uwezo wa kuwasaidia wanachi 6. uhakikika wa kuwa si pandikizi la mafisadi/magamba wa vibaraka wao. 7. Waliojitokeza pia kuomba kuchaguliwa kwenye hizo nafasi.

Tuikomboe nchi yetu toka mikononi mwa Mkoloni wa ccm(MAFISADI) ili tuweze kupata maendeleo ya kweli
 
kwa malumbano haya katiba mpya kuipata ni ndoto ya mchana...kwani nategemea malumbano makali ya udini kuliko lengo halisi la katiba mpya.!
 
Mtei kasema kweli inakuwaje wakristo wakipigia kelele jambo la kutokuwa na usawa katika uwakili wa dini inaonekana ni udini na waislamu wakipiga kelele inaonekana ni haki? mfano Sumaye alipounda bodi ya parole wakrsto walikuwa wengi na waislamu walipiga kelele jambo lililofanya ikavunjwa hiyo bodi na kuundwa upya kwanini hapa kwenye katiba ionekane ni udini wakati ni haki?

Haiwezekeni Zanzibar wawe wote ni waislamu wakati kuna makanisa Kikwete kashindwa kuteua wakristo walioko Zanzibar? mbona Jaji Agustine Ramadhani au Issack Sepetu ni wakristo ambao asili yao ni Zanzibar wanopinga hoja wanataka kusema wakristo Zanzibar ni wawili tu Jaji Ramadhani na Sepetu? kama ni hivyo hayo makanisa yaliyoko Zanzibar wanaosali ni waislamu? kama sio waisilamu wanaosali sasa inakuwaje wakose hata wajumbe watatu wakristo toka Zanzibar?

Haya ndio mambo yaliyopo kwenye kamati kuu ya CCM pia ambayo ina wajumbe 32 kati ya hao wakristo ni 9 tu na 21 wote ni waislamu sababu ya 'Zanzibar equation" ndio maana napenda muungano uvunjike na ninamlaumu Nyerere kwa huu Muungano ingawa mimi ni mshabiki wake mkubwa maana muungano unawapa waislamu mamlaka makubwa wakati wao sio wengi kama wakristo Zanzibar isingekuwepo tungekuwa sawa kwa sawa angalia mfano wa Rais na Makamu wa Rais wao waislamu wanaweza kutoa Rais na makamu wote waislamu lakini wakristo hawawezi kufanya hivyo maana wakifanya hivyo tu tayari hoja ya udini inakuja

Hapa Waislamu wote watanyamaza na kupongezana bahati mbaya tuu wale wasiasa kali hawapigi kilauri...Binafsi sijafurahishwa na ratio ya Tume wala issues on relious composition
 
Ni aibu kubwa kusema tunamkuu wa inchi katika hali kama hii akidekeza udini badala ya kuhakikisha watu wake wanakuwa na maisha bora na wanaishi kwa umoja wao bila kujenga matabaka ya

1. udini
2. Utajirisho wa wezi mafisadi
3.Elimu ya watoto maskini shule za kata na elimu za watoto wa wezi mafisadi kama ile ya feza
3.matibabu ya maskini katika hospitali zisizo na madawa wala vitendea kazi na mishahara bom kwa madakitari ikiwa wanasias na wezi mafisadi hata maumivu ya kidole matibabu India.


Siku zote kila lililo na mwanzo linamwisho, lakini mwisho wa mkuu wetu si mzuri kamwe maana anailekeza inchi katika vita mbaya kabisa ya udini. Kila mpenda amaniakemee mgawanyo huu na upendeleo wa kipuuzi

50% kutoka tanganyika yenye zaidi ya watu milion 40 na ukubwa wa eneo zaidi ya mara hamsini ya zanzibar ambayo nayo inatoa 50% kwenye michakato mbalimbali haileti maana wala mantiki.

Hivi katika pato la taifa zanzibar inachangia nayo 50%? au wao nika makinda ya ndege kubewa na muda wote kwa kuhofia kelele zao?

Na Tunaviongozi wangapi wanaongoza viwani wakitokea bara (tanganyika) kama ilivyo kwa wazanzibar wanavyotuongoza
1. waziri wa ulinzi Mzanzibar
2. Waziri wa mambo ya ndani Mzanzibar
3. Makamo wa rais Mzanzibari
4. unaweza kuendeleza idadi.......

