Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mzee wetu mtei, acha wenzako wafanye kazi, usianze kuwneza udini. Mkapa tulisema anazeeka vibaya, cjui ww tusemeje!!-
 
Mzee Mtei kazeeka vibaya.
Ubongo umechoka ndio maana anaropoka tu
OTIS
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.
ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu! Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?
 
Zitto ni member humu ana faida gani ya uanachama wake kama hawezi jitokeza kukanusha ama kuthibitisha habari hii! Wahenga walisema "kuna wakati saa iliokufa husema kweli"
 
ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu! Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?

Hatima ya mustakabali wa tanzania itaamuliwa na kakundi kadogo sana ka watu zaidi kidogo ya milioni moja dhidi ya milioni 44. Bado hatupo salama. ngoja mlazimishwe kufuga midevu!
 
kama zito yupo hapa jukwaani atueleze kama kwel kasema hvo, kwasababu wengi hawana imani na jambo leo kama inavyoonyesha toka kwenye michango yao...mkuu zito, funguka.
 
Sasa mlivyokuwa mnalalamika CCM inawatukana kumbe ni Mwigulu na Lusinde yalikuwa mawazo yao binafsi.

Ivi unaweza kulinganisha context ya lusinde (kwenye jukwaa la kisiasa)wakati wa kampeni na Katibu mkuu wa chama alipoulizwa akadefend na mawazo ya Mtei (sio kiongozi wa chama) tena akiwa nyumbani kwake??

:focus:
Ivi kawa wewe Ritz ni mrefu nikasema wewe ni mrefu natakiwa kuomba radhi sio?? Hebu geuzia upande wa pili wangekuwa ni kina john wamezidi kwenye hiyo tume si kila ijumaa kungekuwa na maandamano?? Humu si kungekuwa hakutoshi? Shukuruni mungu huu upande wa pili kuna ustaarabu na hata mteuzi najua ameliona hilo.
 
Mzee wetu mtei, acha wenzako wafanye kazi, usianze kuwneza udini. Mkapa tulisema anazeeka vibaya, cjui ww tusemeje!!-

Mzee Mtei has stated a fact kuwa katika tume ile waislam ni wengi kuliko wakristo, sasa bisheni kama hilo sio kweli! Mtu wenu anaeeneza udini mkweree mnaacha kumkalipia mnamsonga mtu mwenye ujasiri wa kusema ukweli; hii yote ni kwasababu nyie watu wa magamba mmezoea unafiki!
 
ZITTO, hana adabu, ukweli unamuuma? Zanzibar haina wakristo? Iweje wajumbe 15 wote wawe waislamu? Hakuna wakristo Zanzibar? Aliyefilisika ni Zitto au Mtei? Sisi tunamheshimu sana mzee Mtei, hivyo tuachie mzee wetu, wewe ukiona umechoka? Sepa! Mnafiki sana wewe.
 
namuunga mkono Mzee Mtei! Sabababu ni zifuatazo:
Kadri kundi moja linavyozid ndivyo na hoja za upande huo zitakapopitishwa kirahisi!
Leo hii tunaona ccm inavyoburuza bunge c ni kwasababu ya wingi wao?
Unategememea ije hoja ya mahakama ya Kadhi hapo mezani itapingwa kweli?
tuombe Mungu aingilie kat bila hivo katiba itakuwa ya mrengo mmoja!
 
Hivi uhuru wa kutoa mawazo unakomea wapi? Mzee Mtei yeye kaangalia vigezo kadhaa mojawapo ni takwimu kwamba wale 15 kutoka Zanzibar wote ni Waislamu na 15 kutoka bara ni 4 yaani zaidi ya 63% ni kutoka dini moja tu. Je mtu katika ubinafsi wapi wake, kuna kosa gani akiuliza kukosekana kwa usawa katika hili?

Katika uteuzi wa tume hii uwazi na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ulikuwa unatakiwa zaidi. Kwa kuwa mtu mmoja tu amepewa dhamana hii tutarajie mapungufu mengi zaidi na zaidi kutoka kwenye tume na katiba yenyewe.
 
Hilo ni tamko rasmi.Hivi matusi ya Lusinde niyake au ya chama? Ufisadi ni wa Mkapa au lowasa na sio CCM?
Inategemea hayo mawazo aliyatolea wapi, pia ukumbuke Mtei hana nafasi ktk uongozi wa CDM. Bado naamini hayo ni mawzo yake binafsi
 
Sasa mlivyokuwa mnalalamika CCM inawatukana kumbe ni Mwigulu na Lusinde yalikuwa mawazo yao binafsi.

Hakuna aliyelalamika kuwa CCM imetukana, bali watu wamelalamika kuwa Lusinde, Mkapa, Wassira wametukana
 
Huyu bwana mdogo anachonifurahisha ni kwamba hajui kumun'gunya maneno, na hicho ndicho kinachowatoa watu roho. Inawezekana kweli kasema hivyo, au pia yawezekana mwandishi kaweka vile alivyoona inampendeza.
Mzee Mtei kweli anazeeka vibaya, maswali yake ya udini hayana tija. Rais alizingatia taratibu? Jibu ni NDIO. Tukianza kuulizana uwiano wa wakristu na waislam mbona sisi wakristu tutaumbuka! Lakini ni kwa ajili tunakuwa tunafit kuwa tulipo, sasa vidole vya nini? Hebu tuache uchochezi wa kidini. Maendeleo yenyewe hatuna, halafu tunataka kuongeza matatizo yasiyo na tija.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Hilo la kufilisika kimawazo ni mawazo ya mwandishi na siyo zitto.
 
ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu! Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?[/QU .... Unamheshim sawa, hata akiongea pumba? Akikuambia kula mavi utakula? Mtei hawezi liona hilo leo. Wakat yuko madarakani alifanya nini kuzuia udini. Tume ni ya kukusanya maon ya watz (c waislam). Kuh znz usiwasemee. Mathematically: 2% of znz christians x 15 apointees = 0.3persons. Ni theluthi ya mtu na c mtu kamili, Labda kibabu chako hicho. Nenda zako!
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Jamani let us be objective! Mtei kakosea wapi. Let us count! Waislamu ni wengi hilo halina ubishi. Amekosea nini sasa. Ila tujiulize, wingi wa waislamu utakuwa na athali zozote katika maamuzi ya tume? Uislamu utaathiri matakwa ya wananchi wakitoa maoni yao? and many more philosophical questions of that nature. Kama hakuna madhara yoyote yanayoweza kutokana na wingi wao, then hakuna shida. Kama wingi wao unaweza kuathiri utendaji (hasa maamuzi) wa tume, then Mtei has a point. Lakini naona haina madhara maana tume haitoa maoni ila inayaratibu!!!
 
Inasikitisha mtu kutumia muda wake kujibu taarifa inayozushwa na hii toilet paper ya magamba JAMBO LEO kuwa Mtei kasema! huwa halina suala lingine lakuandika au kuizushia CDM na watu wenye kuhusiana nayo. Mbona haya ya magamba huwa haliandiki? Kuzusha propaganda kuhusu CDM kila kukicha, Mtei amewasiliana na Toilet Paper hii tu kuelezia msimamo wake kuhusu tume? Mbona magazeti hayajaandika kuhusu suala hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom