Interested Observer
JF-Expert Member
- Mar 27, 2006
- 2,665
- 3,048
- Wakuu samahani sana naomba kuuliza swali kidogo tu na linaweza kua nje ya mada, hivi kwa standard za ufisadi sasa hivi katika nchi yetu Tanzania, Mzee Mtei binafsi, hawi fisadi pia?
- I mean mali yote aliyonayo ambayo aliikusanya akiwa katika uongozi mbali mbali wa taifa letu, ni kweli haina ufisadi kabisaaa? Kama inayo anapata wapi moral authority ya kum-lecture rais wetu wa sasa kuhusu ufisadi wakati yeye ni mmoja wa waanzilishi wa ufisadi, kama sikosei katika taifa letu, au?
- Ninafahamu kwamba aliwahi kufanya kazi nje, lakini hivi mbona hata wakina Dk. Salim, waliwahi kufanya kazi nje lakini hawana mali za ajabu kama za huyu Mzee wetu muhasisi wa upinzani nchini?
- Ahsanteni Ndugu Zangu na Pasaka njema Sana.
William.
Hapana sio kila mtu mwenye mali ni fisadi; huyu ni shujaa, na ana-tofauti kubwa sana na wengine, kama hao ambao huganga njaa kama mzee wetu wa Glasgow.
1. Mtei-Pamoja na cheo chake kikubwa bila ya kujipendekeza kwa Mwalimu alitofautiana na siasa zake (za mwalimu) akaachia ngazi.
2. We understand that others have chosen "to sleep with the devil"; meaning; even if they hated that devil; kwao kuganga njaa ndiyo muhimu zaidi.
3. Huyu jamaa alichagua kuacha cheo na kufanya shughuli zake tangu mwaka 1979; and he was a high profile guy; another example was Justinian Rweyemamu who also diiffered.
We fikiria hawa wazee wetu wangepangana vizuri wawe wanatoa hekima zao kama huyu mzee wangekuwa wapi? Chukulia Mtei, Salim, Mwinyi, Mzee Wa Glasgow, Msuya, na wengine kama wangepangana na kuona "country first" hao mafisadi si wangeogopa?