Kama ndivyo muungano uvunjwe hauna maana wala faida kwa watanganyika zaidi ya kututia hasara na na kutuvurugia uchumi wetu amani yetu an utulivu wetu ona sasa udini unaingia kwa mlango wa uzanzibar.
 
Ukitaka kuanza kuteua kwa kuangalia idadi sawa ya udini basi huo ndio mwanzo wa udini, haiwezekani mtu ashindwe kuteua watu flan hata kama wanauwezo eti kisa ni wa dini flan, raisi kateua tume kulingana na uwezo wa mtu husika suala la dini umeliona wewe na mtei baada ya kuanza kuhesabu wateuliwa kwenye hiyo tume na ulipoona wengi ni waislam basi ukakurupuka na hoja udini, vipi ungekuta wakristo ni wengi ungesema? au babaako mtei angesema?

Hoja ya idadi ya wajumbe kwa imani zao ilitolewa mwanzo na balaza la maimamu na radio imani na magazeti ya el-nuur

Pili je nisahihi waislam kuomba 50% bara wakati idadi yao ni chini ya 20% bara. Mikoa yenye waislamu wengi kwa bara ni Tanga, pwani, Mtwara, Lindi tu. Dar kunawageni wengi sasa idad ni sawa. Vip 50%?

Uliza maustadhi wakuambie habari za Marca. Mwanzo waislamu walikuwa 20% na mtume akaongoza kuandikwa katiba maswala ya uongozi kwa idadi hayakuwepo swala ni kuaminiana.

Inshu hapa ni kwamba kunabaadhi ya madai yasiyo ya haki ambayo baadhi ya wasioelewa uislamu wanayapigania
Mfano: Mahakama ya kadhi si kitu kibaya kama wengi wanavyodhani kwani inahusu mashwala ya miradhi na ndoa kwa waumini wa kieslamu tu. Ila ubaya wanataka Majengo, Mahakimu na uendeshwaji ugaramiwe na selikali. Je waislamu wachamungu hawawezi kuchangia uendeshwaji wake?

Kuna inshu za Shule za sec za selekali zilizokuwa za makanisa kama Nganza, Nsumba, Kahororo na Minaki zina Makanisa ya zamani pia. Wanalazimisha zijengewe misikiti na selikali! Je waumini wanafunzi wa makanisa mengine
yasifungamana na kanisa lililopo wajengewe makanisa pia? Na wakristo wakidai shule zao itakuwaje.

Kuna inshu ya misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini zinazotoa huduma na haziko kibiashara kama Hosptal za Bugando, KESMC, Aghakani tena zinaudumia bila ubaguzi wa dini. Eti nao wanaomba wapate fear hizo japo hawana hosptal. Ila wanauza jina la BAKWATA kwa wafanyabiashara ili wakwepe kodi. Hizo za BAKWATA misikiti haijui ata uendeshaji wake. NaUNAFIKI WA MKULO HUKU AKIJUA HILI AKAJA NA MPANGO WA KUTOA MSAMAHA WA KODI kwa asasi za makanisa.

WASIOJUA WANAPOTOSHA JUU YA IMANI YA UISLAMU.
Ukifuatilia historia ya MTUME Alipenda amani. Fuatilia juu ya uundwaji wa katiba ya maka. Aliheshimu watu wote. Alitumia busara sana na si nguvu.

Narudia chimbuko la dini zote mbili ni IBRAHIMU. Ila wote tu wamoja ni bora tuungane tupambane na maadui wa kweli UJINGA UMASIKINI RUSHWA MAOVU KATIKAJANII MFUMO MBOVU WA ELIMU TOFAUTI KUBWA ZA KIPATO UONGOZI MBAYA.

Nchi inayumba kwa uteuzi usizingatia uwezo bali urafiki udini na matabaka.
ONA MUSTAPHA mkulo uchumi hoi
OMARI NUNDU na mgomo wa madaktari
VUAI NAHODHA na magari ya maji ya kuwasha na kupiga raia
ELIMU walimu madai yasiyoisha na kufaulu wasiojua kusoma na ajira za walimu mpaka maandamano

OMARI NUNDU wapi Meli Ndege na Reli?
Ngeleja? Labda H Mwinyi
UMEFIKA WAKATI WA KUHOJI LAZIMA TUHOJI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom